Taasisi ya Mwl Nyerere ..inamdahalilisha Mwl Nyerere

Mwangaza

Senior Member
Feb 26, 2008
198
64
Wanabodi,


Leo tumeshudia taasisi ya Mwl Nyerere ikitumika kisiasa kufanya kampeni za waziwazi kwa mgongo wa mdahalo wa Amani.

Hakuna duniani mdahalo wasemaji wakuu wakawa wa itikadi moja tu??..hii ajabu imetokea leo kwenye hii taasisi nia aibu kubwa kwa heshima ya Mwl.

Tumeona wasemaji wakuu Polepole, Butiku na Mama Mongela wote wakivika UNAFIKI na wakitoka nje ya mada kuu kabisa na kuanza kufanya kampeni za wazi wazi huku wakimshambulia directly na inderectly Mh Lowassa tu.

Mfano Polepole huyu huyu aliyekuwa anasimamia katiba ya wananchi .leo anaungana na waliopola mdaraka ya wananch kwenye rasimu katiba na kutengeneza katiba yao...akifanya unafiki wa ajenda ya UADILIFU. Ni uadilifu gani tunaotaka zaid ya mtu anayehishu katiba/maoni ya wananchi? Ni uadilifu gani tutauona kwa mtu aliyegawa nyumba za serikali kwa hawala? Ni UADILIFU gani anaongelea huyu aliyedhalau amri ya mahakama ya Tabor, huyu anayeendelea kudhalau amri ya taasisi za kiserikali kama BASATA kumfungia Shilole yeye anazunguka naye. HAKUNA UADILIFU MKUBWA KAMA KUHESHIMU MAMLAKA NA KATIBA,


Polepole anajisifia kutoa msaada wa mawazo kuhusu rasimu kwa UKAWA,anasahau alilipwa kwa kodi zetu Tsh 500,000/- kila siku kuandaa rasimu hiyo. sasa alitaka UKAWA wakacchukue maoni wapi kama sio kwao hao tuliowalipa kodi zetu??

Maana ya AMANI NI UWEPO WA HAKI NA USAWA. Hawa WANAFIKI hawajongelewa uwepo wa HAKI na USAWA..Wakati Mgombea Mmoja anazuiliwa kutumia uwanja wa Taifa, mwingine anaruhusiwa kutumia viwanja hvyo, anatumia mpaka ndege ya serikali na magari..HAKI IPO WAPI? Wakati


Hayati Mwl Nyerere alipata kusema "ccm sio mama yangu". Tunaamini angekuwepo leo asingweza kuendelea kuwa ndani ya ccm hii inayonuka ESCROW,EPA,KAGODA,KIWIRA,DOWANS,..ccm hii inayoua na kutesa watu kama Mwangosi, ulimboka! ccm hii inayopandisha Twiga ndege,inayomaliza Tembo..ccm hii inayo ingia mikataba kuuza rasilimali zetu kila siku.nk...Mwalimu Nyerere ASINGEKUWEPO HUKO, sio UNAFIKI UNAOFANYWA NA TAASISI YAKE KUYAFUMBIA MACHO HAYA...watz tunayaona na tunataka MABADILIKO YA MFUMO MZIMA.
 
Back
Top Bottom