Taarifa za Zitto na Dr. Kitila kwa Umma Juu ya Kuvuliwa Nafasi za Uongozi ndani ya CHADEMA

Status
Not open for further replies.
Mzee kama Mtei HAFAI kuwa mentor wa mwanasiasa progressive.

..OK, lakini wazee wengine wapo huko CDM na hatujamsikia Zitto akisema yuko karibu na wazee hao.

..hivi akitokea mwana CCM akatamka kwamba Mzee Mtei ndiyo political mentor wake, na Dr.Slaa ni "baba yake" au "mzee wake" kweli ktk siasa za kileo mtamwamini mwanachama huyo ktk nafasi nyeti za uongozi?
 
..hivi akitokea mwana CCM akatamka kwamba Mzee Mtei ndiyo political mentor wake, na Dr.Slaa ni "baba yake" au "mzee wake" kweli ktk siasa za kileo mtamwamini mwanachama huyo ktk nafasi nyeti za uongozi?

Hatutamwamini kwa sababu CCM ina vipngozi wengi walio tayari kwa moyo mkunjufu kuwasaidia vijana wao mawazo ya kimaendeleo.
 
Sijazungumzia makosa aliyopewa nimezungumzia swali lako lililouliza bila kukunukuu, je angewataarifu kwanza chama?

Kama haya ndiyo maelezo mbona taarifa ya kikao hiki kilionyesha kutolewa taarifa ya fedha za chama, je aliingia kwenye hicho kikao? Kwakua siyo kiongozi sifahamu undani wa unayoyazungumzia lakini pia kama kulikuwa na hilo tatizo la kifedha si angetoa huo utetezi? Mbona anakimbilia kutoa utetezi usio na mashiko?

To be honest with you, wewe ni shahidi tulimweleza huyu jamaa hapa hapa JF anavyoonekana kwenda kinyume na wenzake ndani ya chama sasa leo ni kipi kitatufanya mm na wewe tuamini hayo maneno yake huku tabia yake public ikiwa obvious?

Labda unipe update ya wewe uliwezaje kuamini baadaye huku mkiniacha mimi njia panda kama tulivyokuwa wote hapo mwanzo!
Mkuu wangu kitu kimoja tu ni kwamba ZZK hakuwa na haja wala sababu ya kuwashtua CDM ikiwa swala la kuwakilisha matumizi ya kila mwaka ni sheria ambayo kila chama kinatakiwa kufanya.

Pili, nijuavyo mimi kutokana na maelezo ya viongozi wa CDM ni kwamba wao tayari walikwisha wakilisha mahesabu yao kwa msajili wa vyama kwa miaka yote iloytakiwa isipokuwa inasemekana msajili wa vyama ndiye hakuwakilisha hayo mahesabu kwa CAG kulingana na sheria.

Hivyo Basi ZZK kudai vyama vyote ni lazima vikaguliwe mahesabu yao ina maana tu kwamba alikuwa akiwalenga CCM, CUF na vyama vinginevyo maana CDM tayari walishawakilisha mahesabu yao kwa msajili. Ukweli wa hili, mimi na wewe hatujui ila tu najua hili swala la ukaguzi wa CGA ni moja ya sababu zilofikia kikomo cha watu kumstahimili ZZK. Upande mwingine wa shilingi, miye kama mwanachama wa CDM ambaye nategemea viongozi wangu tupo pamoja ktk vita hii ya UFISADI nilitegemea wangelifurahia hatua hii ya ZZK zaidi kwa kuelewa kwamba hao CCM hawajafanya hivyo na mahesabu yao yatawamaliza kisiasa. Ukaguzi wa mahesabu ndio njia pekee ya kukomesha Ufisadi na ndipo tunapoweza kusema kwa ufasaha wapi fedha inatumika vibaya.

