Tabia 5 za watu waliofanikiwa ambazo unaweza kuziiga

Mikael Aweda

JF-Expert Member
Dec 17, 2010
2,973
3,901
TABIA TANO ZA WATU WALIOFANIKIWA SANA

Na MIKAEL AWEDA

Kwenye maisha unavuna ulichopanda. Kwa hiyo, ukitaka kuwa na afya njema lazima (panda)wekeza kwenye mazoezi. Ukitaka ndoa nzuri panda uaminifu. Vivyo hivyo, ukitaka kuwa na pesa nyingi lazima upande au ujijengee tabia fulani za waliofanikiwa ili na wewe ufanikiwe kama wao.

Kwa mujibu tafiti mbali mbali zifuatazo ni tabia za kila siku za watu waliofanikiwa. Huu ndio mfumo wao wa maisha ya kila siku. Ni tabia ambazo hata mimi na wewe tunaweza kuziiga. Tabia hizo ni hizi:

Mosi, thamini asubuhi Yako. (Worship your Morning)
Asubuhi akili yako ina nguvu sana, ina 'focus' sana. Asubuhi hakuna usumbufu kabisa. Ndio muda ambao waliofanikiwa kwenye eneo lolote waliutumia vizuri. Muda huu ni *marufuku* kuingia kwenye mitandao ya kijamii. Fanya kitu muhimu kinachoongezea hatua kwenye malengo yako ya siku na malengo yako ya mwaka. Au jipe motisha kwa kisikiliza kinachokujia moyoni. Ndo njia ya waliofanikiwa, na wewe pita humo humo.

Pili, ukiila keki inaisha. Huwezi kula keki na wakati huo huo ikaendelea kuwepo. Haiwezekani! Chagua moja. Huwezi kuendelea na starehe na wakati huo huo unataka kufanikiwa makubwa. Haviendi hivyo. Kama unataka kufanikiwa acha starehe na anasa. Acha kununua vitu visivyo vya lazima.

Acha kula na kunywa kwa anasa. Acha kupoteza muda. Jizuie kujiingiza kwenye vitu visivyo na ulazima kila siku. Mwanzo lazima utoke jasho kidogo. Ndio njia waliyopita waliofanikiwa. Na wewe pita humo humo.

Tatu, ushirikiano (Partnership and Collaboration.)
Watu waliofanikiwa huwa wanashirikiana na wenzao. Wewe siyo malaika. Huwezi kila kitu.
Mwandishi maarufu Mmarekani John C. Maxwell alisema 'One is too small to archieve greatness'. Tafsiri yake ni: 'mtu mmoja ni mdogo sana kuweza kufikia ukuu au mafanikio'. Huo ndo ukweli. Watu wawili wakishirikiana kwa pamoja wanaweza kufanya jambo kubwa kuliko watu watano wanaofanya kila mtu kivyake.

Tatizo ni pale shuleni ulipoambiwa kushirikiana na mwenzako kufanya mtihani pamoja ni kuiba. Ni mbaya na uliadhibiwa. Lakini kwenye maisha halisi ni kinyume chake. Tunashirikiana. Tunasaidiana. Haiwezekani kuwa peke yako. Mnaposhirikiana mnaleta ujuzi na udhaifu wa kila mtu pamoja.

Kila mtu anajazia udhaifu wa mwenzake halafu kitu kikubwa kinatokea. Kwa hiyo, na wewe unaweza kufanya hivyo. Tafuta mshirika wako ili ufikie ukuu. Tunapita humo humo kama wao.

Nne, ukitaka kufanikiwa Kuwa na muda binafsi kila siku (Find Time for Reflection)
Mwanafalsafa mashuhuri, Plato alisema, "un examined life is not worth living". Kwa tafsiri yangu anasema 'Maisha yasiyofanyiwa tathmini hayafai kuishi". Ni muhimu kwa kila mmoja wetu kupata muda wa kutulia na kujitathmini maisha yake. Aangalie anakotoka na anakoenda.

Kama maisha yako ni ya kutoka mapema unaenda kazini na kisha unarudi nyumbani na unaendelea na kazi bila kupumzika na kujitafakari---ni hatari kuliko unavyodhani. Huwezi kujijua bila kujitathmini. Wewe utakuwa kama gari lisilo na dereva. Utakuwa unajiendea bila mwelekeo. Badilika. Wao walitenga muda kidogo wa kujitafakari. Na sisi ili tufanikiwe lazima tupite humo humo.

Tano, Ukitaka kupiga hatua kimaendeleo, Jipe muda wa kutosha kulala. Kuna watu wanasema ili ufanikiwe acha kulala. Siyo kweli. Hatuna utafiti wa waliofanikiwa kwa kuacha kulala au kulala masaa mawili tu kwa siku. Wasomi waliotikisa dunia kama Albert Ainstain alilala masaa kumi. Winston Churchill aliwaruhusu Askari wake kuwa na muda mfupi wa kusinzia mchana japokuwa usiku pia walilala. Wewe ni nani usilale? Lazima upunzike kwa muda wa kutosha ndivyo Mungu alivyotuumba. Siku ina masaa 24 ukilala masaa nane una masaa 16 ya kufanya kazi. Yanakutosha. Kama wao walipata muda wa kupumzika wakafanikiwa na sisi tunapita humo humo.

Ni hitimishe kwa kusema ukitaka kufanikiwa kwenye eneo lolote la maisha yako iwe ujasiriamali au eneo lolote lingine basi tumia vizuri asubuhi yako, acha starehe isiyo ya lazima, shirikiana na wenzako, kuwa na muda wa kujitafakari kila siku na pumzika muda wa kutosha kila siku. Nasi tupite humo humo mpaka kieleweke!

Anza leo, hatua mia huanza na moja.

Mikael Aweda
0784 583 330
Facebook Mikael Aweda
21/05/2020.
 
1.Kuzalisha wanawake wengi
2.Kuimba matusi matusi
3.Kuita media mpaka kwenye kutoa misaada
4.Kugombana na wanaotaka kukufunika
5.kuiba idea za wenzako na kutowapa fadhila

Nimeeleweka au niongeNGEZE SAUTI??.

Ngoja wenye mtu wao waje wakuambie umetumwa na Mawingu Studio au Team Kibamia.
 
TABIA TANO ZA WATU WALIOFANIKIWA SANA

Na MIKAEL AWEDA

Kwenye maisha unavuna ulichopanda. Kwa hiyo, ukitaka kuwa na afya njema lazima (panda)wekeza kwenye mazoezi. Ukitaka ndoa nzuri panda uaminifu. Vivyo hivyo, ukitaka kuwa na pesa nyingi lazima upande au ujijengee tabia fulani za waliofanikiwa ili na wewe ufanikiwe kama wao.

Kwa mujibu tafiti mbali mbali zifuatazo ni tabia za kila siku za watu waliofanikiwa. Huu ndio mfumo wao wa maisha ya kila siku. Ni tabia ambazo hata mimi na wewe tunaweza kuziiga. Tabia hizo ni hizi:

Mosi, thamini asubuhi Yako. (Worship your Morning)
Asubuhi akili yako ina nguvu sana, ina 'focus' sana. Asubuhi hakuna usumbufu kabisa. Ndio muda ambao waliofanikiwa kwenye eneo lolote waliutumia vizuri. Muda huu ni *marufuku* kuingia kwenye mitandao ya kijamii. Fanya kitu muhimu kinachoongezea hatua kwenye malengo yako ya siku na malengo yako ya mwaka. Au jipe motisha kwa kisikiliza kinachokujia moyoni. Ndo njia ya waliofanikiwa, na wewe pita humo humo.

Pili, ukiila keki inaisha. Huwezi kula keki na wakati huo huo ikaendelea kuwepo. Haiwezekani! Chagua moja. Huwezi kuendelea na starehe na wakati huo huo unataka kufanikiwa makubwa. Haviendi hivyo. Kama unataka kufanikiwa acha starehe na anasa. Acha kununua vitu visivyo vya lazima. Acha kula na kunywa kwa anasa. Acha kupoteza muda. Jizuie kujiingiza kwenye vitu visivyo na ulazima kila siku. Mwanzo lazima utoke jasho kidogo. Ndio njia waliyopita waliofanikiwa. Na wewe pita humo humo.

Tatu, ushirikiano (Partnership and Collaboration.)
Watu waliofanikiwa huwa wanashirikiana na wenzao. Wewe siyo malaika. Huwezi kila kitu.
Mwandishi maarufu Mmarekani John C. Maxwell alisema 'One is too small to archieve greatness'. Tafsiri yake ni: 'mtu mmoja ni mdogo sana kuweza kufikia ukuu au mafanikio'. Huo ndo ukweli. Watu wawili wakishirikiana kwa pamoja wanaweza kufanya jambo kubwa kuliko watu watano wanaofanya kila mtu kivyake.
Tatizo ni pale shuleni ulipoambiwa kushirikiana na mwenzako kufanya mtihani pamoja ni kuiba. Ni mbaya na uliadhibiwa. Lakini kwenye maisha halisi ni kinyume chake. Tunashirikiana. Tunasaidiana. Haiwezekani kuwa peke yako. Mnaposhirikiana mnaleta ujuzi na udhaifu wa kila mtu pamoja. Kila mtu anajazia udhaifu wa mwenzake halafu kitu kikubwa kinatokea. Kwa hiyo, na wewe unaweza kufanya hivyo. Tafuta mshirika wako ili ufikie ukuu. Tunapita humo humo kama wao.

Nne, ukitaka kufanikiwa Kuwa na muda binafsi kila siku (Find Time for Reflection)
Mwanafalsafa mashuhuri, Plato alisema, "un examined life is not worth living". Kwa tafsiri yangu anasema 'Maisha yasiyofanyiwa tathmini hayafai kuishi". Ni muhimu kwa kila mmoja wetu kupata muda wa kutulia na kujitathmini maisha yake. Aangalie anakotoka na anakoenda. Kama maisha yako ni ya kutoka mapema unaenda kazini na kisha unarudi nyumbani na unaendelea na kazi bila kupumzika na kujitafakari---ni hatari kuliko unavyodhani. Huwezi kujijua bila kujitathmini. Wewe utakuwa kama gari lisilo na dereva. Utakuwa unajiendea bila mwelekeo. Badilika. Wao walitenga muda kidogo wa kujitafakari. Na sisi ili tufanikiwe lazima tupite humo humo.

Tano, Ukitaka kupiga hatua kimaendeleo, Jipe muda wa kutosha kulala. Kuna watu wanasema ili ufanikiwe acha kulala. Siyo kweli. Hatuna utafiti wa waliofanikiwa kwa kuacha kulala au kulala masaa mawili tu kwa siku. Wasomi waliotikisa dunia kama Albert Ainstain alilala masaa kumi. Winston Churchill aliwaruhusu Askari wake kuwa na muda mfupi wa kusinzia mchana japokuwa usiku pia walilala. Wewe ni nani usilale? Lazima upunzike kwa muda wa kutosha ndivyo Mungu alivyotuumba. Siku ina masaa 24 ukilala masaa nane una masaa 16 ya kufanya kazi. Yanakutosha. Kama wao walipata muda wa kupumzika wakafanikiwa na sisi tunapita humo humo.

Ni hitimishe kwa kusema ukitaka kufanikiwa kwenye eneo lolote la maisha yako iwe ujasiriamali au eneo lolote lingine basi tumia vizuri asubuhi yako, acha starehe isiyo ya lazima, shirikiana na wenzako, kuwa na muda wa kujitafakari kila siku na pumzika muda wa kutosha kila siku. Nasi tupite humo humo mpaka kieleweke!

Anza leo, hatua mia huanza na moja.

Mikael Aweda
0784 583 330
Facebook Mikael Aweda
21/05/2020.

Mwenzetu umeshafanikiwa tayari.kwa kufuata huo ushauri? Mbona sikufahamu? Acheni kutuletea vitu vya kwenye mitandao.kuna watu wana piga party kila siku 90%ya fedha walioipata na maisha wamefanikiwa.

Acha kututisha kama tulivyotishwa na Corona.usipotumia hela haiwezi kukuzoea mkuu.tumia sana upate akili ya kutafuta zingine

*akili za kuambiwa changanya na zako*
 
Sawa mkuu ila kuhusu kulala ni muhimu kwel lakin unapokua ndio unaanza hustlings, usingiz ni adui wa mafanikio makubwa.. Waliofanikiwa wanalala sana kwa sababu tayari wamejijenga imara lakn mwanzo ukiwauliza watakwambia walikua hawalal sana, kiuhalisia uliza shule zinazofanya vzuri hapa tz e.g mzumbe, tabora boys, kibaha, watakwambia watu wanakesha sana wakisoma ila afta kufaul wapo vyuon wanakula bata eti kusoma kdgo tu pata na mda wa kupumzika, so UKIAMBIWA KITU CHANGANYA NA ZA KWAKO... Ifike wakati tutafute fursa na kuzitumia kulko kuhangaika kutafuta makala za eti 'vitu vya kufanya ili ufanikiwe' mana vinajirudia tu kila siku.... LET'S WORK! ASANTE
 
Back
Top Bottom