Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
Taasisi ya TPRI imefunga zaidi ya maduka ishirini ya dawa za mimea na mifugo kwenye miji ya Nyasa Mbamba Bay na Mbinga na kukamata idadi kubwa ya dawa bandia za kuhifadhi nafaka ania ya Supre Actellic 500e pamoja na karate zenye viambata vya sumu zinazo tajwa kuingizwa kinyemera kupitia mpaka ya nchi jirani za Malawi na Msumbiji huku baadhi ya wauzaji wa maduka wakifunga maduka na kukimbia wakaguzi.
Katika ukaguzi huo wakaguzi walipata wakati mgumu baada ya kuona maduka mengi yakiwa yamefungwa katika kipindi kisicho zidi dakika ishirini baada ya wakaguzi kuwasiri lakini operesheni iliendelea na kukamata dawa hizo ambazo msambazaji wake kampuni ya Syngenta ya jijini Dar-es-Salaam amethibisha kuwa dawa hizo ni feki kwakuwa zimetumia jina lake lakini hawazitambui na zimekuwa zikilalamikiwa na watu wengi.
Kwa upande wao baadhi ya wauzaji wa viutalifu wamesema watu kufanya biashara bila vibali na kuuza dawa feki inatokanana wakaguzi kutotembelea maeneo ya pembezoni kwa muda mrefu hali inayo athiri malashi ya wakulima na uhai wa watu wanaotumia mazao yanayo hifadhiwa na kutibiwa na dawa dandia.
Chanzo: ITV