Taasisi za kifedha zaaswa kuwa makini ma mitandao ya uhalifu ya kimataifa

mkiluvya

JF-Expert Member
May 23, 2019
802
725
Waziri wa Fedha na Mipango Dokta Philip Mpango amezitaka taasisi za kifedha hapa nchini kuwa makini na mitandao ya uhalifu ya kimataifa.

Waziri Mpango amesema hayo leo Julai 8,2019 katika hafla fupi ya kupokea hundi ya gawio kwa serikali kutoka benki ya NMB ambapo jumla ya Tsh.Bilioni 10.48 zimetolewa na Benki hiyo kama gawio kwa serikali ambayo ni sehemu ya faida.

Waziri mpango amesema pamoja na mafanikio ya benki Ya huduma za kibenki hapa nchini lakini bado kuna changamoto za uhalifu wa kimtandao ambapo Wizara yake imepokea kesi na malalamiko mbalimbali yanayotokana na uhalifu wa mitandao.

Hivyo Dokta Mpango ametoa tahadhari kwa taasisi za kifedha nchini kuwa macho na wahalifu na watakatishaji wa fedha kupitia Mitandao ya kimataifa.

Mwenyekiti wa bodi ya Benki ya NMB Prof.Joseph Semboje amesema kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita Benki hiyo ilishalipa Tsh.Milioni 118 serikalini kama gawio.

Naye Afisa mkuu wa Fedha kutoka benki ya NMB Bi.Ruth Saikuna amesema benki hiyo ilitengeneza faida ya Tsh.Bilioni 142 kwa mwaka 2018 sawa na ongezeko la asilimia 3%.
 
Back
Top Bottom