Sasa, iwe ni mawazo binafsi ya ZZK kulingana na jukumu alopewa bungeni, nachoweza kusema tu ni kwamba hakutakiwa kumshitua mtu yeyote ikiwa hoja zake zote zinapitia Bungeni ambako viongozi wetu wote wapo, walimsikia ZZK akisisitiza ukaguzi na hadi kufanikiwa kwake, sisi wana CDM tulitakiwa kushangilia hilo. Hatukumhitaji ZZK wala malaika kutushtua ikiwa sisi ni wasafi.

Swala la Posho ambalo kuna watu wanadai ZZK amelivamia wakati likiwa ni swala la chama. Ajabu ni kwamba hadi leo hatujasikia chama kimefanya maamuzi gani kluhusiana na posho za vikao! Miaka inakwenda, fedha inaliwa na binafsi yangu sioni tofauti baina ya viongozi wanguy na wale wa CCM isipokuwa majukwaani. Ni Dr.Slaa peke yake aloweza kusimama kama ZZK tena yeye alifikia kusema hata mishahara ya wabunge ni mikubwa tuache mbali posho. Leo hii wabunge wetu tulowachagua wanalilia Posho na wengine kudai hawawezi kuishi maisha ya kimaskini kwa sababu tu jirani zao ni maskini...Tena anayasema haya kwa kumkashifu kiongozi wake wazi wazi ktk mitandao wala sii waraka wa siri lakini yuko wapi? ANAPETA na watu wamefurahia kuona ZZK akitukanwa na kwa kutopokea posho ya vikao.


Mkuu wangu sijasema ZZK hana makosa ama matatizo, nadhani umewahi nisoma humu nikizungumzia matatizo ya ZZK lakini ndivyo alivyo ni mbegu ya KGM na asili ya Wabembe inajulikana kuwa ni wabishi na jeuri hasa wanapojua kwamba wanajua zaidi yako. Kibaya zaidi watu kama ZZK wana msemo wa kwamba wao wanawajibika kwa WATANZANIA wote na sio CHAMA.. Hizi ni fikra za Kikomunit ama Madikteta ambao kwa fikra zao hudhani wao tu ndio wanajua wananchi matatizo ya wananchi na jinsi ya kuyaondoa. Kwa kumsoma ZZK ilinilazimu kuandika mada moja humu inayomsihi kujumuika na wenzake kwa kuelewa umuhimu wa UMOJA wa watu ktk utambulisho wa fikra pevu ambazo zinaweza kujadiliwa na kuunganishwa ktk sera ama ilani za chama zna zikatetewa na wengi.

Vyama vimekuwepo kwa sababu maalum, waswahili husema kidole kimoja hakiwezi kuvunja chawa, ama vichwa viwili sii sawa na kimoja. Mkusanyiko wa mawazo tofauti ndipo hoja huzua hoja, zile what IF hutafutiwa plan B lakini mtu mmoja huja na agenda moja tu na mara zote wazungu huziita ambition. Unaweza kutaka kuwa mwenyekiti au rais kwa sababu tu unataka iwe ukomo wa sifa na wadhifa wako hapa duniani nothing elde, Na haiwezekani mtu mmoja ujue mahitaji ya watu millioni 40 na njia zipi zitatosheleza mahitaji hayo isipokuwa kiongozi huongoza tu kama nahodha baada ya kupokea dira, na kipimo chake hufuatia mafanikio yake ktk kukabiri matatizo ya safari sio mashindano ya nani mwenye uwezo wa kufikiri hata kabla safari haijaanza.

ZZK ni mfano mzuri wa rais mstaafu Ben Mkapa, pengine tofauti yao tu ni kwamba ZZK sii FISADI lakini kitabia hasa ktk uongozi nadhani wana vitu wanafanana sana maana Mkapa alikuwa jeuri na akifanya yanayompendeza yeye kulingana na elimu yake ama kichwa chake kinavyomtuma. Tatizo la watu kama hawa huvubja nguvu ya chama na kujenga Ufalme fulani ambao sera na ilani za chama zinakufa.

Na kama unakumbuka wakati wa Mkapa CCM ilikufa kabisa, tena naweza sema binafsi yangu nilidhani Mbowe atachukua Urais hadi siku nilisikia kuwepo kwa mtandano wa Lowassa na Rostam kumweka JK. Lakini je Mkapa alifukuzwa uongozi wa chama au hata kunyang'anywa Uenyekiti na JK?. Na madudu yote ya Mkapa ambaye hadi leo JK anamwekea kifua hata kama hawakubaliani!.. Hii yote ni kutunza heshima sio ya Mkapa nali ya CHAMA. wakianza kutoana ufisadi hatabakia mtu maana usiri uliopo CCM ni Ufisadi tu. Hivyo walimwacha Mkapa hadi muda wake umefikia lakini siye tumeshindwa kusubiri hadi uchaguzi wetu mwaka huu kwa kuhofia ati waraka uloandikwa na watu watatu. Jamani watu kama hawa wanavumilika kwa kutunza heshima ya CHAMA. Hii ndio hekima inayozungumziwa kila siku iwe kwa mabaya ama wazuri.

Katika swala hili, simtetei ZZK wala Kitila isipokuwa napingana na adhabu ilotolewa tena ati wamepewa muda kujieleza zaidi laa sivyo watanyang'anywa hadi uanachama!.. jamani for what?.. waraka huu ama kuna jingine? na kama hilo jingine ni yale ya pandikizi, jamani mbona wapo wengi humo CDM na ndio haswa wanaoeneza habari za uzushi ili mradi tu ifikapo 2015 tumesha vurugika? Hivi kweli mnategemea tutaendela kuwa imara ikiwa hawa mapandiki wataendelea kuwemo CDM kwa hizi tofauti za ZZK na uongozi uliopo? come on gyz, Kuwaondoa madarakani hawa viongozi tena kwa kuwaita WAHAINI!. tusi kubwa sana ni fedheha kubwa sana kwetu sisi tunachokiona ktk waraka huu ni fikra za mageuzi,ni mabadiliko ya uongozi ndani ya chama iwe kwa sababu hizo ama nyinginezo lakini mabadiliko yanatakiwa. Ni makosa makubwa kuwavyua madaraka ZZK na Kitila haswa ktk wakati huu ambao najua fika ni timing za CCM kukibomoa chama. Je, makamba alipoondolewa akaletwa yule Mjita na sasa Kina na tuliambiwa sababu za mabadiliko au walifanya mabaya gani? Kwa nini tunaanika vitu ovyo namna hii kama watoto wadogo ama wahuni ambao ktk ndoa zao hawamwachi mke pasipo kutangaza ubaya wake japo kaishi naye kwa miaka 20!

ZZK hatakuwa ZZK tena, na kwa bahati mbaya hata CDM haitakuwa CDM ile tuloipenda zaidi maana tmeanza kulaumiana. Tunaopinga hatua hii tunaonekana washabiki wa ZZK japo swala hapa ni adhabu ambayo kwa kuutazama waraka ule ZZK hakuhusika kabisa na hata kama angehusika CDM inahitaji mabadiliko ya uongozi. Binafsi yangu sikubaliani kabisa na mfumo wa uongozi ndani ya chama ambapo mtu mmoja ana vyeo 2 au zaidi, uongozi wenyewe hauna muda wa kuachia ngazi, na tati Wabunge wetu ndio hao hao viongozi wa chama na vikao vyote vya chama kitaifa. Hii inawapa nguvu kubwa kupita kiasi na naweza sema ni kama muundo wa serikali tunayoipiga vita leo kutaka katiba mpya. Tukiweza kuwaondolea madaraka viongozi mengine viongozi hawa utaona nguvu ya Udikteta itapungua na kila mmoja wao ataifanya kazi alopewa kwa ufanisi zaidi na hao ndipo tutaweza kuwapima uwezo wao. ZZK ataendela kuwa ZZK lakini hatakuwa yule ZZK tunayempenda na kumchukia ndani ya CDM.

Lakini pamoja na yote haya, mageuzi ni lazima, sipinga kabisa Mbowe kuendelea kuwa Mwenyekiti, na naweza sema sioni mtu zaidi yake kulingana na mazingira ya TZ isipokuwa agombee kazi moja ya Ubunge au Uenyekiti wa chama. Inanisikitisha sana kuona viongozi wangu wakijilimbikiza vyeo ambavyo vinahusiana na malipo zaidi iwe kichama au toka serikali kuu. NI muhimu CDM iwe tofauti na vyama vingine na itaanzia kwa viongozi wetu, asiyependa mashrti haya ajikate mapema na tujue nani hasswa ndiye Mhaini..
 
Mkuu wangu kitu kimoja tu ni kwamba ZZK hakuwa na haja wala sababu ya kuwashtua CDM ikiwa swala la kuwakilisha matumizi ya kila mwaka ni sheria ambayo kila chama kinatakiwa kufanya.

Pili, nijuavyo mimi kutokana na maelezo ya viongozi wa CDM ni kwamba wao tayari walikwisha wakilisha mahesabu yao kwa msajili wa vyama kwa miaka yote iloytakiwa isipokuwa inasemekana msajili wa vyama ndiye hakuwakilisha hayo mahesabu kwa CAG kulingana na sheria.

Hivyo Basi ZZK kudai vyama vyote ni lazima vikaguliwe mahesabu yao ina maana tu kwamba alikuwa akiwalenga CCM, CUF na vyama vinginevyo maana CDM tayari walishawakilisha mahesabu yao kwa msajili. Ukweli wa hili, mimi na wewe hatujui ila tu najua hili swala la ukaguzi wa CGA ni moja ya sababu zilofikia kikomo cha watu kumstahimili ZZK. Upande mwingine wa shilingi, miye kama mwanachama wa CDM ambaye nategemea viongozi wangu tupo pamoja ktk vita hii ya UFISADI nilitegemea wangelifurahia hatua hii ya ZZK zaidi kwa kuelewa kwamba hao CCM hawajafanya hivyo na mahesabu yao yatawamaliza kisiasa. Ukaguzi wa mahesabu ndio njia pekee ya kukomesha Ufisadi na ndipo tunapoweza kusema kwa ufasaha wapi fedha inatumika vibaya.

Sasa, iwe ni mawazo binafsi ya ZZK kulingana na jukumu alopewa bungeni, nachoweza kusema tu ni kwamba hakutakiwa kumshitua mtu yeyote ikiwa hoja zake zote zinapitia Bungeni ambako viongozi wetu wote wapo, walimsikia ZZK akisisitiza ukaguzi na hadi kufanikiwa kwake, sisi wana CDM tulitakiwa kushangilia hilo. Hatukumhitaji ZZK wala malaika kutushtua ikiwa sisi ni wasafi. .

Mkuu najua unampenda sana Zitto kiasi cha kuweza kuwa nje ya control kabisa kuliko zitto abanwe ktk kona.

Well, naona umekubali kupotoka hapa:ZITTO KWA SIFA ALITAKA SEMA CHADEMA WALIMLAUMU KWA KUTOWATONYA ,KWA AKILI YAKE ANAPIGA POINT BIL AKUJUA HASARA KM KAWAID AYAKE KUTOKUWA RESPONSIBLE.KI UKWELI NI KWAMBA HAYO MAMABO ALIAYOKOMAA NAYO KUPITI AKAMATI YA BUNGE KWA CHAMA NDIYE ALIPASWA YAFUATILIA YAFANYWE.YEYE HAKUFANYA KWA VILE HAKAI OFFISINI.NA NDIO MAANA HAKUTEGEMEA KUWA MATOKE O YANGEKUWA TOFUATI.

kwanini sasa atake point kw akitu alichpaswa fanya.Na nyinyi wana CCM mnakuwa wepesi sana kupotezea ??? ili mpate faida.
 
Sinto kujibu kwakuwa wewe kwasasa ni mwanachama wangu na paswa kukushauri maadili ya chama na misingi yake.. Kuwa huru karibu ofisi za mkoa nitakuelekeza mwanachama wangu.

naomba tafsiri halisi ya neno "mwanachama wangu" au wewe kileo ni mwanachama wa nani?
Au wewe ni miongoni mwa watu walio juu ya chama.
 
