Taasisi za Twaweza na Uwezo Tanzania, yazindua ripoti ya 'Tathmini ya kiwango cha kujifunza nchini Tanzania 2019'

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,789
11,930
Taasisi ya Twaweza pamoja na Taasisi ya Uwezo Tanzania leo Desemba 11 zinazindua ripoti ya 'Tathmini ya Kiwango cha Kujifunza Nchini ya mwaka 2019'

Tathmini kubwa iliyofanywa na Taasisi ya Uwezo Tanzania kwa Wananchi tangu mwaka 2011 imetoa mchango madhubuti katika kuongeza uelewa wa hali ya kisomo nchini

1.jpg

Tathmini hizo zimesaidia kuboresha maarifa juu ya usawa ambao unaendelea katika upatikanaji wa elimu na upatikanaji wa ujuzi wa kusoma na kuhesabu

Ripoti hiyo inatarajiwa kuzinduliwa katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar kuanzia majira ya saa 3:30 asubuhi

Aidan Eyakuze - ED Twaweza

Utafiti huu uliwafikia watoto 65,000 na kaya 25,000, tumefikia wilaya 56 na tumetumia vijana 3,360 kupata matokeo haya.

Utafiti huu Haukinzani na tafiti nyingine ambazo pia zina uhalisia wake. Huu utafiti unajazia tafiti nyingine ambazo labda hazikumulika hapa.Huu mchango wetu, mchango wenu kama wadau na walaji wa hizi data.

Ripoti hii inawahamasisha wazazi kufuatilia mienendo ya watoto wao kwa ukaribu ikiwa ni pamoja na kuchukua mawasiliano ya walimu wanaowafundisha watoto.


Zaida Mgalla - Meneja wa Uwezo Tanzania

Tunaangalia mazingira ambayo yatapelekea mtoto kujifunza kama vyoo bora, chakula, maji

Tunaanga rasilimali kama je walimu wapo wa kutosha

Tunaangalia suala zima la elimu jumuishi- watoto wote wanaenda shule

Tunaangalia parental participation


Jitihada hii inapima uwezo wa wananchi ili kupima uwezo wa watoto kusoma na kuandika.Tunatengeneza majaribio yetu kwa kuzingatia mtaala wa Serikali kwa darasa la pili, Lengo ni kutoa tathmini ya uwezo wa watoto wetu ktk kujifunza

Ripoti hii ni takwimu ambazo tulizikusanya mwaka 2017. Tumefanya tathmini ya mwaka 2017 kukiwa na msisitizo mkubwa sana wa kufundisha KKK na Elimu bure kwa watoto wote.Takwimu zitatuonesha kama kweli watoto wote walikwenda shule

Uwezo ni jitihada iliyoanza 2009 katika nchi za Afrika Mashariki, Hufanyika nyumbani ili kupata watoto wote walio katika umri wa kwenda shule (miaka 6-16) ambao wako shule au la

Tunaangalia uwepo wa rasilimali watu katika shule. Je, kuna walimu wa kutosha shule. Pia tunaangalia suala la elimu jumuishi kama watoto wote wanakwenda shule hata wale wenye ulemavu pamoja na ushiriki wa wazazi katika masuala ya elimu

Kwanini #Uwezo ni muhimu? Taarifa tunazopata tunaleta mwanga mpya. Mfano katika suala la elimu jumuishi, upatikanaji wa mahitaji muhimu shuleni kama maji. Tunaamini matokeo yetu haya yanasaidia kuongeza ladha katika takwimu zinazotolewa na Serikali

Takwimu zinaonesha idadi ya kuandikisha watoto shule imeongezeka. Ktk upande wa jinsia hakukuwa na utofauti kwani watoto wote walikuwa wameandikishwa kwa uwiano ulio sawa. Kwa watoto wenye mahitaji maalumu, asilimia 28 hawakuwa wameandikishwa shule

Kwa darasa la 7 ufaulu umeshuka ila kwa darasa la 3 umefaulu umeongezeka kidogo kutoka 29% mwaka 2011 mpaka 62% mwaka 2017. Kinachochangia kwa darasa la 3 ni kutokana msisitizo wa kufundisha KKK tofauti na kwa madarasa ya juu kama darasa la 7

Bado kuna shida ya wanafunzi kusoma Kiingereza ambapo kwa takwimu takriban nusu ya darasa hawawezi kusoma Kiingereza. Hii italeta shida kubwa pale watakapokuwa wamefika madarasa la juu hasa Sekondari kwani masomo mengi yapo katika Kiingereza

Asilimia kubwa ya watoto kutoka maeneo ya mijini waliweza kujibu maswali ya jaribio la #Uwezo tofauti na wale wa vijijini,Pia watoto waliotoka familia zenye uwezo kiuchumi waliweza kujibu maswali kwa usahihi zaidi kuliko wale wa kaya masikini

23% ya shule zinatoa chakula kwa wanafunzi na kuna utofauti ktk Mikoa na Wilaya. Mfano karibu shule zote za Moshi na Ludewa wanatoa chakula kwa wanafunzi. Aidha 39% ya kaya ndizo zilibainika zinatoa chakula kwa watoto kabla ya kwenda shule asubuhi

Asilimia 50 ya wazazi waliohojiwa ndiyo walionekana kwamba wanatembelea Walimu mashulenu katika kufuatilia maendeleo ya mtoto. Asilimia 21 ya wazazi walionekana kuwa hukagua madaftari ya watoto wao watokapo shuleni

Tulichokiona ni kuwa Watoto wanaotoka kwenye kaya masikini na wale wa vijijini wana fursa ndogo sana ya kuweza kujifunza

Tunapendekeza kwamba hizi takwimu huria zipewe kipaumbele na pia ni muhimu kushughulikia suala la usawa kwa watoto kupata elimu.Tumekusanya data pia kwenye Governance and accountability

RIPOTI KWA UFUPI
 
Kwa kuwa halijagusa maslahi ya watawala i hope litapita salama
 
Tusubirie ripoti mkuu, nachojua elimu si mbaya sana kama tunavyodhani. Shule za umma ndo mbovu kulinganisha na shule binafsi.

Sasa ' Logically ' tu ukishakiri kama ulivyokiri hapa mwenyewe kuwa Elimu inayopatikana katika Shule za Umma ndiyo mbovu hiyo haiwezi kuwa ' justification ' kwamba Elimu ya Tanzania ni mbaya na iko ICU kama nilivyosema hapo awali? Hizo Shule Binafsi zinapokea Idadi kubwa ya Wanafunzi wa Kitanzania ambao 90% yao wanatoka katika mjumuisho wa Familia za Kawaida tu na Duni?

Siasa za Tanzania zimeharibu Sera nzima ya Elimu nchini Tanzania na hapa tusidanganyane au kupakana tu Mawese / Mafuta.
 
Sasa ' Logically ' tu ukishakiri kama ulivyokiri hapa mwenyewe kuwa Elimu inayopatikana katika Shule za Umma ndiyo mbovu hiyo haiwezi kuwa ' justification ' kwamba Elimu ya Tanzania ni mbaya na iko ICU kama nilivyosema hapo awali? Hizo Shule Binafsi zinapokea Idadi kubwa ya Wanafunzi wa Kitanzania ambao 90% yao wanatoka katika mjumuisho wa Familia za Kawaida tu na Duni?

Siasa za Tanzania zimeharibu Sera nzima ya Elimu nchini Tanzania na hapa tusidanganyane au kupakana tu Mawese / Mafuta.
Mkuu inaonesha una mawe ya kutosha sana, Karibu eneo la tukio maana kutakuwa na mjadala huru labda mabeberu yatasikia points zako mkuu.
 
Mkuu inaonesha una mawe ya kutosha sana, Karibu eneo la tukio maana kutakuwa na mjadala huru labda mabeberu yatasikia points zako mkuu.

" Purely Talented, Charismatic Fella, Game Changer and Entertainer " ataachaje kutokuwa na Mawe / Madini mengi Kichwani?
 
Wawe wamejiridhisha kuhusu vyeti vyao vya kuzaliwa na mambo kama uhujumu uchumi wasijejikuta wanafanya biznez na Dipipii
Hakika wewe ni great thinker.

Kama Mwele yumo humu ata ku-tag
 
Ngoja ripoti ije tusaidiane kuichambua tujue kama imaharibiwa na mabeberu au mtu kataka tu kujikomba kwa vichwa na mengine mengi..........
Ripoti tayari mkuu japo imewekwa yale machache ya muhimu sana jamii kuyajua, unaweza kujadili kuanzia hapo wakati ripoti kamili ikichakatwa na kupakiwa hapa
 
Back
Top Bottom