Tabaka kandamizi kwa namna yoyote ile haitafurahishwa na vitendo kama hivi vya Serikali ya awamu ya tano

Stroke

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
34,671
40,912
Kwa miaka mingi sasa, kuna tabaka flani ambalo limehodhi haki ya mambo flani katika jamii zetu.

Awamu hii pamoja na kujitahidi kuwaletea maendeleo wananchi wake, kwa upande mwingine linahakikisha usawa wa kufaidi matunda ya uhuru kwa wananchi wa kada zote unakuwepo.

Kishiria cha hayo ni pamoja na yaliyotokea jana huko Morogoro kwa huyu mama mfanya biashara ndogo ndogo.

Kwa namna yeyote ile, wanufaika wa mfumo huo kandamizi hawatafurahishwa na vitendo kama hivi vya Rais wetu. Hivyo vitendo vya kumpinga kwa nguvu zote vinaeleweka chanzo chake ni nini.

Tangu aingie madarakani Rais Magufuli amejitahidi na anaendelea kuonesha nia yake ya dhati ya kuleta usawa wa kada zote katika jamii katika kufaidi matunda ya Uhuru.

 
Back
Top Bottom