Taasisi ya Hassan Maajar Trust ni ukombozi au biashara? serikali imeshindwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Taasisi ya Hassan Maajar Trust ni ukombozi au biashara? serikali imeshindwa?

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by VIKWAZO, Jul 11, 2011.

 1. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #1
  Jul 11, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  [TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
  [TR]
  [TD][​IMG][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: tr-caption"]Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Salma Kikwete (kulia) akizindua nembo ya (HMT) kwaajili ya uzinduzi ya Taasisi ya Hassan Maajar Trust na kuanzisha kampeni ya kusaidia kutokomeza uhaba wa madawati mashuleni jijini Dar es Salaam (juni 11.2011) (kushoto) ni Makamu Mwenyekiti wa Taasisis hiyo Shariff Hassan Maajar ,akifuatiwa na Mwenyekiti wa HMT Balozi Mwanaidi Maajar[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  [TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
  [TR]
  [TD][​IMG][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: tr-caption"]Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete (kulia) leo (julai 11,2011) akibadilishana mawazo na Seneta JACKIE WINTERS kutoka Marekani (kushoto) alipomtembelea ofisini kwake jijii Dae re Salaam .[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  [TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
  [TR]
  [TD][​IMG][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: tr-caption"]Mwalimu mkuu shule ya msingi ya Amani DSM Eliwaza Shirima akichangia kwenye mkutano[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]


  [TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
  [TR]
  [TD][​IMG][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [/TR]
  [/TABLE]  Kama huyu balozi huko marekani anaweza serikali yake imeshindwa nini?
  au huu ni mradi wa kuombea hela matajiri wa marekani kwa kisingizio cha madawati?
  mama salima anauzindua TAASISI ya mabozi kama nani?
  inapobeba jina la mwanafamilia wa balozi na kuzinduliwa na balozi na first lady kuna hapa?
   
 2. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #2
  Jul 11, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Hii taasisi inaanza na maseneta kuitembelea , nina wasiwasi ofisi za ubalozi wetu huko NW YORK ni pango la biashara,
  serikali ilisha sema charge ya rada inaweza kutatuma matatizo ya madawati sasa hapa inakuwaje DAR-ES- SALAAM inavamiwa na wana new york?
   
 3. F

  FJM JF-Expert Member

  #3
  Jul 11, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  I dont like this story kabisa! Ina harusi mbaya!
   
 4. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #4
  Jul 11, 2011
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Wezi katika kushirikiana kutafuna keki ya Taifa, huu ni mpango katika ile mipango khe khe khe kheeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee poor Tanzanians.
   
 5. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #5
  Jul 11, 2011
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,434
  Likes Received: 2,303
  Trophy Points: 280

  "You know achuman ndavanda go to ze river. Mamba kumkamata kumsorasora, mahundi na matumbo yote finish!!
   
 6. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #6
  Jul 11, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  hii yako kiboko lakini nadhani ulikuwa na hasira sana umetukana kwa kilugha chako kukwepa BAN

  KIKWETE mshikishe break first lady unaweza kustaafu na mke mwenye tuhuma nzito kuliko mama mkapa
   
 7. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #7
  Jul 11, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  huyo mme wa balozi naona kama ana wasiwasi hana uzoefu na dilli za kuchomekea nini?
   
 8. p

  politiki JF-Expert Member

  #8
  Jul 11, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  mwenyekiti wa taasisi ni mwanaida maajar na makamu ni sharrif maajar hii taasisi inaonekana kama ni ya kifamila zaidi badala ya kuwa ya kuwa na muonekano wa kitaifa zaidi. lengo na nia ni nzuri lakini kunaweza kutokea kikwazo ktk uwajibikaji ni ngumu mke kumwajibisha mume au mume kumwajibisha mkewe makosa yanapotokea na ni rahisi kwa taasisi kuongozwa kwa personal feelings which is lethal in any business transaction
  badala ya kuzingatia professionalism. ushauri wangu kwao ni kwamba ingekuwa vizuri wao wangeingia kwenye board of trustees na kuwaachia
  wengine waendeshe taasisi kwani inakuwa rahisi kwao kumonitor all the activities na kurekebisha makosa kuliko wao kuwa ndio wakurekebishwa.
   
 9. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #9
  Jul 11, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,102
  Likes Received: 22,142
  Trophy Points: 280
  Wakati wa Nyerere balozi zetu zilikuwa kisiasa, mambo hayo yamepitwa na wakati zamani sana. Sasa mambo ni biashara kwa kwenda mbele. Badala ya kukaa mkawa negative kwa kila kitu, hebu anzeni kuwa wabunifu na kufanya mambo ya maendeleo. Nafasi za kujijenga ni nyingi sana Tanzania. Wacheni majungu yasiyo na mpango.
   
 10. Limbani

  Limbani JF-Expert Member

  #10
  Jul 11, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1,438
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Ni wazo zuri, lakini nina wasi wasi na nia yao!! Hizo fedha zitafika kweli zote kwenye hayo madawati? au ni kukinga bakuli tu watu wajalie..
   
 11. b

  bulunga JF-Expert Member

  #11
  Jul 11, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 290
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Ni kweli huyu mama yupo kibiashara zaidi angalia hii Malaika Kids UK
   
 12. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #12
  Jul 11, 2011
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  With love from London to New York it is all about money, money and money - the famous money trail ! Kwa njia hii tusishangae kwa nini safari za Marekani zimepungua, si ofisi ya kudumu imepatikana Washington bila jasho na kwa hela ya walipa kodi masikini wa Tanzania. Madawati ? Ha, ha, ha !
   
 13. N

  Ndjabu Da Dude JF-Expert Member

  #13
  Jul 12, 2011
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 3,648
  Likes Received: 408
  Trophy Points: 180
  Huyu mama hivi majuzi alikuja na group la Wafanyabiashara wakubwa kutoka Marekani, ambao aliwafanikisha kuonana na Dikteka JK Ikulu. Kama mwanae alifariki 2006, kwa nini asubiri miaka yote hii hadi leo kumuenzi? Go figure!
   
 14. p

  politiki JF-Expert Member

  #14
  Jul 12, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  huyu si ndiye yule mama alikuwa balozi uingereza akapata kashfa ya ubadhirifu wa pesa chungu mzima, leo hii anataka kukusanya pesa za madawati
  simpi pesa yangu mpaka aeleze kuhusu ubadhirifu ule uliotokea chini ya usimamizi wake .
   
 15. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #15
  Jul 12, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  huyu mama kaligeuza taifa mradi bana, amefanya hivyo kwenye madini sasa nazoa hela ya maseneta kwa jina la madawati.
  mwizi hawezi kuacha mpaka atiwe adabu
   
 16. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #16
  Jul 12, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Katika wachangiaji wote katika thread hii naona wewe ndio uliyefunguka kimawazo. Wengine wote wanaendekeza siasa na kusahau uchumi.

  WaTanzania lazima muwe na mtazamo chanya. Balozi za nchi zote hapa Duniani zinafanya kazi za kutangaza na kuvutia mazuri kwa ajili ya kukuza uchumi wa nchi zao. Kwani Bila uchumi hakuna maendeleo. msiendekeze siasa zenu za chuki kwani hizo haziwezi kuwasaidia na mtaendelea kuwa nchi maskini tena maskini wa kutupwa hapa Duniani.

  Ndio maana Wakenya wanatangaza mambo yenu kama Mt Kilimanjaro na hata Babu wa Samunge wapo kenya , Nyie wenyewe mnakalia siasa.

  Labda mjifungue, Ni nani mtanzania ambaye ni msafi? Fungukeni na mbadili mitazamo yenu iwe ni kwa ajili ya kuendeleza uchumi wa nchi yenu.
   