Waraka wa Dr. Kitila Mkumbo nimeusoma na kuuelewa vizuri na mimi nitaeleza niliyoyaona.

Kwanza Maudhui ya Waraka si mabaya ila ubaya ni njia waliyotumia au wanayotumia ili kufikia malengo yao. Hapa Dr. Kitila Mkumbo anataka kutuaminisha kuwa wameshajaribu njia zote halali za kidemokrasia zimeshindikana sasa wanaanza kutumia njia ambayo ni hatari zaidi!

Flow ya huu waraka ukiusoma unajua kuwa aliyeuandika ni Dr. kitila, lakini kama walikuwa na lengo zuri na nia njema kwa nini wafanye siri? any way, mikakati ya ushindi huwa ni siri lakini kwa nini watumie majina feki ya "MM" M1, M2, M3, na kama nia ni njema kwa nini hadi sasa wamegoma kumtaja M2? hadi kusababisha usumbufu na matumizi yasiyo ya lazima ya kikosi kazi kilichoundwa ili kumbaini M2?

Demokrasia ina mipaka yake, kwanza Demokrasia hiyo hiyo inahitaji Nidhamu kwa waliopo ktk uongozi kwa sasa waheshimiwe, pia inahitaji "Uwazi" sasa kwa waraka huu wa Dr. Kitila amabo ni wa siri je hapa kuna Demokrasia?

Demokrasia inahitaji "Uvumilivu" sasa kama akina Dr. kiltila wameshindwa kuwa wavumilivu kwa viongozi na uongozi uliopo je hii ni demokrasia?

Demokrasia inahitaji "Utiifu" kwa uongozi na viongozi waliopo hata kama hukubaliani nao ktk baadhi ya mambo au huwapendi naturally kuwa mtiifu, na hapa ndo nataka Dr. Kitila mkumbo ajifunze kutoka china, kile chama cha kikomunist cha CPC kimefika hapo kwa sababu viongozi wake ni watiifu kwa uongozi na viongozi waliopo, hata CCM si wote wanampenda kikwete lakini hata kama humpendi au hukubaliani naye ktk baadhi ya mambo mtii tu!! shida ni nini? ipo siku na wewe utapata hiyo nafasi tu!!

Napenda kutofautiana vikali na Dr. mkumbo, yeye kuwa msomi na mchambuzi wa masuala mbali mbali hapa nchini si kigezo cha yeye na kundi lake kutaka kufanya mapinduzi, ajue kuwa anaweza kuwa msomi lakini asiwe kiongozi mzuri! mbona Kikwete ana degree moja lakini aliwashinda Akina prof. Mwandosya? Dr. Salimu A. Salim na wengine?

Hivi mwakani, Mbowe akiacha kugombea Uenyekiti, akagombea Lisu au mwingine na Zitto na Zitto akashindwa ktk huo uchaguzi hivi watasemaje tena??

Vile vile: Naomba Chadema wafanyie kazi yale yote ya kweli yaliyomo ndani ya waraka wa Dr. Kitila Mkumbo.

 
kaka kabwe huaminiki tena siku hizi. kwa wenye akili tumeona wazi wewe umejipambanua kuwa unatumika kwa ajili ya kuidhoofisha chadema. pamoja na kwamba unakuja na porojo, lkn muonekano wako wa matendo ni kwamba unatumiwa na ccm kuhujumu chadema. hata kama utaamua kuendelea kuwa mwanachama wa chadema lkn ukweli ni kwamba wewe si mwenzetu tena. unafiki unakusumbua, ni bora uende huko ccm unakowatumikia hiv sasa.
 
'Vurugu' zote hizi za akina Zitto, Mkumbo, Mwigamba, na wengineo ni mpango maalum wa CCM unaoitwa Operation Chaos...!!!

Soma hapa uone jinsi gani mpango wenyewe na malengo yake.

Hii ni nukuu toka ukurasa wa facebook ya W.J. Malecela (Le Mutuz), kada wa CCM, na mratibu wa mpango huo...

