Taasisi ya Uislam Dar walaani Uamsho wa Zanzibar

mshikachuma

JF-Expert Member
Dec 2, 2010
2,853
626
Mwenyekiti wa taasisi ya kiislam Dar bwana Sadiki Kotikoti na wajumbe wenzake wamelaani vitendo vya wanauamsho wa Zanzibar na wamesema UAMSHO hawana tofauti na Alshabaab au al-qaeda.

Pia ameiomba serikali iwachukulie hatua kali sana za kinidhamu.

Source: ITV Habari saa mbili usiku leo
 
Pia aliendelea kwa kusema hata makundi ya kigaidi ya Al-qaeda,Boko haramu na Alshaabab walianza
hivihivi kama hawa Uamusho wa Zanzibar
 
Mnajikosha eeh....hata shain nae mmemlazimisha kutoa tamko...ukimuangalia usoni hakuendani na anachokisema...
 
Hawa jamaa lao moja; tatizo wamepandiza chuki kwa waumini wao kwa muda mrefu bila kufahamu madhara yake yatakuwa nini?.

Viongozi wengi wa kiislamu wamekuwa wakifundisha waumini wao kwamba; matatizo na shida walizonazo (kutokupata elimu, ajira n.k) yanatokana na mfumo UKRISTO unaotumika katika serikali ya nchi hii.

Kwa miaka mingi waliacha kusisitiza waumini wao kujikomboa kwa kusoma na mambo mengine ya msingi ambayo yangeweza kuwaletea maendeleo, badala yake waliendelea kuhubiri chuki. Movement nyingi huanzia msikitini, kuna nini...?
 
Kaongea maneno yenye ujumbe mzito sana. Kwamba kwanini makanisa yachomwe ilhali si taasisi za kiserikali ama kisiasa? Pia akaongeza kanisa visiwani lipo siku nyingi tu kabla ya muungano toka miaka ya 1870 hivi.

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Mnajikosha eeh....hata shain nae mmemlazimisha kutoa tamko...ukimuangalia usoni hakuendani na anachokisema...
lao moja makanisa yamechomwa 23 hakuna mtu alieye kamatwa nikisema kuna mkono wa serekali nimekosea.
 
Hii ndiyo kazi ya ZOKA – yule shushu wa Usalama wa taifa na wenzake, kununua wanaojiita masheikh na kubweka kwa maslahi yao binafsi.

Bahati mbaya sana ni kuwa hawa wanaotumwa; na Zoka anayetuma, hawajipi hata muda kidogo wa kufikiri faida na athari ya hicho wanachotaka kukifanya. Ndiyo maana, yule Dk. Slaa (dk wa ukweli) alisema zamani, "Usalama wa taifa umelishabinafisishwa kwa mafisadi kitambo kirefu."

Hivi kauli ya mashekh hao itasaidia nini kurudisha nyuma harakati za UAMSHO unaoungwa mkono na jamii kubwa ya raia wa Zanzibar? Mimi naona kauli hiyo, inazidi kuingiza nchi kwenye chuki kati ya Bara na Zanzibar.

Madai ya Wazanzibari ni kwamba nchi yao inanyonywa na Bara na inaendeshwa kutoka Bara. Sasa kauli ya bara kutaka serikali idhibiti kundi hili ikitekelezwa, itakuwa inathibitisha madai yao hayo.

Kama usalama wa taifa ungekuwa upo imara kama zamani, wangewatafuta masheikh kutoka Zanzibar, tena wanaoheshima kukemea UAMSHO. Kutumia masheikh wa Bara ni sawa na kutaka kuikemea Iran, wakati wewe ni Mmarekeani. Hakuna atakayekusikiliza.

Mimi naamini masheikh wa bara wamepotoka na muda si mrefu hili litajibiwa kwa nguvu na uamsho. Tusubiri.

 
sasa ZOKA anahusika vipi na haya jamani?

sidhani kama ana muda wa kujihusisha na haya mambo ya maji machafu

Hapa kuna kila mkono wa CCM na NAPE
 
Pia aliendelea kwa kusema hata makundi ya kigaidi ya Al-qaeda,Boko haramu na Alshaabab walianza
hivihivi kama hawa Uamusho wa Zanzibar

Alqaeda na Alshaabab ni makundi matakatifu yanayopambana dhidi ya mfumo kristo duniani na wanapata thwawabu kwa kutekeleza kazi ya allah
 
Watanzania jifunzeni kutobebwa na Propaganda nyepesi, Mmesahau mlivyoletewa Babu wa Loliondo mkasahau kujadili uhalali wa matokeo ya 2010!

Hoja ilikuwa kupinga Muungano tena hawa jamaa wanahoja nzito kwanini hawaruhusiwi kujadili mfumo wa muungano?

Kwa kuwa serikali haina majibu imetumia vijana kuchoma Makanisa ili ipate sababu ya kuifungia jumuia hii iliyoanza kushika nafasi ya CUF visiwan!

Hii serikali ilipofika ipo tayari iwapiganishe ili mradi isalie madarakani, Uamsho wamekanusha na wanajua hata kama Znz ingekuwa ni Dola ya Kiislam hakuna Ruksa ya kuchoma Kanisa, Sinagogi wala pango la Ibada sasa iweje wafanye move hiyo ambayo ingeua ajenda yao kuu ya kuukata Muungano???
 
Watanzania jifunzeni kutobebwa na Propaganda nyepesi, Mmesahau mlivyoletewa Babu wa Loliondo mkasahau kujadili uhalali wa matokeo ya 2010!
Mkuu,

Utaongea mambo mengi sana....lakini habari ndiyo hiyo waislaam wa Bara wamepinga hiyo kitu yenu kwa tamko zito sana
 
Alqaeda na Alshaabab ni makundi matakatifu yanayopambana dhidi ya mfumo kristo duniani na wanapata thwawabu kwa kutekeleza kazi ya allah

Huyo allah anafanyiwa kazi kwa mikono ya binadamu siku hizi? ile kunfa yakun ime ekpaya! acheni hizo, msimfanye allah kuwa duni kwa matakwa yenu duniani.
 
Back
Top Bottom