 17. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #17
  Jul 12, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,102
  Likes Received: 22,142
  Trophy Points: 280
  Ndivyo inavyotakiwa, nna uhakika huyu mama ni kichwa na amejaalia ajira nyingi kwa ubunifu wake.
   
 18. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #18
  Jul 12, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Mke wa Rais na notebooks!!!!

  [​IMG]
   
 19. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #19
  Jul 12, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Binafsi leo asubuhi sasa mbili na robo kwenye kipindi kimoja cha Radio ya Clouds FM, Huyu mheshimiwa Bi Mwanaidi alikuwa anafanya mahojiano. Nilifurahia sana wazo na mradi wake kwni una nia ya kutengeneza Madawati na kusambaza mashuleni lakini pia kuendeleza michezo hususan basket ball.

  Na akatoa changamoto watu kuchangia taasisi hii na kubainisha Ofisi zake zipo ARCADE huko mikocheni njia ya old bagamoyo. hapo pana duka ambalo mtu anaweza kupeleka kitu chochote kile hata kikiwa second hand na kikauzwa kwa nia ya kupata Fedha.

  Mimi nawashauri WaTanzania mjifunze kuchangia maendeleo na sio harusi na mengine ya hanasa.

  Kwa tuliosoma ILBORU enzi za BINO. mmoja wa Board member wa Taasisi hii ni Mama KAMU aliyekuwa Mkuu wa shule ya wasichana WERUWERU. nafikiri wanaomjua wataliona umakini wake.

  Inshallah nikirudi kesh dar kutoka hapa mwanza Nitapita hapo kuchangia kidogo nilichonacho kabla sijaondoka kurudi kwetu.

  Kumbukeni maendeleo ya watanzania hayawezi kuletwa na wafadhili kutoka nje bali yataletwa na watanzania wenyewe. Vijana kuweni na positive ideas na kuondokana na chuki za kisiasa.
   
 20. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #20
  Jul 12, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,102
  Likes Received: 22,142
  Trophy Points: 280
  Ni ukweli usiopingika kuwa chuki kwa biashara na wafanya biashara ilipandikizwa na Nyerere, kila aliyeweza kuwa na kipato wakati wake, alikuwa ni "bepari" na "mnyonyaji" akafikia kutaifisha mali za watu fulani kwa sababu tu alikuwa na roho dhaifu kwa yoyote mwenye mali. Alifikia mpaka kuwatia ndani watu waliokuwa na biashara za maana, mfano mzuri "Lord" Rajpar.

  Hiyo sumu ya nyerere mpaka leo iko, kila afanyae biashara au akiwa mbunifu kama huyu dada, basi huwa ama mnyonyaji, au mwizi, bepari, kwa sababu tu, baada ya Nyerere kutaifisha mali za watu na karibu kila kitu kuwa mali ya umma, njia ya kujipatia kipato ilikuwa ni wizi tu, uibe, ufiche.

  Tukitaka kujikomboa na kuwa na roho kunjufu za ubunifu, zifanywe jitihada za ziada kuwaelimisha wa Tanzania kuwa wabunifu wafanya biashara na wajasiriamali, Hayo ndio mambo ambayo inatakiwa tuyavalie njuga kwa nguvu zetu zote ikiwa tunataka maendeleo.

  Ieleweke kuwa hata zile nchi tajiri kabisa duniani, maendeleo hayaletwi kutoka serikalini, maendeleo huletwa na wananchi wenyewe, leo hii hata iweje kama bado tuna mawazo duni basi na maendeleo yetu yatakuwa duni siku zote.

  Tulijazwa ujinga, tuufute. Wenzetu wanaofanya mambo mazuri ya kujiendeleza tuwaunge mkono na wawe ndio mifano ya kuwaiga na sisi tufanye zaidi. Bila kuwa na moyo wa kujiboresha hatutafika mbali na kila siku tutaona watu wa nje kuwa ni maadui, la hasha, si maadui, wao wakija huku wanayaona ambayo hakuna na yanaweza yakawaletea faida ndio wanayafanya.
   
Loading...