Taarifa za Utendaji wa Viongozi wa Bunge la Tanzania (MPYA Tanzania) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Taarifa za Utendaji wa Viongozi wa Bunge la Tanzania (MPYA Tanzania)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Fred Katulanda, Jul 10, 2012.

 1. Fred Katulanda

  Fred Katulanda Verified User

  #1
  Jul 10, 2012
  Joined: Apr 1, 2011
  Messages: 229
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Ndugu salaam,
  Naomba kuwafahamisha nyote kuwa siku ya Ijumaa tarehe 13 Julai 2012 kuanzia saa 4:00 asubuhi (10.00 Hrs EAT) Taasisi ya Raia ya Haki za Kisiasa na Mwenendo wa Bunge (The Civil and Political Rights Watch) itatoa taarifa juu ya tathmini ya Uongozi wa Bunge kwa mwaka 2011. Tathmini hii inaangalia utendaji na ufanisi wa viongozi wa Bunge, Spika, Naibu wa Spika na Wenyeviti wa Vikao vya Bunge. Tathmini hii imetumia dhana na zana za mfumo wa Uwajibikaji kwa Jamii (Social Accountability Monitoring) kama unavyotumiwa Afrika Kusini kupima vigezo vitano vya kuongoza vikao (Usikivu kwa wajumbe; Kuzingatia kanuni; kuzingatia hoja; Kukwepa Ushabiki; na Upendeleo kwa wajumbe).

  Hii ni tathmini ya kwanza kabisa kufanyika Tanzania na kuwa itatumika kama nguzo ya kupima muelekeo wa utendaji na ufanisi wa viongozi wetu wa Bunge kwa miaka ijayo.

  Waandishi habari wote mnakaribishwa (tafadhali wasiliana nasi at marcossy@yahoo.com kwa maelezo zaidi).
  Taarifa itatolewa kwenye ofisi za taasisi kwenye anuani hapo chini:

  Imetolewa na;
  Albanie Marcossy
  Mkurugenzi Mtendaji,
  Civil and Political Rights Watch
  Plot 522 Block E - Sinza Palestina (Off Shekilango Road)
  P.O Box 522 Dar es salaam
   
 2. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #2
  Jul 10, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  Duh sijui kama kunatakayepata tano ya Mia
   
 3. R

  RC. JF-Expert Member

  #3
  Jul 10, 2012
  Joined: May 24, 2012
  Messages: 446
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  asante kwa taarifa mkuu!!!!!!!!
   
 4. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #4
  Jul 10, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Nina mashaka, jack zoka atakuja kuiona kwanza hiyo riport na mambo yataharibikia hapo!!!!

  Hatakubali bibi kiroboto apate tano ya mia wakati amewasaidia sana kuzuia huduma za afya kwa watanzania zisijadiliwe bungeni kwa kisingizio cha mahakama.
   
 5. T

  Tanganyika2 Member

  #5
  Jul 11, 2012
  Joined: Oct 25, 2011
  Messages: 70
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jack Zoka, Nyoka Mkuu.... Hussein Ramadhani Mwagilo
   
 6. T

  Tanganyika2 Member

  #6
  Jul 14, 2012
  Joined: Oct 25, 2011
  Messages: 70
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tathmini ya Ubora wa Viongozi wa Bunge 2011:

  1. NDUGAI, JOB YUSTINO;
  Amejitahidi sana kukwepa upendeleo wa kisiasa na kuilindaserikali; haoneshi utashi wake kumiliki mamlaka aliyopewa na Kanuni za Bungeanapoongoza vikao.
  USIKIVU KWA WABUNGE 2.500
  UZINGATIAJI KANUNI 2.625
  UPENDELEO WA KISIASA 2.5625
  UZINGATIAJI HOJA 2.375
  USHABIKI BUNGENI 3
  JUMLA KIWANGO 13.0625
  WASTANI 2.6125 (DARAJA LA TATU)

  2 SIMBACHAWENE,GEORGE BONIFACE
  Msikivu kwa Wabunge haswa wenye HOJA zenye maslahi kwaTaifa; Amejitahidi sana kukwepa upendeleo wa kisiasa na kuilinda serikali;Anayumbishwa na makundi au siasa.
  USIKIVU KWA WABUNGE 2.125
  UZINGATIAJI KANUNI 2.3125
  UPENDELEO WA KISIASA 3.28125
  UZINGATIAJI HOJA 2.09375
  USHABIKI BUNGENI 3.4375
  JUMLA KIWANGO 13.25
  WASTANI 2.65 (DARAJA LA TATU)

  3 MAKINDA,ANNE SEMAMBA ;
  Imara kwenye kanuni na kuzingatia hoja; Anayumbishwa naushabiki kisiasa; si msikivu kwa wabunge.
  USIKIVU KWA WABUNGE 3.03125
  UZINGATIAJI KANUNI 2.65625
  UPENDELEO WA KISIASA 3.46875
  UZINGATIAJI HOJA 2.75
  USHABIKI BUNGENI 2.9375
  JUMLA KIWANGO 14.84375
  WASTANI 2.96875(DARAJA LA TATU)

  4. MHAGAMA, JENISTERJOAKIM; Anajitahidi sana kuzingatia kanuni; Anayumbishwa na makundi kisiasa; simsikivu kwa wabunge.
  USIKIVU KWA WABUNGE 3.21875
  UZINGATIAJI KANUNI 3.15625
  UPENDELEO WA KISIASA 3.5
  UZINGATIAJI HOJA 3.53125
  USHABIKI BUNGENI 3.3125
  JUMLA KIWANGO 16.71875
  WASTANI 3.34375(DARAJA LA TATU)

  5 MABUMBA,SILVESTER MASELE ;
  Haoneshi ushabiki wa wazi wa kisiasa; hushindwa kuhimilimivuto ya makundi na upendeleo wa kisiasa; Si msikivu kwa wabunge.
  USIKIVU KWA WABUNGE 4.25
  UZINGATIAJI KANUNI 4.25
  UPENDELEO WA KISIASA 3.78125
  UZINGATIAJI HOJA 3.90625
  USHABIKI BUNGENI 3.25
  JUMLA KIWANGO 19.4375
  WASTANI 3.8875 (DARAJA LA NNE)


  ANGALIZO LA VIWANGO:
  1.00 – 1.49 = Uongozi Mzuri Sana,
  1.50 – 2.49 = Uongozi Mzuri
  2.50 – 3.49 = Uongozi wa Wastani
  3.50 – 4.49 = Uongozi Dhaifu
  4.50 – 5.0 = Uongozi Dhaifu Sana

  Taarifa imetolewa leo kwa waandishi habari na wanaharakatiwaliohudhuria (inapatikana kwenye mabadiriko forum).
   
 7. BHULULU

  BHULULU JF-Expert Member

  #7
  Jul 14, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 4,911
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Wote dhaifu tu
   
 8. kanga

  kanga JF-Expert Member

  #8
  Jul 14, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 1,011
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  mko sahihi hasa kwa mabumba very foolish.
   
 9. m

  magohe JF-Expert Member

  #9
  Jul 14, 2012
  Joined: May 21, 2011
  Messages: 729
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  tena sana mkuu!!!akili ndogo kuongoza akili kubwa.je watz watafika kwa hali hii?
   
Loading...