Taasisi Ya Urais Imepwaya mno Na Mfumo wa Kiserikali Ndiyo Mbovu Kabisa!!

TECH WIZ

JF-Expert Member
Jun 7, 2013
1,675
0
Limekuwa ni jambo la kawaida siku hizi kusikia Rais either amesitisha kazi za Waziri/Mawaziri kadhaa au amevunja baraza la Mawaziri kutokana na sababu kadha wa kadha.

Tatizo kubwa hapa ni jinsi hawa Mawaziri wanavyopatikana kwani wanateuliwa moja kwa moja na Rais bila ya kulishirikisha Bunge ndiyo sababu ya Rais kuishia kuzungukwa na Mawaziri mizigo (Washikaji).

Serikali kuhodhi sehemu kubwa ya madaraka na mamlaka ya ufanyaji maamuzi na utekelezaji mipango ya kimaendeleo imesababisha Wizara kuzidiwa na mizigo ya majukumu.Kwa kuelemewa huku na majukumu baadhi ya Mawaziri wasio na uwezo mzuri wa kiutawala wamejikuta wakilaumiwa na hata kuitwa mizigo na Wananchi waliochoshwa na uzembe wa Viongozi wetu.

Ili kuondokana na matatizo haya siku za usoni ni budi Katiba Mpya ijayo ikasimishe sehemu kubwa ya madaraka katika serikali za Mikoa ili kuipungizia lundo la majukumu serikali kuu na pia ili kupeleka maendeleo haraka Mikoani.

Pia Bunge letu lihusishwe kwa karibu katika kuwathibitisha Wateule mbalimbali wa Rais.
 
Dec 5, 2013
48
0
Ndugu, hata mawaziri wakipitishwa na Bunge, bado wabunge wengi ni CCM, usitegemee la maana hapo. Wameifikisha nchi yetu hapa, afu sasa wanapitia majukwaani wakitwambia nchi inahitaji maombi. Wengine wanadhubutu kutwambia tatizo letu hatuna harambee za kutosha hivyo tunahitaji harambee kubwa, yaani kila kijana awe na boda boda, basi. Ndo walipotufikisha hapa.

CCM hawawezi kukupa katiba ya haki kwa sababu chama chake si cha haki. Kinafaidika na hiyo misingi mibovu. Hii misingi mibovu unayoona ndo neema ya CCM. Wameoza kuanzia kwa Rais mpaka chini. Rais ndo chanza cha yote haya. Hayupo serious na lolote, itakuwaje watendaji kazi wake?

Yeye anajua kupiga picha tu. Juzi alikuwa New York, watanzania wakadanganywa kuwa alikuwa kwenye matibabu, muulize Miraji wa huko US. Yeye ndo anajua anafanyaga nini na JK wakiwa huko.

Kwa sababu tumechoka na ujinga huu, ntaweka picha ambazo alipigwa bila kujua na huu inawezekana ndo mwisho wake...nazifatilia.
 

mavumbi

JF-Expert Member
Feb 8, 2013
457
250
budi Katiba Mpya ijayo ikasimishe sehemu kubwa ya madaraka katika serikali za Mikoa ili kuipungizia lundo la majukumu serikali kuu na pia ili kupeleka maendeleo haraka Mikoani.QUOTE]

1. Kulundika majukumu makao makuu ya wizara
2. Kutotoa fursa ya kutosha kwa kuziwezesha serikali za mitaa kutekeleza majukumu kwenye ngazi za msingi

Haya pia yanachangia sana kushindwa kwa serikali kutekeleza majukumu yake. Lakini ukweli ni mfumo kiritimba ulioasisiwa na mfumo wa kisisasa na kuambukiza hadi serikalini. Utawala wa kisiasa ukiwa na hali mgando kama iliyopo hivi leo, watendaji nao hufanya kazi ki mgando mgando.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom