Taasisi ya Kiswahili neno "Kiate" kwa nini halisikiki sana?

FINDTRUEFAITH

Member
Mar 24, 2011
83
86
Nimekuwa mfuatiliaji sana wa lugha yetu adhimu ya Kiswahili kupitia vyanzo mbali mbali.

Moja ya neno lisilopewa kipaumbele kwa kutamkwa mara kwa mara ingawa ni la muhimu ni neno "kiate."

Neno hili kwa mujibu wa wataalamu wa lugha ya Kiswahili ni; mtoto aliyefiwa na wazazi wote wawili, kwa maana ya baba na mama.

Wengi wamezoea kumuita mtoto alyefiwa na wazazi wote wawili kwamba ni yatima, jambo ambalo si kweli.

YATIMA: ni mtoto aliyefiwa na baba ila mama yake yuko hai. Kwa maana ya yule anayemtimizia mahitaji yake (a bread winner )

MKIWA: ni mtoto aliyefiwa na mama ila baba yake yu hai. Kwa maana ya yule aliyekaribu na mtoto na kumfariji kila wakati (a comforter)

Ndipo anakuja KIATE: aliyefiwa na wazazi wote wawili.

Tuna vituo vingi vya watoto yatima. Tukitumia neno hili moja tu la Yatima kuwatambulisha watoto hao, tuna maana watoto hao wamepoteza mzazi mmoja ambaye ni baba, lakini wanao mama zao, hata kama ukweli ni kwamba wamepoteza wazazi wote wawili kwa maana ya mtoa mahitaji na mfariji, ambayo hiyo ndiyo sababu ya kutafutiwa mtoa mahitaji na mfariji mwingine (social workers).

Vitabu vya dini vimetusaidia kuliongelea hili vizuri kuhusu yatima ni nani; na mkiwa ni nani.

Ndani ya Biblia katika kitabu cha Maombolezo 5:3 imeandikwa, " Tumekuwa yatima waliofiwa na baba; Mama zetu wamekuwa kama wajane."

Katika aya hii imeoneshwa kwamba yatima ni mtoto aliyefiwa na baba.

Kuhusu mkiwa, katika kitabu cha Injili ya Yesu kama Ilivyoandikwa na Mathayo, Sura ya 23: 37-38 amenukuliwa Yesu akiuelezea mji wa Yerusalemu kuachwa ukiwa, kwa sababu haukutaka kukusanywa kama vile kuku (tetea-kuku jike) anavyowakusanya vifaranga wake. Imeandikwa,

37 Ee Yerusalemu, Yerusalemu, uwauaye manabii, na kuwapiga kwa mawe wale waliotumwa kwako! Ni mara ngapi nimetaka kuwakusanya pamoja watoto wako, kama vile kuku avikusanyavyo pamoja vifaranga vyake chini ya mabawa yake, lakini hamkutaka!
38 Angalieni, nyumba yenu mmeachiwa hali ya ukiwa."

Ni kawaida nchi yoyote kuchukia sifa ya kike (she). Hapa kwa sababu Yesu alitakiwa apokelewe Yerusalemu kama mfalme wao walimkataa. Kila mfalme ana mji wake anaoutawala. Hapa anaelezea nyumba yao kuwa ukiwa yaani bila mfalme.

Maneno mawili haya; yatima na mkiwa yanafahamika sana, lakini hili la kiate halifahamiki sana, ingawa ni neno lililojitokeza kutokana na maendeleo ya kukua kwa Kiswahili. Profesa Abdallah Safari analijua vizuri neno hili.

Ninawaomba wahusika na wadau kulitangaza zaidi neno hili ili lijualikane vyema kwa watumiaji wa lugha yetu adhimu ya Kiswahili.

Jioni njema!
 
kwa mimi binafsi hapo ndipo ninapokerwa na kiswahili, kwanini mlazimishe misamiati isiyotumiwa na wengi ndio iwe "rasmi"? kwa mfano ni nani leo hii anaenda dukani anasema "nataka gurudumu"? au "nataka jokofu"? kwanini tusiyakubali maneno yanayotumiwa na wengi kama vile tairi, friji, kumpyuta, kamera n.k iwe misamiati rasmi. kuazima misamiati kutoka lugha nyingine sio dhambi hata kiingereza kimejaa misamiati ya kuazima toka lugha kama kifaransa na kilatini. Tuachane ni misamiati ya ajabuajabu ya kubuni inaifanya lugha rahisi kuwa ngumu.
kuna siku nilozima TV baada ya kuona natizama taarifa ya habari ya kiswahili alafu sielewi mtangazaji anaongea nini, mara aseme "viwatilifu" mara " mpakato" na upuuzi mwingine
 
Uko sahihi. Kama hii mada anayozungumzia mwanzisha thread mimi naona ni kupoteza muda na kuturudisha nyuma. Yatima limeshazoeleka na kukubalika kiasi ambacho ni vigumu kuchomeka tena maneno mengine. Tulikubali na tusonge nalo mbele. Pia maoni yako yana mantiki, tusilazimishe. Halafu kwa upande wangu hakuna kitu kinachonikera kama kuita hizi ''mobile phones'' eti ''simu ya kiganjani''. Huyu aliyechomeka hili neno alilazimisha ni bora tutumie ''simu ya mkononi''. Kwani kiganja si ni sehemu ya mkono? Mbona tuna maneno kama mpira wa miguu na siyo mpira wa kwato or whatever?
 
