Taasisi ya usalama wa taifa (TISS) ina bajeti?

Status
Not open for further replies.

Nyambala

JF-Expert Member
Oct 10, 2007
4,465
1,170
Wakuu nimejikuta nikijiuliza maswali kadha wa kadha kuhusiana na hiki chombo kinachoitwa usalama wa taifa.

1. Je chombo hiki kina bajeti?

2. Bajeti hiyo huwa inajadiliwa bungeni na kupitishwa kama zingine.

3. Katika bajeti hiyo kama ipo ni eneo lipi ambalo hutumia fedha nyingi?

4. Mwaka huu wa fedha imetengewa shilingi ngapi?

5. Je bajeti ya usalama wa taifa Tanzania ni siri na ni makosa kuihoji, kuiulizia, kuijadili?????

Haya yote yanakuja kufuatia hoja za wanasiasa mawaziri ndani ya serikali. Pinda na Masha zinazodhihirisha kwamba TISS hupata pesa kupitia kampuni zinazoanzishwa kwa muda maalumu na kwa majukumu flani muhimu ya kitaifa.

6. Je mwaka huu tuna kampuni ngapi zilizoanzishwa au zitakazoanzishwa on the same basis??

7. Ukaguzi wa matumizi ya TISS hufanywa na nani??????? au hairuhusiwi kukagua mahesabu yao?

Pls anayefahamu atufahamishe.
 
Aisee hawa huwa hawaulizwi wala kuhojiwa, wanadai kuwahoji hawa ni sawa na kuanika siri za serikali!! Bajeti yao nadhani iko Ofisi ya Rais Utawala Bora
 
Aisee hawa huwa hawaulizwi wala kuhojiwa, wanadai kuwahoji hawa ni sawa na kuanika siri za serikali!! Bajeti yao nadhani iko Ofisi ya Rais Utawala Bora

...usalama wa taifa AKA Meremeta....just Bullshit supreme!
 
kila Ofisi lazima iwe na Bajeti,Kwa hiyo Usalama wa Taifa wana bajeti yao....Ila waziri Mkuu si katukataza tuache kuzungumzia masuala yanayohusu Usalama
 
Bajeti yao iko ofisi ya rais utumishi, na mwaka huu wametengewa zaidi ya 130 bilioni.
kila mwka inapanda..ilikuwa 91bilioni ikaenda 111 bilioni. mwaka jana.ni hiii kwasababu ya Infalation?

imeongezwa na Bajeti nyingine ya kuwachunguza watu wa Jamii Forums,wameaanza kazi tayari..mie kidume yeyeyote atakenifuata tu,aombe wanifunge na nisirudi mtaani sababu nitamuongezea matiti ili aolewe...
 
Bajeti yao iko ofisi ya rais utumishi, na mwaka huu wametengewa zaidi ya 130 bilioni.

Sasa kama huwa wanatngewa bajeti ni wakati gani huwa wanatakiwa kupata pesa kwa njia ya kufungua makampuni ya ajabu ajabu??? I mean ikitokea nini hasa ndipo hata serikali huridhia kuruhusu kampuni hewa kufunguliwa, mapesa kuchotwa na kisha kuifunga hiyo kampuni.
 
imeongezwa na Bajeti nyingine ya kuwachunguza watu wa Jamii Forums,wameaanza kazi tayari..mie kidume yeyeyote atakenifuata tu,aombe wanifunge na nisirudi mtaani sababu nitamuongezea matiti ili aolewe...

Kuna fungu lao nadhani katika wizara ya ulinzi na jeshi la kujenga taifa , wizara ya mambo ya ndani pamoja na ile wizara ya ofisi ya rais nadhani wamo kwenye kapu moja na hao PCCB. TISS ni wide sana na hata consolidated fund nadhani wanakula hawa. JF itakuwepo na itaendelea kuwepo there are people withn the system who are fed up with these shameful acts by our political leaders they just fake it for them to get their daily bread thats all.
 
Haina bajeti katika siri-kali, huwa inapata pesa kutokana na miradi yao midogo-midogo kama meremeta na kagoda.....kwi..kwi..kwi
 
bajeti yake ni siri na haipaswi kutajwa hadharani kama bajeti za wizara, otherwise mwenye data na atupe.
 
nasubiri data za kua ni matumizi gani ya wanusaji hao ambayo yanawekwa hadharani manake me nijuavyo secret institutions zina principle ya secrecy at al times;sasa iweje matumizi yaanikwe????????? Tunaacha kujadili mambo muhimu ya kimaendeleo-tunaleta humu mambo ya bajet za taasisi nyeti.kuweka bajeti hadharani manake unaanika mapato na matumizi- sasa ukitaja matumizi c ndio utakua una reveal secret operations za watu hao muhimu kwa taifa? me nadhani mjadala wa bajet ya wanusaji wetu c muhimu kimaendeleo na kimaslahi ya taifa letu changa.
 
Last edited:
1. Je chombo hiki kina bajeti?

2. Bajeti hiyo huwa inajadiliwa bungeni na kupitishwa kama zingine.

5. Je bajeti ya usalama wa taifa Tanzania ni siri na ni makosa kuihoji, kuiulizia, kuijadili?????


7. Ukaguzi wa matumizi ya TISS hufanywa na nani??????? au hairuhusiwi kukagua mahesabu yao?

Kamati ya Kudumu ya Uinzi na Usalama ya Bunge.

THE STANDING ORDERS (2001 Edition) Sect. 98 (1)

Pursuant to Article 89(l) of the constitution

The Defence and Security Committee shall have not less than twelve and more than fifteen Members who shall be appointed by the Speaker, and its responsibilities shall be as follows:

(a) To consider and examine the Annual Estimates of Expenditure of National Defence and Security bodies

(b) To consider matters pertaining to defence and security of citizens and National Security.

(c) To consider any other matter which shall I be referred to it by the Speaker.


Iko chini ya Wilson Masilingi (CCM, Muleba Kusini). Anateuliwa na Spika.

Ni utaratibu ambao umekosolewa in some quarters kwa sababu Standing Orders ni taratibu za kuendesha Bunge lakini hazina uzito mahsusi kama Sheria, Acts. Hapa Masilingi ni kama bosi wa Rashid Othman, ana nguvu ya oversight juu ya Idara yake. Lakini cheo cha Othman ni cha Kisheria, cha kuteuliwa na Raisi, wakati cha Masilingi ni cha Standing Orders, cha discretion ya Sitta. Mteuliwa wa Raisi anakuwa chini ya Oversight ya Mteuliwa wa Spika!

Criticism nyingine, na labda ya muhimu zaidi, ni kwamba, kwa sababu ni Tume ya Bunge, basi inakuwa susceptible to partisan politicization. Kina Masilingi, ili kuilinda CCM, wanaweza wakatunza, au kutengeneza, siri za Kijeshi kuficha uovu. Siku Pinda alipowaambia kina Dr. Slaa (Mb.) kwamba Meremeta ni siri ya nchi, ilibidi Dr. Slaa aombe waende chemba akaonyeshwe nyaraka. Maana kuna Kanuni ngingine ya Standing Orders inasema Spika anaweza akaamuru vikao vya siri, closed sessions. Lakini Masilingi, Mkuu wa Tume ya Kudumu ya siri za nchi bungeni, anaweza asikubali kuona CCM na Pinda wao wanakuwa unraveled. Atategemewa akatae kumuonyesha Dr. Slaa (Mb.) vithibitisho vya uwepo au kutokuwepo kwa siri, na kama ni authentic na za maana. Sio kuficha siri hata za mshahara wa Raisi!

Ilibidi Usalama iwe under the oversight of a non-partisan ministerial organ.

(Integrity ya Wilson Masilingi kuongoza Tume ya Kikachero inaweza kuwa sio impeccable. Alikuwa na kashfa za ngono za wazi wazi akiwa kwenye cabinet ya Mzee wa ANBEN. Uaminifu au kutokuwa mwaminifu kwa mke wako kunaweza kutoa picha ya character yako inapokuja kwenye uaminifu au kutokuwa na uaminifu katika kutunza siri za nchi.)

Mmoja wa critics wa hii Tume anaiiongelea Bungeni hapa:

http://www.jambonetwork.com/jn/chacha-wangwe-great-stuff-bungeni-bot-schandal/
 
Wilson kama alivyo Dr. Kitine na Vicent Mrisho ni watu wenye ushawishi mkubwa TISS, lakini kwa wanaowajua vizuri ni watu wenye Tamaa za akina Mama na uroho wa pesa.Idara hii nyeti ina fungu kubwa na ipo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu - Utawala bora.

Si kweli kwamba Budget yake haijulikani, ukifuata utaratibu budget yake ipo wazi, lakini huwezi kufuatilia pesa zimetumika wapi, kwa sababu operation nyingi, pesa zake zinaangukia kwenye Matumizi ya Utawala.

Kuna Taarifa kuwa Budget ya Mwaka huu imekuwa kubwa karibu mara mbili ya Mwaka wa pesa uliopita..
 
Wakuu, sasa huwa inakuwaje biashara inafanyika kwa niaba ya TISS (Meremeta, Tangold, Kagoda etc) badala ya kutumia bajeti yao. Na in the last 3 yrs kulikuwa na threats gani kubwa zilizopelekea TISS kuburst bajeti yao na kutafuta fedha kwa njia ya kampuni fake??????
 
Wakuu, sasa huwa inakuwaje biashara inafanyika kwa niaba ya TISS (Meremeta, Tangold, Kagoda etc) badala ya kutumia bajeti yao. Na in the last 3 yrs kulikuwa na threats gani kubwa zilizopelekea TISS kuburst bajeti yao na kutafuta fedha kwa njia ya kampuni fake??????

Jamani, hao TISS wanasingiziwa tu kuhusu Kagoda and the like ili kuzima mjadala kwa kisingizio cha Usalama wa nchi. Hapo ni kwamba hao TISS usikute hawakuambulia hata shilingi moja kwenye hizo pesa, zimeliwa na wahindi wajanja kwa kushirikiana na viongozi wtu wetu mafisadi. Take my words!
 
Nimeomba kupata ufafanuzi katika hili kwani kuna taarifa zinatia shaka juu ya matumuzi ya taasisi hii ambazo zina onyesha matumizi yasiyo na tija kwa mfano zile pesa walizochukua pale CRDB na kumpatia Zitto zilikua na lengo gani na tija ipi kwa taifa then yawezekana vitabu vyao viliandikwa pesa yote milioni 450 na huku Zitto wamempa milioni 200

Nime yaandika haya kwa kuzingatia maslahi ya nchi na mapungufu makubwa ya idara hii kwani wameshindwa kusimama katika misingi ya kazi na kuwa wenye tamaa na pesa kuliko kuliko maana halisi ya kazi husika, naomba ufafanuzi katka hili na njia mbadala kama CAG aruhusiwi kukagua idara hii
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom