Taarifa za Tanzania: Nani tumsikilize? Naona kila mmoja siku hizi ni mtoa habari kwa watanzania!!

tramadol

JF-Expert Member
Oct 10, 2015
5,383
4,317
Kila siku Tanzania imekuwa nchi ya matamko toka pande zote za nchi na maajabu unakuta suala moja lakini linatolewa taarifa tofauti tofauti na watu tofauti tofauti wa ndani ya Serikali na nje ya Serikali.

Matokeo yako huku mitaani, sehemu za kazi,majumbani na hata vijiweni kumekuwa na mijadala ambayo hata sababu huioni.

Kwani taarifa za nchi hii zinatolewa na nani au kila mmoja unaweza kuitisha press comference na kutoa taarifa maana naona kila iitwayo leo watoa taarifa mnatuchanganya tu.

Sasa tumuamini nani jamani?
 
Wakati wanakujibu hilo,na mimi wanijibu hili. Ni kwa nini taarifa inatolewa tena kwa lugha ya kiswahili halafu baada ya moto kuwashwa na wananchi, taarifa inakuja kutolewa ufafanuzi kwa ile ile ya kiswahili?
 
Wahusika watakujibu
 
Wewe siku hizi ukiwa na neno ita watu hata chini ya mti na waandishi toa Taarifa zako uzijuazo watasilikiza itabaki wenye alikili ya kuchambua hayo ulosema
 
Kila siku Tanzania imekuwa nchi ya matamko toka pande zote za nchi na maajabu unakuta suala moja lakini linatolewa taarifa tofauti tofauti na watu tofauti tofauti wa ndani ya Serikali na nje ya Serikali.

Matokeo yako huku mitaani, sehemu za kazi,majumbani na hata vijiweni kumekuwa na mijadala ambayo hata sababu huioni.

Kwani taarifa za nchi hii zinatolewa na nani au kila mmoja unaweza kuitisha press comference na kutoa taarifa maana naona kila iitwayo leo watoa taarifa mnatuchanganya tu.

Sasa tumuamini nani jamani?
Tolea mfano, huko mtaani mmechanganywa na taarifa gani?

Au ni zile za kutoka “Noah”, “balimi saba hadi kufikia tatu”, na sasa naskia ni juisi ya Azam embe ya jero mia.

Kama hiyo lazima uwe confused!
 
Dunia ya sasa imefikia mahali ambapo ni lazima sana utumie ubongo wako.

Wewe unataka upate habari zinazofanana kutoka vyanzo tofauti kama enzi za uhuru na mzalendo.

Changanya na zako, dunia ya kibepari haina kubaby sit! Kama huelewi unaachwa nyuma. Na kwasababu hiyo, unajikuta unachukuwa maamuzi mabovu kwa taarifa hizo mbovu.

Enzi za ujamaa mlitafuniwa na kumezewa. It’s now a “wild wild world” where only the fittest shall survive!
 
Makusanyo ya kodi ni billio 600 taarifa ya Zitto au trillion 1.2 taarifa ya TRA
 
Kwahiyo wewe ulitaka Zitto na TRA wakae pamoja ili waje na taarifa moja “sahihi”?

Au hujasoma my previous posts. Zipitie na hizo pia uzijibu. Zimebeba baadhi ya majibu ya maswali yako.
 
Kila siku Tanzania imekuwa nchi ya matamko toka pande zote za nchi na maajabu unakuta suala moja lakini linatolewa taarifa tofauti tofauti na watu tofauti tofauti wa ndani ya Serikali na nje ya Serikali.

Matokeo yako huku mitaani, sehemu za kazi,majumbani na hata vijiweni kumekuwa na mijadala ambayo hata sababu huioni.

Kwani taarifa za nchi hii zinatolewa na nani au kila mmoja unaweza kuitisha press comference na kutoa taarifa maana naona kila iitwayo leo watoa taarifa mnatuchanganya tu.

Sasa tumuamini nani jamani?
Wasemaji ni wawili tu Dr Abbas na ndugu Polepole, yule Jerry Muro anajipendekeza tu!!
 
Kwahiyo wewe ulitaka Zitto na TRA wakae pamoja ili waje na taarifa moja “sahihi”?

Au hujasoma my previous posts. Zipitie na hizo pia uzijibu. Zimebeba baadhi ya majibu ya maswali yako.
Zitto na TRA hawawezi kukaa meza moja kuandaa taarifa kwa umma ila wananchi tunahitaji taarifa sahihi
 
Katika zama hizi za teknolojia ya habari na mawasiliano,vyanzo vya habari ni vingi.Usahihi wa habari unategemea uwezo wako wakuchambua mambo,au imani yako kwa chanzo cha habari.Kwa mfano kuna watu habari ikitoka serikalini/ccm hiyo ndio taarifa sahihi,wengine taarifa ikitoka Chadema/upinzani kwao ndio taarifa sahihi.Lakini wengine huwezi kuwaambia kitu Kwa Mange Kimambi.
 
Back
Top Bottom