Kwa jinsi ile lugha za makabila zilivyo kufa, ndivyo pia kiswahili asilia kitakavyopotea kabisa kwa kumezwa na uzungu.
 
Uko sahihi. Kama hii mada anayozungumzia mwanzisha thread mimi naona ni kupoteza muda na kuturudisha nyuma. Yatima limeshazoeleka na kukubalika kiasi ambacho ni vigumu kuchomeka tena maneno mengine. Tulikubali na tusonge nalo mbele. Pia maoni yako yana mantiki, tusilazimishe. Halafu kwa upande wangu hakuna kitu kinachonikera kama kuita hizi ''mobile phones'' eti ''simu ya kiganjani''. Huyu aliyechomeka hili neno alilazimisha ni bora tutumie ''simu ya mkononi''. Kwani kiganja si ni sehemu ya mkono? Mbona tuna maneno kama mpira wa miguu na siyo mpira wa kwato or whatever?
Mpira wa miguu sio sahihi ,mpira wa kwato sio sahihi pia kwasababu binadamu hana kwako,tutumie mpira wa nyayo basi
 
Sentensi: Mhamasishaji aliihamasisha jamii kujitolea kuwalea kiate, wakijua kwamba watoto ni watoto waliopoteza wazazi wote
Mkuu kumbe hilo neno kiate halina wingi. Mimi nilidhani wakiwa wengi ni '' Viate''.
Naomba Muongozo, maana hili neno nimelipenda mkuu.
 
Asante kwa kutukumbusha kuhusu kiate, neno lenye asili katika Kiamu (Kiswahili lahaja ya Lamu). Ila tu sioni ya kwamba unaitumia sawa. Ushahidi wa zamani inaonyesha: ilimaanisha yatima asiye tena na mama.
Sacleux alishika neno hivi: kiAte (Am.). Orphelin (de mère seulement) (alikusanya msamiati katika miaka ya 1900-1930)
Asili ni Kiamu "ku-ata" ambayo ni matamshi yao ya "ku-acha". Kiate= aliyeachwa, aliyebaki

Yatima ni pana zaidi. Ni neno lililopokelewa kutoka Kiarabu (kama asilimia 30-40 ya msamiati wa Ksiwahili kwa jumla). Yatima inammaanisha asiye na wazazi tena. Mfano wa Biblia haisaidii. Maana kwa Kiebrania neno ni יָתוֹם yatom (sawa na Kiarabu yatim, maana ni lugha ndugu) ni ama mtoto bila baba au mtoto bila wazazi kabisa.
 
Nywila, ukarabati na ukarafati 🙉🙉🙉

kwa mimi binafsi hapo ndipo ninapokerwa na kiswahili, kwanini mlazimishe misamiati isiyotumiwa na wengi ndio iwe "rasmi"? kwa mfano ni nani leo hii anaenda dukani anasema "nataka gurudumu"? au "nataka jokofu"? kwanini tusiyakubali maneno yanayotumiwa na wengi kama vile tairi, friji, kumpyuta, kamera n.k iwe misamiati rasmi. kuazima misamiati kutoka lugha nyingine sio dhambi hata kiingereza kimejaa misamiati ya kuazima toka lugha kama kifaransa na kilatini. Tuachane ni misamiati ya ajabuajabu ya kubuni inaifanya lugha rahisi kuwa ngumu.
kuna siku nilozima TV baada ya kuona natizama taarifa ya habari ya kiswahili alafu sielewi mtangazaji anaongea nini, mara aseme "viwatilifu" mara " mpakato" na upuuzi mwingine
 
Uko sahihi. Kama hii mada anayozungumzia mwanzisha thread mimi naona ni kupoteza muda na kuturudisha nyuma. Yatima limeshazoeleka na kukubalika kiasi ambacho ni vigumu kuchomeka tena maneno mengine. Tulikubali na tusonge nalo mbele. Pia maoni yako yana mantiki, tusilazimishe. Halafu kwa upande wangu hakuna kitu kinachonikera kama kuita hizi ''mobile phones'' eti ''simu ya kiganjani''. Huyu aliyechomeka hili neno alilazimisha ni bora tutumie ''simu ya mkononi''. Kwani kiganja si ni sehemu ya mkono? Mbona tuna maneno kama mpira wa miguu na siyo mpira wa kwato or whatever?
Aliyeweka hilo neno wala hakulazimisha yupo sahihi lakini wewe ndio unalazimisha kuweka hili neno lingine, kuna tofauti kati ya kiganja (palm) na Mkono (Arm) simu inashikwa na kiganja kwanini aseme simu ya mkono?

Lugha sio ngumu bali sisi ndio tunaifanya iwe ngumu kwa kutaka kuweka maneno yetu ambayo tunahisi ni rahisi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom