Taasisi Gani iondolewe kabisa katika aktiba mpya?

YeshuaHaMelech

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
2,597
37
Jamani,
unaona taasisi gani ivunjwe kabisa na ifutwe kabisa toka ktk katiba. Sio tu kwamba iundwe upya bali ifutwe kabisa!
Karibuni!
 
Wakuu wa Wilaya na Mikoa waondolewe kabisa
Teuzi za Raisi zipunguzwe na nyazifa nyingi ziwe za kuomba
 
wakuu wa wilaya waendelee kuwepo ila wakuu wa mkoa na jopo lao lifutiliwe mbali,
-Taasisi ya haki za binadamu iwe kitengo chini ya wizara ya sheria na katiba na isiwe taasisi inayojitegemea
-Tanzania Investment ifutwe kabisa sitaki kuisikia,Wizara ichukue jukumu
-Wizara zote chini ya Ofisi ya Makamu wa Raisi,chini ya Raisi na chiny ya Waziri Mkuu ziondolewe,ziwe idara ndani ya ofisi
-Tume ya uchaguzi iteuliwe na bunge na iwajibike kwa wananchi
-Raisi atawale kwa miaka mitano tuu inatosha
-Wabunge wawe na kikomo miaka kumi inatosha kabisa
 
Jamani,
unaona taasisi gani ivunjwe kabisa na ifutwe kabisa toka ktk katiba. Sio tu kwamba iundwe upya bali ifutwe kabisa!
Karibuni!

Mkuu,

mimi ningefurahi kuona Serikali ya Muungano na taasisi zake zote zifutwe na badala yake iundwe serikali ya Tanganyika na bunge la Tanganyika na taasisi zake hasa kwa vile tunasherehekea sherehe za 50 za uhuru wa Tanganyika.

well, sio hasa ifutwe lakini ifanywe iwe ndogo sana. tuwe na shirikisho ndani ya shirikisho.
 
Ziondolewe taasisi zote na kuanzishwa chache mpya. Taasisi nyingi ziemanzishwa kinyemela ili kuwapa watoto wa vigogo ajira na mishahara minono...

unakuta taasisi imejaa kabila moja au dini ya aina moja tu. Useless....
 
tume zote zifutwe kazi zifanywe na wizara husika; iwe marufuku kuunda ispokuwa kama kuna janga na dharula
 
Ziondolewe taasisi zote na kuanzishwa chache mpya. Taasisi nyingi ziemanzishwa kinyemela ili kuwapa watoto wa vigogo ajira na mishahara minono...

unakuta taasisi imejaa kabila moja au dini ya aina moja tu. Useless....

zitaje basi ambazo ungependa zifutwe kabisa! Ukitaja kwa majina ni rahisi kuzijadili
 
so far so good, karibuni wengine pia mtuambie! Taasisi gani hai perform ifutwe? Na mimi niongeze tu:
takukuru ifutwe,
Tiss ifutwe iundwe taasisi nyingine ya kusimamia mambo ya kijasusi, iajiri upya kabisa!
TTCL ifutwe na TCRA pia. Iundwe taasisi moja itakayosimamia majukumu yote ya taasisi hizi.
 
mkuu,
Hukupenda pendekezo la kuifuta serikali ya muungano na kuunda serikali ya Tanganyika?
Hii itatusaidia sana kufikia hatua unayoitaka kuunda taasisi zetu upya!
 
  1. takukuru
  2. wale wanaoitwa sijui mawaziri chini ya ofisi ya rais na waziri mkuu hawana cha kufanya, ziwe ofisi za kawaida tu wanatumia hela bila kazi yoyote ya msingi.
  3. wakuu wa mikoa, wilaya.
  4. wabunge wa kuteuliwa.
 
Wabunge wa kuteuliwa, Taasisi ya rais, pamoja na wizara ya utawala bora,na wamaziri wote ktk ofisi ya waziri mkuu.
 
Hapa napo nami niweke wazo langu dogo nikiwa nina maana ni mdau mdogo wa katiba mpya hapa nyumbani tanzania wapo pia wadau mimi nawaita wadau wakuu nikiwa na maana si wasomi tu bali pia ni wasomi katika katiba hawa wanaweza wakawa wanasheria na sio wazazi wangu walio kule katika vijaruba vya mpunga kule mabwawani ambao hata ukiwaambia katiba mya ni kuzuia mvua basi wataipinga wakijua vijaruba vitakosa maji na mwakani watakufa njaa...hivyo suala laweza kuwa si kubadili taasisi au jina lake maana hata kama jina lake litakuwa ni UCHAWI ila kama kilichomo ndani ya taasisi iitwayo UCHAWI ni faida kwa watoto wangu,wajukuu zangu na vilembwe vyangu basi mimi sioni kunasababu ya kubadilisha taasisi mbalimbali kwa ngozi yake bali iwe kwa nyama yake.....ukitaka nyama iwe nono basi hatuna sababu ya kuichukia ngozi yake bali tumpe malisho ng'ombe mwenye ngozi mbaya ili atupe nyama nono...nadhani tupo.
 
Back
Top Bottom