Taasisi ya Urais chini ya Amiri Jeshi Mkuu siyo sehemu ya vichekesho

Oct 7, 2019
51
156
Tukirejea ktk kumbukumbu ya tarehe 14 November 2019, Siku ya Alhamisi, Idriss Sultan akiwa mbele ya Waandishi wa Habari alimuomba Msamaha Rais

Magufuli kwa kuweka picha mbili tofauti zilizoleta taswira mbaya kwa Taasisi ya Urais wa Tanzania (JMT Presidency) na Rais Mwenyewe Binafsi. Idris alilazimika kuomba Msamaha huo baada ya kuangukia Mikononi Mwa Sheria.

Ktk Picha zile, Picha ya kwanza katika editing Idris aliondoa kichwa cha Rais akaweka kichwa chake yeye Mwenyewe na picha ikawa ina mwonekano Mpya Wa sura na kichwa cha Idris akiwa ameketi katika kiti chenye nembo ya Taifa lakini mwili uliovaa suti na kuketi ktk kiti hicho ni wa Rais Magufuli. (Mkuu wa Nchi na Amiri jeshi Mkuu).

Picha ya pili Idris aliweka kichwa Cha Rais ktk Mwili wa Mtu Mwingine aliyevaa shati jeupe na suruali yenye mikanda inayoshikizwa Mabegani (Suspenda)

Sasa katika hili jipya ni vema Tuendelee kufahamu kuwa "Kucheka picha yoyote hata ya Mama yako Mzazi au Baba yako Mzazi iwe picha ya Zamani au ya sasa sio kosa kabisa Kisheria" ila kuichukua picha hiyo hiyo au ya mtu mwingine, kuitengenezea video na kuhamishia kicheko hicho ktk social Media kwa kushirikisha kicheko chako na jamii nyingine unakuwa umeingia katika hatua nyingine pia.

Hapa inaweza kuwa tu sio tu kumkosea heshima Mwenye picha bali inaweza kuwa kinyume cha Sheria ya kimtandao, hapo hakuna Excuse, Uhuru wa Habari wala Uhuru wa Manyani. Picha halisi ya Kiongozi Mkuu wa Nchi ni tofauti na Michoro ya Viongozi wakiwa na Vichwa vikubwa, ipo tofauti kubwa kati ya"Kuhabarisha, kuchekesha na kudhalilisha". Ni Taasisi ya Urais iheshimiwe!

Rais aheshimiwe kama Mkuu wa Taifa, kama Baba wa Familia. Rais wa Jamuhuri hii ya Muungano wa Tanzania ni kiongozi na Mkuu wa Nchi ambaye anasimama Mstari wa Mbele kabisa katika Taifa hili kama Raia nambari Moja, Watanzania wengine wote Nyuma yake.

Rais ni Kiongozi wa Taasisi ya Urais ambayo pamoja na kuwa kiongozi wake bado taasisi hiyo ina jukumu la kumlinda yeye binafsi, kulinda Reputation yake na hata kutekeleza Majukumu mbalimbali kwa miongozo yake...Taasisi ya Urais pia ina wajibu wake wa kikatiba wa kulinda na kutetea Heshima ya Taasisi hiyo kwa mujibu wa sheria na kuchukua hatua pale inapovunjwa, kudhihakiwa ama kuchezewa na Mtu yeyote.

Nikumbushe tu kwamba Dunia imewahi kuwa na All timers ktk tasnia ya Comedy, Magwiji kama Bill Cosby, Charlie Chaplin, Eddie Murphy, Rowan Atiknson, Jim Carey na wengine wengi lakini hawa wote wanatoka ktk Mataifa ambayo yanajiongoza kwa mujibu wa Sheria zake.

Sheria za Marekani anapotoka Eddie Murphy inaweza kuwa sawa au si sawa na Uingereza anapotoka Rowan Atiknson (Mr Bean), lakini hawa wote wanaheshimu Mamlaka za Mataifa yao..Wanajua Mipaka yao ktk kuutafuta Ugali wao, Huwezi kukuta Kichwa cha Mr Bean kwenye Mwili wa Malkia Elizabeth kwa kisingizio cha Comedy. Never!
.
 
Mnaendelea kupaka paka rangi bado? Watanzania wanajua kuliko mnakotaka kuwaelekeza.
 
Idris anashtakiwa kwa kosa la kutumia laini ya simu isiyokua yake.Kosa la kucheka picha ya rais ilikua ni kitega uchumi tu.
Hebu waulize hao waliomsweka ndani, ni kwanini wamebadilisha mashitaka na kumshitaki Idris Sultan kwa kosa la kutumia line ya simu ya mtu mwingine na sivyo anavyosema yeye kuwa huyo Idris ameidhalilisha taasisi ya Urais?
 
Naona leo moja ya watumishi wa ikulu kaja hapa kutolea maelezo swala hili.Mkuu naomba ajira hapo bhana mm ni kijana mzalendo wa taifa hili.
 
Hebu waulize hao waliomsweka ndani, ni kwanini wamebadilisha mashitaka na kumshitaki Idris Sultan kwa kosa la kutumia line ya simu ya mtu mwingine na sivyo anavyosema yeye kuwa huyo Idris ameidhalilisha taasisi ya Urais?
[/
Hebu waulize hao waliomsweka ndani, ni kwanini wamebadilisha mashitaka na kumshitaki Idris Sultan kwa kosa la kutumia line ya simu ya mtu mwingine na sivyo anavyosema yeye kuwa huyo Idris ameidhalilisha taasisi ya Urais?
😅😅😅
Zaidi nawashangaa ambao bado wanang'ang'ania kuwa jamaa alifanya kosa kisheria kumcheka rais na ni haki kushtakiwa wakati waliomkamata walisha change gear angani kitambo!
 
Kwani jamaa ameshtakiwa kwa kosa gani?
Si ameshtakiwa kwa kutumia line ambayo sio yake.Sasa kama ilo wewe unalosema ndio kosa y mashtaka hayasemi hivyo.
 
Huu ni mmomonyoko wa maadili, adhabu ya Idris inatakiwa kuwa mfano kwa watu wengine wenye tabia kama yake!

Nakumbuka miaka ya 2006 hivi, kuna mtu alitengeneza picha ya kumdhalilisha Rais Kikwete kupitia mtandao wa 'Ze Utamu' alitafutwa kwa hudi na uvumba hadi nje ya nchi na mtandao huo ulifungwa!
 
Unafuatilia kweli comedy? Maana Kama unafuatilia na unapenda comedy Basi utakuwa unajua jinsi huku unakokutaja hao macomedian wanavyoongoza kuwatania Tena utani wa matusi viongozi wao..
 
Huu ni mmomonyoko wa maadili, adhabu ya Idris inatakiwa kuwa mfano kwa watu wengine wenye tabia kama yake!

Nakumbuka miaka ya 2006 hiv, kuna mtu alitengeneza picha ya kumdhalilisha Rais Kikwete kupitia mtandao wa 'Ze Utamu' alitafutwa kwa hudi na uvumba hadi nje ya nchi na mtandao huo ulifungwa!
Mkuu,kutumia line ya simu ya mtu mwingine na mmomonyoko wa maadiri vinahusianaje hapo?
Idris anaadhibiwa kwa kosa gani?
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom