Taarifa za Zitto na Dr. Kitila kwa Umma Juu ya Kuvuliwa Nafasi za Uongozi ndani ya CHADEMA

Status
Not open for further replies.
Mwacheni Zitto,ni watanzania wangapi wanalala njaa?wamama wangapi wanalala wawili wawili mawording?Kila siku maralia inaua maelfu.CHADEMA hamna akili waoneni CCM sasa hivi wameamua kudeal from bottom kila siku wako vijijini huko wakijenga chama,nyie mmekalia Zittto Zitto,non sense
Aisee! Napita tu, hayo nayo maneno!
 
Kwenye tamko alilotoa Zitto Kabwe jumapili, moja ya mambo aliyoyasema yeye mwenyewe ni kuwa anatuhumiwa na Kamati Kuu ya CHADEMA kwa kupokea rushwa kutoka kwa matajiri wakubwa wa CCM -- Nimrod Mkono na Mohamed Dewji -- kwenye uchaguzi wa 2010 ili awashawishi wagombea wa CHADEMA wajitoe na majatiri hao wapite bila kupingwa. HII NI HATARI!

Maneno ya Zitto mwenyewe haya hapa:

"Tuhuma kwamba nilishiriki kuwashawishi wagombea wetu katika baadhi ya majimbo kujitoa katika uchaguzi wa mwaka 2010 ili kuwapisha wagombea wa CCM wapite bila kupingwa kwa njia ya rushwa. Majimbo yanayotajwa ni pamoja na Sumbawanga, Musoma Vijijini (NIMROD MKONO) na Singida Mjini (MOHAMED DEWJI). Kama nilivyokwisha kueleza katika vikao mbalimbali vya chama jambo hili si la kweli na hakuna popote ambapo watoa tuhuma hizi wamewahi kutoa ushahidi kwamba nilifanya jambo hili. Nipo tayari kwa uchunguzi ndani ya chama na watoa tuhuma waje na ushahidi bayana wa jambo hili. Si afya kwa chama kuendelea kurudiarudia tuhuma hizi kila mara tangu mwaka 2010 bila uchunguzi wowote kufanyika na jambo hili lifikie mwisho."

Video ya Zitto mwenyewe akiongea kuhusu hizi tuhuma hii hapa:
http://www.youtube.com/watch?feature=player_embedded&v=fLl3ibzU0b0
 
Mi kinachonishangaza kwa hawa Zito na Mwenzie Kitila wanazungumzia demokrasia ipi! kufanya mapinduzi ya siri? Hivi Demokrasia msingi wake ni mkakati wa siri? kama hayo madai yao ndo demokrasia kwanini wasingeweka wazi ili kila mtu aujue mkakati wao wanao amini ni wa kuijenga Demokrasia ndani ya chama! lkn pia wote wako kwenye vikao vya maamuzi vipi wameshindwaje kusema hicho wanachokiona ndo tatizo la CDM? usiri huu wanini wakati sasa unasema kila kitu tuendeshe kwa uwazi! Zito nae bila kujitambua anasema angeuona huo mkakati angeutekeleza maramoja ni mjinga tu anaeweza kukataa kwamba zito anahusika na njama haramu za kufanya mapinduzi haramu. Tena ktk waraka wao wanakiri kabisa kwamba mpinzani wao ni mzuri zaidi na namna pekee ya kumshinda ni kupandikiza viongozi ili waweze kushinda coz wanajua kama hata ingekuwa leo uchaguzi ukaitishwa Zito hawezi kumshinda Mbowe. kitu kingine cha kijinga watu wanataka Mbowe asigombee sababu za msingi hakuna zaidi ya uzushi na majungu na tamaa ya kutaka madaraka ya kuiangamiza CDM.
....Sababu kuu ni kumpiga mchungaji ili kondoo watawanyike. Hivi ubora wa Zitto dhidi ya Mbowe ni nini?
 
pamoja mkuu

  1. wanacdm walikuwa wanamheshimu sana dr.mkumbo.ni msomi wa wa ngazi ya uzamivu.kukiri kwake kutayarisha waraka ule sasa watu wanamwona kama choo.wanajiuliza maswali mengi bila majibu.hata dr mkumbo amekuwa mchumia tumbo????amejidhalilisha sana.amekidhalilisha chuo anachokifanyia kazi.amewadhalilisha sana watu singida anakotoka.kweli mrina asali ni mrina asali tu.ametudhalilisha sana wasomi wa ngazi ya uzamivu.ndio maana elimu imekufa hapa nchini kwa sababu ya watu kama hawa.nasikia anawafundisha waalimu.waraka ule angeandika dr bana tusingeshangaa.dr mkumbo.?????cdm wamchunguze sana anaweza akawa ni litiss.!!!!!chadema ni chama makini jamani.sera zake ni za kizalendo.wanasema wataweka uchumi mikononi mwa watanzania!!!mtanzania yoyote popote alipo anakipiga vita anapingana na sera hii.atataka uchumi umilikiwe na wageni.atataka tuendelee kuwatumikia wageni tu??ndivyo dr kitila mkumbo anavyotaka.ndivyo zitto anavyotaka.wamebadilika ghafla na kuanza kutuhujumu.nchi nzima wanacdm wanawalaani.badala ya kukijenga chama wanapanga mipango ya kutuondolea makamanda wetu!!!!!!!!!!!mungu atawalaani tu.
 
Wewe ndo unageuzwa Mbuzi siyo Wabongo! Unaonekana una uelewa mdogo sana katika mambo ya siasa! ZZK ana upeo na falsafa ya hali ya juu sana na kusudi umwelewe ni lazima u read between the lines. Ndo maana yule kiongozi wenu DJ wa ....Hotels anamshindwa, hapa ni suala la falsafa siyo ubabe!!!

Umewasikia wale wafuasi wake kule Kigoma kaskazini?, eti " kama Zitto akihamia popote wataenda naye, Akienda Chelsea, watamfuata, akienda Real Madrid watamfuata" Sasa kama haongozi mazuzu ni kitu gani? Nawe ni zuzu mojapo!!
 
Kumbe ZItto na DR Mkumbo wana busrara kiasi hiki,kuanzia leo nakuwa pro Zitto,hayuko kama nilivyofikiri,ametumia busra ya hali ya juu yeye na mwenzake,watu walitegemea angeanza kutoa kashfa na siri za chama kwa hasira na jazba lakini imekuwa kinyume,nadhani ana nia nzuri tu na chama.
Kwa upande wangu naona Dr. Kitila katumia busara na hekima kubwa sana, naweza kusema ni kweli ana mapenzi ya dhati na CHADEMA, kwa upande wa Zitto, swa katumia busara kutokishambulia chama lkn nona bado anaegemea upande wake zaidi. Bado ninamaswali mengi sana kichwani.
 
DANCING%20BLACK%20CAT.gif


When a Black Cat Crosses the Road..........
 
Zitto yuko kwenye panic syndrome, ameacha aliyoshutumiwa na chama chake kwenye kikao cha sasa anaongea yale aliyoyatekeleza mika mitatu nyuma si anaonyesha trend ya usaliti wake chadema komaeni naye huyu sasa na iwe mwisho nilidhani alisema CC nusu ni wake na nusu ni mbowe mbona kwenye press conference alikuwa na msaliti mwenzake peke yake
 
hawa kamati kuu wamechemsha zitto siyo wa kuhongwa wanalao jambo.

Wewe wenyewe CC wanajua anahongwa kaa hapa ukatae mpaka kesho ndio kang'olewa hakuna vyeo anavyotambia eti niliwaomba si mulinipa wenyewe leo anavililia ha ha
 
Namalizia, kwa waliosoma lugha na saikolojia pale chamani wanaweza kutambua mengi katika speech ya jana mfano; kwanini hajatumia lugha POLITE wakati kiukweli ana hatia?kwanini katengeneza debate badala ya kuwa submissive?n.k
Jibu langu ni bado anaaminishwa CDM hawawezi kumtimua kabisa,anahisi akifukuzwa CCM watambeba na hapa anakosea

Nashauri mipasho ya jana iongeze effect kwenye siku 14 ili yatimie ..zaidi ya hapo uoga utakigharimu chama kuanzia chaguzi za ndani,mitaa mpaka mkuu ..Afukuzwe Completely
Ni kweli kuna arrogance fulani.
 
Nawashukuru Zito na Mkumbo kwa angalau kuonyesha some loyalty kwa chama chao. Kwa hili kidogo wameonyesha wanaweza 'kusikilizika'. Hii ni pale walipouhakikishia Umma wa Tanzania kuwa hawatakuwa wa kwanza kujiondoa CDM. Hata hivyo, nikianza na Zito nipende kumshangaa kama kweli yeye ni mwanasiasa mkomavu sasa iweje aitishe press conference na kuanza kujibu ambacho 'hajatuhumiwa nacho'? Ingetosha sana kuiambia hadhara ya watanzania kuwa kilichosababisha nisimamishwe sicho kilichotolewa hadharani. Baada ya hapo ukaisubiri barua ya kujieleza ndipo kama kweli unayo nia ya kujibizana ukarudi na kututhibitishia kwa ushahidi wa umeandikiwa nini ujieleze. Iwapo barua ya tuhuma zako ikiwa ni sawa sawa na alichotueleza Tundu utatuambia nini tena ambao hatukuwa kwenye kikao cheni cha CC? Na iwapo tuhuma zikija zaidi ya 'ulizojibu' utakuja na nyimbo gani tena?
Dakta huyu naye kanishangaza sana. Dokta mzima unakiri.....yaani kweli ulishiriki katika ujinga huu? Kwamba 'mpinzani wenu' aharibu chama mkitazama tu ili baadae 'mnayemtaka' awe mwenyekiti? Hii ni bila hata kuona hatari ya kutengeneza ushindi kwa wapinzani wa chama chenu. huyu ni daktari kabisa! Busara pekee uliyoionyesha angalau ni kuomba radhi lakini sympathy ya wenye kufikiri huwezi kuipata. Utetezi eti hata Barack Obama alitengenezewa mkakati na kupata urais! Hii ndo justification? Obama akiuza ikulu na sisi tuuze! Usomi wetu unanipunguzia sifa kama huku ndiko kufikiri kwa wasomi wetu. Mkumbo, hata kama kweli unampenda kiasi hicho rafiki yako aongoze CDM huwezi kutumia mambo yaleyale yanayodaiwa kutumiwa na JK na wana mtandao wenzie kumwingiza madarakani. Huoni/husikii ambavyo hadi leo CCM inahangaika na hii mitandao?
Ingalikuwa ni mimi ningetulia pasina kuanza malumbano na kutafuta namna ya kurejesha tumaini jipya kwangu toka kwa wanachama wenzangu. Kwa sasa mlilolifanya ni sawa na kuwahimiza CDM wawafukuze kundini. Aliyewadanganya kuwa mnakubalika sana huku uraiani, pasipo kumung'unya maneno ANAWADANGANYA!
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom