Taarifa za Zitto na Dr. Kitila kwa Umma Juu ya Kuvuliwa Nafasi za Uongozi ndani ya CHADEMA

Status
Not open for further replies.
Huyo ndiyo anakufa taratibu kisiasa hasa
kipindi hiki ambacho bila kulinda kinywa
chake vema huenda ikabaki historia tu ya

Huyo mtu anayeitwa ZZK lakini hao anao
kula nao ndiyo wamechoshwa na dhambi
huoni sasa kila kitu kiko wazi.
 
Mkuu najua unampenda sana Zitto kiasi cha kuweza kuwa nje ya control kabisa kuliko zitto abanwe ktk kona.

Well, naona umekubali kupotoka hapa:ZITTO KWA SIFA ALITAKA SEMA CHADEMA WALIMLAUMU KWA KUTOWATONYA ,KWA AKILI YAKE ANAPIGA POINT BIL AKUJUA HASARA KM KAWAID AYAKE KUTOKUWA RESPONSIBLE.KI UKWELI NI KWAMBA HAYO MAMABO ALIAYOKOMAA NAYO KUPITI AKAMATI YA BUNGE KWA CHAMA NDIYE ALIPASWA YAFUATILIA YAFANYWE.YEYE HAKUFANYA KWA VILE HAKAI OFFISINI.NA NDIO MAANA HAKUTEGEMEA KUWA MATOKE O YANGEKUWA TOFUATI.

kwanini sasa atake point kw akitu alichpaswa fanya.Na nyinyi wana CCM mnakuwa wepesi sana kupotezea ??? ili mpate faida.

USHAURI KWA ZITTO: MAJUNGU UNAYOPIGWA YANATOKANA NA KUTOKUJENGA UHUSIANO BINAFSI NA WENZAKO

Tatizo la Zitto sio ukanda, udini, ukabila, usomi na siamini Waraka ambao wanasema Zitto anahusika kwasababu umeandikwa kitoto sana.

Tatizo kubwa la Zitto na Chadema ni uhusiano binafsi na watu anaofanya nao kazi. Ukweli ni kwamba kazi ni zaidi ya sera, sheria za kwenye vitabu.

Viongozi wengi ni watu wa kawaida na wana uhusiano wa karibu hata wa kifamilia tumeona Kikwete analala kwa magufuli kwasababu Magufuli amegundua uhusiano binafsi ni njia moja wapo ya kufanikiwa kwenye jambo lolote. Hivyo Zitto hayo majungu yanatokana na kutokuaminiana kwasababu hujachukua muda kuweka mahusiano ya karibu na watu unaofanya nao kazi na hili ni tatizo kila mahali hata kwenye biashara au kazi nyingine.

Je unajua familia za wenzako, unajua wameamkaje asubuhi, unajua matatizo waliyonayo kama wagonjwa nyumbani? haya yote ni muhimu kwa watu unaofanyakazi nao sehemu moja. Vitabu vipo, sera zipo na sheria zipo lakini kwenye Chama kama Chadema ambacho ndicho kinakuwa na viongozi wachache kutupiana maneno kwenye mtandao inaonyesha hakuna mahusiano binafsi ambayo mnaweza kuongea kwenye chai ya asubuhi na kumaliza.

Hakuna jambo duniani linalofanikiwa kwa sera pekee bali mahusiano ni muhimu sana. Vilevile ni lazima uelewe mahusiano ni kati ya mambo muhimu ambayo ni lazima ukubali kama ni upungufu wako na kulifanyia kazi kama alivyofanya magufuli.

Magufuli pia alikuwa anaogopwa na JK na wengine kwa misimamo lakini aligundua hilo na kujenga mahusiano.

Zitto unakipaji na huna sababu ya kuwaeleza watu hilo kwasabbau kipaji ni kutoka kwa mungu na hakuna anayeweza kukichukua hivyo focus on your weakness.

Huu ni ushauri wangu kujibizana nani yuko sawa na nani hayuko sawa haitakusaidia popote pale na kwenye chama chocote au biashara.
Kitakacho kusaidia ni mahusiano-relationship.

Source : http://www.udakuspecially.com/2013/11/ushauri-kwa-zitto-majungu-unayopigwa.html?m=1
 
Mbowe na chadema wanapaswa kuturidhisha juu ya
yaliyoandikwa kama madhaifu yake kwenye Mkakati wa mabadiliko 2013 ndani ya
taasisi...... atolee ufafanuzi hata kama
itamgharimu..

anapaswa atoe ufafanuzi wa dhaifu moja baada ya jingine ili kutudhihirishia umma kwamba waraka ule ni wa uchochezi na uhaini.

Kapitie maoni ya Dr. Lwaitama then rudi tena hapa... Mipango yoyote ya siri juu ya Uongozi katika taasisi yoyote yenye nia ya kumuondoa au kuondoa uongoz uliopo kinyume na katiba ni uhaini... Full stop.
 
CREDIBILITY YA ZITTO KABWE NA ALIYOONGEA YAZIDI KUSHUKA ZAIDI.
Ndugu wana jamii forum, Natambua wengi wetu tumelewa na umahiri wa Mh Zitto Bungeni tukasahau kabisa kuwa kwenye Siasa Credibility ni moja ya nguzo kuu za’’ Ethics za mwanasiasa’’.
Mashaka kwa Zitto ni mengi sana, Toka alipoombwa na Wazee wa chama kuondoa form yake ya kugombea M/kiti wa CHADEMA Taifa na akafanya hivyo kinafiki [Zitto hakuridhia moyoni] hadi aliposimamishwa Uongozi Zitto kakipitisha chama sehemu za hatari hatari.
KWANINI UCHAGUZI WA KUMUWEKA MH NASSARI HAKUWAHI HATA SIKU MOJA KUMPIGIA KAMPENI WAKATI CCM KARIBU WOTE WALIHAMIA ARUMERU?
Mimi huyu Bwana nilianza kumtilia shaka zaidi hapo, pamoja na umahiri wake wakujieleza lakini Zitto sio HONEST kwa chama? Viongozi wengine wapo bussy na kampeni yeye anaibuka na kusema Nataka Kugombea Uraisi[ wewe ukishaona kiongozi yeyote wa Upinzani anasifiwa na Mwigulu & Nape jua tu hawana madhara kwa chama chao], Uraisi wa kuwa na wabunge 37 tu? Kwanini usihangaike wabunge waongezeke kama kiongozi shupavu!. ‘’Zitto kumbuka kuwa ni heri kuwa Porini kwenye kila dalili za hatari kuliko kuwa chumbani kwako huku umejiachia lakini kuna nyoka mwenye sumu kali’’.
KWANINI UVCCM WASHIRIKI KUANDAA MKUTANO WAKO ZITTO?
Hebu soma hapa nukuu toka Gazeti la Mwananchi.
Leo, uongozi wa Chadema umeitisha mkutano wa waandishi wa habari ambao pamoja na mambo mengine, utajibu baadhi ya hoja za utetezi ambazo zilitolewa na Zitto pamoja na Dk Kitila. Katika mkutano wa juzi, Zitto na Dk Kitila ambaye alikuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, walizungumzia kuvuliwa kwao madaraka, lakini maandalizi na uendeshaji wa mkutano huo yanazua shaka kutokana kuwahusisha watu wanaodaiwa kuwa ni wanachama wa Jumuiya ya Vijana ya Chama cha Mapinduzi (UVCCM).
Miongoni mwao, wamo waliowahi kuwa wanachama wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha), Habib Mchange na Mtela Mwampamba ambao walitimuliwa kwa makosa yanayofanana na yale yalizosababisha Zitto na wenzake kuvuliwa nyadhifa zao.
Mchange na Mwampamba pamoja na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Bavicha, Juliana Shonza, walivuliwa uanachama wa Baraza hilo Januari 5, mwaka huu baada ya kupatikana na hatia ya kutumia mitandao ya kijamii kukihujumu Chadema na kuwatukana viongozi wake wakuu. Baadaye walihamia CCM wanakoendeleza harakati zao za kisiasa.
Jana, Machange alipotafutwa, alisema: “Mimi sikuwahi kuondoka Chadema, nilifukuzwa kihuni kama walivyowafanyia Zitto na Kitila. Nimepeleka malalamiko yangu tangu Januari hadi leo sijajibiwa, hivyo siwezi kusema nimeondoka.
Nataka nimuunge mkono mwathirika mwenzangu kama ilivyokuwa mimi lakini nitabakia kuwa mwanachama mwaminifu.
“Mimi ni mwanaChadema na sikuwahi kujiunga na CCM au chama chochote, walioondoka ni Mwampamba na Shonza.” Mwampamba alisema: “Nilijitokeza pale kuonyesha mshikamano kwa sababu mimi pia ni mwathirika. Kwa hiyo nilitaka ulimwengu ufahamu kuwa mimi ni kati ya wanaopinga siasa za aina hii... Chadema ni chama kinachojiandaa kuchukua dola, sasa kama kila mwenye mawazo tofauti anaonekana mhaini itakuwaje siku wakichukua dola? Ubaguzi huu haujalishi uko chama gani, hata kama niko CCM, hilo halinizuii kuungana na mtu aliyepatwa na tatizo kama langu.”

