Taasisi ya elimu tanzania, siyo jukumu lenu kuandika na kutathmini vitabu

Mapigomoto

Member
Jan 21, 2016
19
11
Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) shughuli yenu ni kuhakikisha uwepo wa mitaala, mihtasari na pia ufuatiliaji wa utekelezaji wa hayo.

Kwa sasa TET wanaona kuwa vitabu vilivyoko shuleni ni vibaya, basi wameamua waandike wenyewe. Walimu ni wabovu, basi waamue kufundisha wenyewe. Watathmini wa vitabu ni wabovu, basi wameamua watathmini wenyewe. Tabia hiyo inayumbisha shughuli za uimarishaji wa taaluma katika shule zetu.

Kwa sababu mnataka huku na huku, ona sasa. Mnasema kwenye mihtasari yenu kuwa, Umahiri unafundishwa darasani. Nani aliwaambia kuwa Umahiri hufundishwa? Hii ni sawa na kusema kuwa majibu ya maswali katika somo la Hisabati hufundishwa. Mngezingatia kazi yenu, tatizo kama hilo mngeliona. Msiwaze sana pesa. Mjue wazi kuwa vitabu vya darasa la kwanza mlivyoandika ni vibovu na havifai kabisa. Hivyo ninyi wenyewe ni wabovu.

Kazi za kuandika vitabu na zile za kutathmini vitabu sio kazi za Taasisi ya Elimu. Kama kuna kasoro katika uandishi wa vitabu au tathmini ya vitabu, marekebisho yafanyike na wanaohusika na usimamizi wa upatikanaji wa vitabu.
 
Back
Top Bottom