Taasisi ya Nyerere, kiko wapi kitabu alichokitoa Baba wa Taifa kiitwacho "HATIMA YA TANZANIA"?

Ishaka

Member
Nov 1, 2011
74
12
Yanayoendelea sasa katika nchi yetu, mwasisi wa Taifa hili alishayaona na ili kunusuru nchi pamoja na kizazi hiki alichukua hatua ya kutoa WOSIA kwa watanzania katika kitabu chake cha Hatima ya Tanzania karibia ukingoni mwa serikali ya awamu ya pili ya Mzee A.H. Mwinyi. Mtakumbuka kwamba katika kitabu kile kwa waliopata bahati ya kukisoma, kuna viongozi aliwataja hadharani kwamba hawafai kabisa kuongoza nchi yetu. Kitabu hiki Baba wa Taifa Mwl J.K. Nyerere aliingia garama ya pesa yake ya mfukoni kwenda nje ya nchi kuchapisha kitabu hiki ili kutuelimisha na kutufumbua macho watanzania, lakini ajabu ni kwamba katika hali isiyokuwa ya kawaida maelfu ya nakala zilizoingizwa nchini zilifyonzwa gafla hapahapa Dar es salaam kikatoweka katika mazingira ya kutatanisha! Watanzania wengi waliolengwa tulikikosa hatujakisoma. Mimi nafikiri katika kumuenzi Baba wa Taifa ni pamoja na kufanyia kazi yale aliyokuwa akiyakemea waziwazi na kuyafanyia kazi vinginevyo ni unafiki tu wa kutumia jina lake kwa manufaa binafsi. Hivyo naiomba Taasisi ya Mwl Nyerere ifanye kazi hiyo, siamini kwamba hawana nakala ya kitabu hicho. Toeni nakala nyingi kadiri inavyowezekana maana tunaamini kuna mambo mengi juu ya msitakabari wa nchi yetu aliyaandika.
 
Back
Top Bottom