 
Mbowe na chadema wanapaswa kuturidhisha juu ya
yaliyoandikwa kama madhaifu yake kwenye Mkakati wa mabadiliko 2013 ndani ya
taasisi...... atolee ufafanuzi hata kama
itamgharimu..

anapaswa atoe ufafanuzi wa dhaifu moja baada ya jingine ili kutudhihirishia umma kwamba waraka ule ni wa uchochezi na uhaini.

kwani ninyi ni kina nani?
 
kuwaadhibu watu wanaokuambia madhaifu yako ni uzuzu

Kuna Presidaa aliyepata kuwa na madhaifu kama huyu tuliye naye... Lakin nani ndan ya kijan anayeweza thubutu kutia neno nje ya utaratibu wa chana... Huyu jamaa tenu tuna hesabu siku za kumvua uanachama... Hatuwezi muacha hata kidogo... Jamaa nu smart sana kama vipi mchukueni... Kwani chama ni chadema tu... Si aje chama tawala na uwaziri mumpe.
 
Huo waraka ukiusoma nizuri utagundua makosa kibao ya kitaalamu hadi napata shida kuamini kuwa ukiandaliwa na Dr. Kitila. kama ndo hivyo basi uelewa wake na hao wenzie ni wa chini mno.Kwa kifupi tu niataaisha machache.

1. Wanaonyesha takwimu jinsi chama kilivyoongeza wawakilishi tangu watatu mwaka 1995 hadi 49 mwaka 2013: lakini bado wanadai kiongozi aliyefanikisha mafanikio haya ni dhaifu hivyo hawana budi kumtoa.very poor analysis!
2. Wamedai elimu ya mbowe ni ya kimagumashi, hata vipaji vya kuzaliwa hana, Mbowe ndiye mwenye elimu ndogo kuliko viongozi wengine wa taasisi.
Hii imenishangaza sana.kuna makala iliwekwa humu kuwa Mbowe anajiendeleza kimasomo nchi za ulaya kwa shahada ya kwanza na ya uzamili. Dr. Kitila akasapoti mpango huo na kumsifia mbowe. Sasa imekuwaje tena hiyo elimu ambayo ilionekana ilifaa sasa imekuwa ya kimagumashi? unadhani ili kuwa kiongozi wa chama unahitaji elimu gani? jaribu kuulizia elimu za hawa wafuatao ili upate kuelewa; Mzee Mwinyi, Kawawa, Mzee Makamba,Mzee Mrema, Mzee Mangula, Zuma Afrika kusini n.k.
3.Matumizi mabaya ya fedha: Walipaswa kuliwasilisha kwenye vikao vya chama ili lijadiliwe na kama majibu hayajitoshelezi ndipo wangetoa hitimisho kuwa kunaufujaji wa pesa, nk. vinginevyo ni majungu na kuchafua viongozi wao wa chama.
4. Wanadai Zitto ni kiongozi anayeweza kuongoza taasisi bila makundi: mpaka hapa wameshajitoa ufahamu na kujivika upofu. Kwa mtu yeyote hata asiye mwanachadema anajua fika kuwa Zitto ni mtu wa makundi na anapenda mno sifa binafsi kuliko maslahi ya nchi hata chama chake.
5.Wanadai Zitto ni msomi wa hali yajuu na uwezo wa kuchanganua hali ya uchumi, kisiasa na kijamii: Hilo ni sawa ni kweli amesoma shahada ya uchumi chuo kikuu cha Dar es salaam. Isipokuwa nina mashaka kuhusu uwezo wake wa uchambuzi hasa pale nilipomsikia kwenye kipindi cha television siku moja akibeza watu waliopata Lower Second kuwa viongozi wa serikali na taasisi za umma. Hapo nilimshangaa sana Zitto kwa sababu kigezo cha alama za darasani hakiwezi kuwa kigezo pekee cha mtu kuwa kiongozi. Mjadala mwingine nilimsikia yeye na Mwigulu ambapo wote waliishia kujisifia uwezo wao wa darasani na alama za juu kiasi cha kupotea kabisa kwenye mada husika. Kwa maoni yangu, huwezi kutumia kigezo cha ufaulu darasani pekee kama ni sifa ya uongozi.

