Mikael Aweda
JF-Expert Member
- Dec 17, 2010
- 2,973
- 3,901
Kuna mtu anayeitwa Ngwechele (sijui kama spelling ni sawa) wa Mwanza aliyejiita mkiti wa matawi ya Chadema Mwanza ambaye taarifa zake zimeteka ukurasa wa Mbele wa magazeti ya Rai, Jambo Leo, Uhuru na Majira siku ya Leo. Huyu ni mtu ambaye hajulikani kabisa lakini ameteka vichwa vya magazeti hayo kuliko hata mbunge mwenye jina. Ukweli ni kwamba, kwa muda wa karibu miaka 10 nikiwa kiongozi wa chadema sijawahi kusikia hata siku moja cheo cha m/kiti wa matawi ya chadema mahali po pote. Kiufupi hakuna kitu kama hicho. Huu ni usanii wa kulazimisha chanzo cha habari cha magazeti tajwa kwa maslahi yao. Maswali ya kujiuliza.Je, kwa nini magazeti yenye mlengo wa kiccm yaandike habari hii ya Chadema kwa kiasi hiki tena kwa kulazimisha chanzo (source) ambayo haipo kwa mujibu wa katiba ya Chadema??Pili, Je, magazeti haya lenye mlengo wa kiccm kuendelea kuandika habari hii kwa nguvu zote inatupa picha gani kwa mwanachadema anayetumia akili yake kufikiri??Nikisema hii ni ishara ni ukweli wa kuumia kwa ccm nitakosea au ndo ninazidi kuweka ukweli uliojificha hadharani!Je,Kitendo cha hawa wenye malengo yao kushindwa kupata m/kiti halali wa chadema wa kijiji/mtaa, kata au wilaya au mkoa wa kutoa kauli hiyo na badala yake wakaibua chanzo feki na kukipa cheo kikubwa ambacho hakipo ndani katiba ya chadema, siyo ishara ya umoja kwa wanachadema wote katika sakata hili?? Nihitimishe kwa kusema kuwa malalamiko ya makada wa ccm kama Nape, Mwigulu na wengineo, press ya zitto kuandaliwa na uvccm na kitendo cha magazeti yanayomilikiwa na wanaccm kushupalia jambo hili kiasi cha kutumia chanzo feki na kuiweka ukurasa wa mbele kunafichua ukweli moja tu. Ukweli huo ni kuwa ccm imeumizwa sana na uamuzi huu. Binafsi sijajua kwa nini wasishangilie kama ni uamuzi wa kuiumiza chadema. Akili za kuambiwa nachanganya na zangu.