Taasisi zinazohamasisha ushoga kufutwa

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
3,162
2,000
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba ametaka apewe taarifa kuhusu taasisi na mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO) wanaohamasisha au kutangaza ndoa za jinsia moja nchini ili azifutie usajili mara moja.

Aidha ametaka kutajwa kwa watu wanaojihusisha na vitendo hivyo ili wachukuliwe hatua za kisheria kwa kujihusisha na vitendo hivyo ambavyo vinapigwa vita dunia nzima.

Nchemba aliyasema hayo jana mjini Kibaha alipokuwa akizungumza na taasisi za Kijeshi za mkoa huo zikiwemo Uhamiaji, Polisi, Magereza na Zimamoto juu ya kujua changamoto mbalimbali zinazowakabili.

Alisema kuwa taasisi hizo hazifai kwani zinafanya kazi ya laana ambayo ni kinyume cha maadili ya Kitanzania na hazistahili kuendelea kufanya kazi kwa upotoshaji huo.

“Leteni majina ya taasisi hizo ili tuzifute kwani hazistahili kuendelea kufanya jambo hilo ambalo ni laana na halipaswi kufumbiwa macho ndani ya jamii,” alisema Nchemba.

Kamanda wa polisi mkoani Pwani Bonaventura Mushongi alisema kuwa jeshi hilo linakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na upungufu wa vitendea kazi, ikiwa ni pamoja na magari.

Mushongi alisema kuwa licha ya kukabiliwa na changamoto hizo wamekuwa wakikabiliana na uhalifu kwenye mkoa huo ambao umekuwa kimbilio la wahalifu kutoka mikoa jirani ya Dar es Salaam.
 

saimon111

JF-Expert Member
Apr 5, 2012
1,726
2,000
Waanze na mawingu fm maana wanajitahidi sana kuhamasisha ushoga.....na baadhi ya wafanyakazi wake ni mashoga.
 

pye Chang shen

JF-Expert Member
Jul 11, 2016
5,514
2,000
Kuna wengine wanaoana na vyeti vya ndoa wanapewa mume kwa mume bonge la laana kazana baba na mungu atakusaidia utafanikiwa
 

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 31, 2016
7,703
2,000
Hivi hizi TAASISI au ngo's ni zipi hizo mbona naskia ZIPO Ila hazijulikani au .. Tuzitaje hapa hapa tumsaidie mheshimiwa waziri
 

ovi

JF-Expert Member
Aug 5, 2016
407
500
James delicious asisahaulike mana lile ni shoga kinyaa
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom