Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) imekuwa kero kwa foleni yake, mamlaka ishughulikie

Mjenda Chilo

JF-Expert Member
Jul 20, 2011
1,467
513
Kwanza nianze kwa kuipongeza Serikali kwa kuanzisha kituo hiki ambacho kinasaidia maelfu ya wananchi hasa wale walioshindwa kumudu gharama kubwa za matibabu ya moyo huko ng'ambo.

Ninafahamu mna madaktari wazalendo na wabobezi hasa katika fani hii Tena wengi wao wakiwa bado vijana.

Tatizo kubwa ambalo limekuwa Kero kubwa Sana Sana Ni suala la utoaji huduma ambalo halizingatii Wala kujali muda. Mtu anafikaje alfajiri anakuwa wa kumi na au ishirini mpaka jioni hajamuona Daktari? Sio siku moja Ila Mara kadhaa Jambo hili limekuwa linajirudia.

Hamna utaratibu wa kuwaona hao mnaowaita VIP (mnaowafahamu ninyi) kiasi kwamba mnaacha wazee wanateseka kwenye mabenchi siku nzima? Inakera Sana Sana.

Niwaombe mtafute mtaalam wa foleni Kama hamna ili awashauri njia Bora ya kushughulikia wateja wenu kwa wakati, vinginevyo mnaharibu kazi nzuri mnayofanya kwa kuwaachia wasaidizi wenu kufanya watakavyo kwenye taratibu za kuona wagonjwa. Over.
 
Back
Top Bottom