Taasisi ya IPSOS na utafiti feki juu ya Cloud Fm

frema120

JF-Expert Member
Jan 1, 2012
5,099
1,338
IPSOS sijui ni Taasisi ya nini Tanzania, ilifanya shindano la kutafuta watangazaji bora katika segments mbalimbali na vipindi vywa radio bora katika radio mbalimbali pia.

Sasa cha kunishangaza vipindi vyote cloud fm ni namba moja!!???, watangazaji wote wa radio ni namba moja!!??.
(Source: Cloud fm matangazo ya kila mara)

Baraza la Habari wapo kimya tuuu, kweli inawezekana hali hii ikawa ndio ukweli, tuna radio zaidi ya 50 tanzania zenye vipindi vingi sanaaa. shida nini??? hadi kudanganya.
 
Unahitaji Kuwa Na Moyo Kama Wa Mwendawazimu Kuanza Kuijadili Hiyo Redio Kwani Ina Mapungufu Mengi Mno Ya Kiueledi Na Wanaboa Sana Tu.
 
Tafiti ya waliopungukiwa akili, mie siwezi kukaa nisikilize radio ya wambea ndio maana hata hilo tangazo sikulisikia
 
Hiyo taasisi ndio iliyotangaza eti said kubenea ndio mwandishi mahili namba Tanzania ,virojaaa.
 
Hiyo radio ina kipindi kimoja moja tu cha michezo vingine ni utumboutumbo.
 
ndio muhimili tunao utafuta sisi waandishi kwa vituko kama hivi hatufanikiwi
 
Hao jamaa ni feki sana..eti presenter bora wa habari za michezo ni shaffi Dauda??? jamaa hata kusema sentensi moja iliokamilika kwa lugha ama ya kiswahili au kiingereza ni shida.
 
Sijui walipambanisha na Radio gani hadi clouds wakabeba makombe yote.
 
Mkuu hiyo taasisi ni yao wala usipate tabu nao. Kila mtu anasifia cha kwake. Bado wanajitangaza wape muda wakikua wataacha
 
Eti kipindi namba moja cha kaunti dauni za habari tanzania,hebu jiulize hicho kipindi walishindanisha na kipindi cha redio ipi ambayo inakipindi kama hicho ili kiwe namba moja!!!?
 
Eti kipindi namba moja cha kaunti dauni za habari tanzania,hebu jiulize hicho kipindi walishindanisha na kipindi cha redio ipi ambayo inakipindi kama hicho ili kiwe namba moja!!!?

Hao jamaa hawawezi kuingia kwenye kinyang'anyiro cha ushindani wa redio za bongo na vipindi kwa sababu wao hawana level ya professionalism hata kiduchu. Pale maadili ya utangazaji hamna. Yeyote anaweza kuachiwa redio akaendesha kipindi. Wao kipaji ni kuweza kuongea tu on air basi. The only exception nnayoiona pale na ubunifu mkubwa ni Amplifaya. Millard anajitahidi sana kile kipindi chake anaweza kukuza redio yoyote kikauzika. Hao wengine wababishaji tu kazi kupigana studio na kuvuta bangi na kilevi. Yangu nimeanza kusikiliza redio hapa Tanzania nadhani ni hiyo tu ndo nimesikia watu wanapigana studio hewani. Bangi mbaya sana esp ukiingiza mahala pa kazi. Na wakianzisha category ya kupigana studio wao ndo watakuwa hawana mpinzani. Wajitangaze na hiyo basi tujue.
 
Back
Top Bottom