@ LE MUTUZ STRAIGHT TALK!!:
Leo kuna habari njema sana kwetu CCM, kwamba Mwenyekiti wa Chadema ameamua kujitoa kugombea Urais 2015, so I told you OUR OPERATION CHAOS is working kwani our never ending online attacks zimemfanya ajipime, ok now one more to go, next on line ni Dr. Slaa, naye ni lazima ajitoe kugombea ili our best interest Zitto ndiye awe mgombea wao 2015!

- NILIWAAMBIENI HAWA HAWANA MGOMBEA URAIS 2015, SO SASA WALE WOTE TUNAOSHIRIKIANA KUWADHOOFISHA KWA KUTUMIA MITANDAO TUZIDISHE MASHAMBULIZI KAMA ILIVYO SASA, NINALO BOMU MOJA LA KIONGOZI WAO MMOJA MAARUFU KUTAKA KUMBAKA DEMU MMOJA MAJUU NA KESI IPO MAHAKAMANI NA DOCUMENTS ZIPO, INA MAANA HUYU AKIPEWA KUGOMBEA CHADEMA AKAPATA URAIS HATARUHUSIWA KWENDA HIYO NCHI, SASA TUTAKUWAJE NA RAIS AMBAYE NI LIMITED KWENYE INTERNATINIONAL COMMUNITY? SAAFI SANA MHESHIMIWA MBOWE KWA KUJIPIMA NA KUACHIA NGAZI SASA MSHAURI NA MWENZAKO SLAA AJIPIME!!

KIDUMU CCM!

KIDUMU CHAMA TAWALA!!

HA! HA! HA! HA!

- LE MUTUZ!!
 
watu wanataka kuwa viongozi wa maisha wengine nao wanataka kuongoza hapo ni patashika nguo kuchanika.
 
watu wanataka kuwa viongozi wa maisha wengine nao wanataka kuongoza hapo ni patashika nguo kuchanika.

Uongozi Chadema unapatikana kupitia uchaguzi, sio 'waraka' wa akina Mkumbo.
Maskini Zitto, bado siku 9 tu atakua historia..!! Atakua 'out of the political picture'...!!
Wana-CCM wa JF itabidi watafute 'shujaa' wao mwingine wa kumpigia debe...!!
Wapi Team Zitto...??? Wapi Ritz...??? Wapi 'mrembo' Mamndenyi...???
 
Last edited by a moderator:
Sinto kujibu kwakuwa wewe kwasasa ni mwanachama wangu na paswa kukushauri maadili ya chama na misingi yake.. Kuwa huru karibu ofisi za mkoa nitakuelekeza mwanachama wangu.

ulimbukeni huuu unatumiwa na mbowe wewe,sasa mbona unahitaji kuja ofisini kwako?MBONA WARAKA ULIUMWAGa humu jamvini?KUMBUKENI CDM IKIWA NA MALENGO YA KITAIFA TUTASHINDA NA KAMA MNAPOKEA MALENGO KUTOKA TENGERU KWA MZEE MTEI NA MNATAKA KUIFANYA SACCOSS MTAKUFA KIBUDU
MHAFIDHINA WA SIASA WEWE!!siasa za mjomba fulani ,mwagia watu tindikali!!
 
Wanajamvi, Salaam za kuelekea mwisho wa mwaka 2013.

Nimekuwa msomaji tu tokea sakata la kuvuliwa majukumu ya Unaibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Mh. Zitto Zuberi Kabwe. Na hata pale alipoamua kuitisha mkutano na waandishi wa Habari kutoka aliyoyatoa.

Leo nimeamua kujiuliza juu ya kauli tofauti za Mheshimiwa huyu kijana mbona huwa zina utata na nyingine hazina mwisho wa matukio yake?

Kati ya kauli hizi ni kama zifuatazo:-

  1. Ndugu zangu wanakigoma hii itakuwa mara yangu ya mwisho kugombea ubunge katika jimbo hili kwani Geita wanataka niwe mbunge wao.
  2. Ndugu wananchi msimwamini mwanasiasa yeyote.
  3. Ninapigwa mishale na watu wengi nje na ndani ya chama changu.
  4. Nitagombea Urais mwaka 2015 kupitia CHADEMA.
  5. Ninaacha siasa kwani nataka kutafuta chuo cha kufundisha.
  6. Nimeamua kutoacha siasa kutokana na hali mbaya ya maisha ya wananchi.
  7. Waliodhani leo nitachua maamuzi magumu wamejidanganya.
  8. Hakuna chama kilichokaguliwa mahesabu na CAG pia makatibu wa vyama wanatakiwa kutoa taarifa za fedha kwa PAC.
  9. Vyama vyote vimekaguliwa mahesabu yao.
  10. CC ya CHADEMA walitaka niwatonye kabla ya kutoa tamko la wito wa mahesabu.
  11. Viongozi wa CHADEMA msinichagulie marafiki.
  12. Nitataja majina ya watu walioweka fedha Uswiss.
  13. N.K.......

Hizi kauli zote amekuwa anazitoa katika mikutano mbali mbali, Twitter au Facebook na ukizifuatilia utaona hakua hata moja imefika au itafika mwisho wa utekelezaji wake.

MY TAKE:

ZZK huwa anatafuta nini hasa katika kauli zake hizi?
 
Mbowe na chadema wanapaswa kuturidhisha juu ya
yaliyoandikwa kama madhaifu yake kwenye Mkakati wa mabadiliko 2013 ndani ya
taasisi...... atolee ufafanuzi hata kama
itamgharimu..

anapaswa atoe ufafanuzi wa dhaifu moja baada ya jingine ili kutudhihirishia umma kwamba waraka ule ni wa uchochezi na uhaini.
 
Wanajamvi, Salaam za kuelekea mwisho wa mwaka 2013.

Nimekuwa msomaji tu tokea sakata la kuvuliwa majukumu ya Unaibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Mh. Zitto Zuberi Kabwe. Na hata pale alipoamua kuitisha mkutano na waandishi wa Habari kutoka aliyoyatoa.

Leo nimeamua kujiuliza juu ya kauli tofauti za Mheshimiwa huyu kijana mbona huwa zina utata na nyingine hazina mwisho wa matukio yake?

Kati ya kauli hizi ni kama zifuatazo:-

  1. Ndugu zangu wanakigoma hii itakuwa mara yangu ya mwisho kugombea ubunge katika jimbo hili kwani Geita wanataka niwe mbunge wao.
  2. Ndugu wananchi msimwamini mwanasiasa yeyote.
  3. Ninapigwa mishale na watu wengi nje na ndani ya chama changu.
  4. Nitagombea Urais mwaka 2015 kupitia CHADEMA.
  5. Ninaacha siasa kwani nataka kutafuta chuo cha kufundisha.
  6. Nimeamua kutoacha siasa kutokana na hali mbaya ya maisha ya wananchi.
  7. Waliodhani leo nitachua maamuzi magumu wamejidanganya.
  8. Hakuna chama kilichokaguliwa mahesabu na CAG pia makatibu wa vyama wanatakiwa kutoa taarifa za fedha kwa PAC.
  9. Vyama vyote vimekaguliwa mahesabu yao.
  10. CC ya CHADEMA walitaka niwatonye kabla ya kutoa tamko la wito wa mahesabu.
  11. Viongozi wa CHADEMA msinichagulie marafiki.
  12. Nitataja majina ya watu walioweka fedha Uswiss.
  13. N.K.......

Hizi kauli zote amekuwa anazitoa katika mikutano mbali mbali, Twitter au Facebook na ukizifuatilia utaona hakua hata moja imefika au itafika mwisho wa utekelezaji wake.

MY TAKE:

ZZK huwa anatafuta nini hasa katika kauli zake hizi?

Pinda ni mzigo kwa taifa.
 
mkuu hongera kwa kuweka post yako ili kujua yale yanayokutatiza ni kweli uongozi wa chadema wanapaswa kujibu wapi waraka ule umeonesha uhaini kama siyo ni uoga wa demokrasia kwa viongozi wa chadema.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom