Tabia 20 za watu zinazowazuia katika mafanikio makubwa

willtarimo

Member
Mar 20, 2014
21
10
Usipite bila kusoma mahali hapa kama unahitaji Kubadilika na Kwenda hatua nyingine ya Kufikia katika Kilele chako cha Mafanikio makubwa; iwe Mafanikio ya Kiuchumi au kifedha, Kiafya, Kiakili na zaidi sana Kiroho pia.

Huu ni ujumbe unaoonyesha tabia ishirini zinazowazuia watu kufikia katika Mafanikio; ila pia ni ujumbe unaoonyesha sababu pekee za kwa nini watu wanashindwa Kufanikiwa.

Lengo la Ujumbe na Makala hii ni kukupa Msukumo utakaoleta Mabadiliko mapya ndani yako yatakayokupa nafasi ya kwenda kufikia katika Mafanikio Makubwa. Fahamu tabia hizi ili upate Kuziepuka na Kusonga Mbele zaidi baada ya Kubadilika.

Tabia hizo ni kama ifuatavyo:

1: Ni watendaji kabla ya Kufikiri.

2: Hawana au Hawajajiwekea Malengo.

3: Wanafikiri wanajua kila kitu.

4: Hawahitaji Kujifunza zaidi.

5: Ni waoga wakati wote.

6: Wanakata tamaa Kirahisi.

7: Ni watu wa Kupoteza Muda (waste their time)

8: Ni wapingaji wa Kila jambo zuri (Criticize).

9: Wanataka Kupitia Njia rahisi wakati wote katika Kufanikiwa.

10: Hawajui Kile wanachokitaka katika Maisha yao.

11: Siku zote ni wahitaji kwa Watu wengine.

12: Wanataka Umaarufu wa Jina kwa Haraka.

13: Kufikiri kwao na Kufanya ni Kwa Mtindo Hasi Muda wote.

14: Ni watu wanaojaribu Kuwashusha wengine chini Muda wote.

15: Ni wenye tabia za Kuwasema wengine Muda wote.

16: Wanaongea sana zaidi ya Kusikiliza na Kujifunza.

17: Hawahitaji Taarifa Mpya za Mabadiliko.

18: Kufeli kwao ni Majaribu, Hawataki Kufeli. Makosa ni Shule na huleta hatua mpya na mawazo mapya. Kubali Kujifunza kwa Makosa.

19: Wanahifadhi Moyoni Mambo ya Zamani waliofanyiwa na watu.

20: Ni watu wasiokuwa na Utayari wa Kujaribu Mambo mapya wakati wote.

Naamini umejifunza jambo jipya na nakutakia Mabadiliko mema. Amua leo kubadilika ili uwe Mana jangwani Mwa watu waliochoka. Mafanikio Makubwa uanza kwa Kubadili kwanza Tabia zinazozuia Mafanikio hayo.

[HASHTAG]#willtarimo2016[/HASHTAG] [HASHTAG]#AsMotivationalSpeaker[/HASHTAG]

Tembelea Mtandao wangu wa www.cicbat.com Kwa Kujifunza Zaidi.

www.facebook.com/WilfredTarimo
www.twitter.com/willtarimo
www.instagram.com/WilfredTarimo
 
Uko sahihi kabisa mkuu, wengi tunashindwa kuendelea kwa kuogopa kua risk takers, elimu na mfumo wa maisha vimetujengea hofu, woga na mashaka, mwisho wa siku tunaishia kujenga maghorofa midomoni na kwenye matumbo.
 
mafanikio hayamo kwenye kufikiri kwa namna hiyo zaidi ya juhudi na maarifa katika kufanya mambo bila kuataraji kufeli kufeli kuje wakati wewe ukifikiri hakuna kufeli mkuu
 
Back
Top Bottom