Tabia gani hupendi au unapenda ukiwa safarini?

Je, ni Tabia Gani hupendi au unapenda ukiwa safarini

Binafsi Napenda kukaa na binti nikiwa safarini ila asiwe na Smartphone kubwa kunizidi. Utakuta wewe una Tecno pop2 F harafu yeye ana iPhone 13. Yaani unakuwa unaona aibu hata kuitoa.

Unakuta kabinti kanajikuta kako busy na Simu kameweka earphone hakatoi ukikakaribisha mhindi unaona kanatoa earphone sikio moja harafu kanajibu "Ahsante stumiagi mimi" na wakati kanaelekea Usukumani

Binafsi hiyo tabia sipendi
Nikikaajirani na anaerudisha chenji huwa naboweka sana
 
Napenda kukaa siti za mbele,macho muda wote natazama nje kuona milima na mabonde...huku nikiimba wimbo wa tazama ramani kimya kimya
 
Je, ni Tabia Gani hupendi au unapenda ukiwa safarini

Binafsi Napenda kukaa na binti nikiwa safarini ila asiwe na Smartphone kubwa kunizidi. Utakuta wewe una Tecno pop2 F harafu yeye ana iPhone 13. Yaani unakuwa unaona aibu hata kuitoa.

Unakuta kabinti kanajikuta kako busy na Simu kameweka earphone hakatoi ukikakaribisha mhindi unaona kanatoa earphone sikio moja harafu kanajibu "Ahsante stumiagi mimi" na wakati kanaelekea Usukumani

Binafsi hiyo tabia sipendi
Unakakomesha kwa kula na mayai mawili ya kuchemsha halafu unakaambia upepo unakuumiza kifua ndipo unapoachia kitu kinaitwa organic gas from Uvinza
 
Kukaa na mtu anakulakula hovyo, yani yeye mayai ya kuchemsha, karanga, mahindi ya kuchemsha mara ya kuchoma, yeye kila anachoona lazima kipite mdomoni. Mwisho anaanza kubeua na kujamba hovyo.

Sipendi hiyo tabia!
🤣🤣🤣 Hiyo inakera endapo akianza kufanya vitu kama hivyo 🤔
 
Nikae siti ya nyuma ya dereva, ili nione barabara vizuri...tena kwenye basi unakuwa juu dereva anakua chini hivi. Safari inakuwa safi kabisa, uwe umekaa na mdada mrembo pembeni, story mbili tatu basi safari itakuwa nzuri.
Hatari sana Bata zote za safarini unazipitia
 
Kukaa na mtu anauliza uliza maswali sijui tumefika wapi, bado masaa mangapi.

Nimewahi kukaa na mdada huyo anaongea sana asee hadi ikabidi nivunge nimesinzia ila kila nikiamka analianzisha. Nilikereka sana, safari niliona chungu.

NB: Mimi sio mtu wa stori na kujuana juana.
 
Dah kama ni binti wa saizi ungetongoza ili akae kimya
 
Kuna wale wanaongelea kwa sauti mambo ya nyumbani kwao kwenye bus, wanakera sana

Unakuta mama anamwambia binti wa kazi tunakuja tupo njiani, hakikisha umepika hiki na hiki, halafu mjaze maji kwenye jaba eeh

Jana usiku mlikula nini? Hamjanimiss na wanacheka cheka sana

Mara Baba yenu yupo hapo mumpe simu nimsalimie Mume wangu???

Yaani mambo ya nyumbani kwao wanaongea kwa sauti kama vile yanatuhusu na sisi.

K E R O K U B W A
Punguza wivu
 
Back
Top Bottom