6.Wanakiri kuwa Zitto ni mropokaji, ana jazba na sio mstahimilivu: cha kushangaza wanajitia upofu kwa kudai tatizo hilo linarekebishika, sijui wana uhakika gani kubadili tabia ya mtu aliyozaliwa nayo? huu ni ushabiki usio na maana. Sifa kuu ya kiongozi ni uwezo wake wa kukabili kila jambo pasipo jazba, anapaswa kutafuta ufuumbuzi wa mambo yanayoisibu taasisi yake kwa hekima ya juu pasipo kukurupuka. katika hili uvumilivu ni sifa kuu ambayo Zitto hana. Hii ni tabia inayojengwa kutokana na ama kuzaliwa nayo ama makuzi, malezi aliyopata katika jamii. Ajabu wapambe wa Zitto wanadai hili linarekebishika! utamrekebisha Zitto sasa hivi?

Kwa hayo machache, nadhani anaysis yao ni ya hali ya chini kwa sababu haijazingatia hali halisi. na kama uchambuzi wao umebaini kuwa Zitto ndiye anayefaa basi nina shaka kubwa na uelewa wao. Vinginevyo tuambiwe kuwa kuna ajenda iliyofichika na ---- mtu kawatuma wafanye hiyo analysis kwa sharti la kumbeba zitto licha ya mapumgufu yake ili kuleta mgawanyiko ndani ya chama.
 
Hahahahahhahaha

Mkuu MuIsrael. Hapo umechanganya madesa. Muasisi wa siasa za kilaghai nchini ni Mtei. Mfuasi madhubuti wa siasa hizo ni Dr. Slaa...

Hapo wewe ndio umechanganya madesa...!!
Umefuatilia responses za makamanda Mnyika na Lissu..??
Zitto kajitungia shutuma, kajijibu mwenyewe...!!
Zitto is out, nine days to full unemployment for Zitto...!!
Zitto atakuwa mzigo m-Zitto kwa CCM, maana atakuwa hana kazi, hana mke, hana chama, hana ubunge, kila kitu 'nehi'.......!!!!
Zitto ni mwanasiasa mlaghai (aliyefukuzwa) kama Lowassa....!!!
"....Zitto ni mwanasiasa mlaghai...." - by ZeMarcopolo.
 
Hatutamwamini kwa sababu CCM ina vipngozi wengi walio tayari kwa moyo mkunjufu kuwasaidia vijana wao mawazo ya kimaendeleo.

..exactly!!

..siasa zetu za vyama vingi hazijakomaa kiasi cha kuruhusu mwana CDM kuwa na mahusiano ya karibu na viongozi wa CCM kama anavyotaka Zitto Kabwe.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom