Taarifa za Ngwechele wa Mwanza imezidi kufichua ukweli wa sakata la Zitto Vs Kamati kuu CHADEMA

Mikael Aweda

JF-Expert Member
Dec 17, 2010
2,973
3,901
Kuna mtu anayeitwa Ngwechele (sijui kama spelling ni sawa) wa Mwanza aliyejiita mkiti wa matawi ya Chadema Mwanza ambaye taarifa zake zimeteka ukurasa wa Mbele wa magazeti ya Rai, Jambo Leo, Uhuru na Majira siku ya Leo. Huyu ni mtu ambaye hajulikani kabisa lakini ameteka vichwa vya magazeti hayo kuliko hata mbunge mwenye jina. Ukweli ni kwamba, kwa muda wa karibu miaka 10 nikiwa kiongozi wa chadema sijawahi kusikia hata siku moja cheo cha m/kiti wa matawi ya chadema mahali po pote. Kiufupi hakuna kitu kama hicho. Huu ni usanii wa kulazimisha chanzo cha habari cha magazeti tajwa kwa maslahi yao. Maswali ya kujiuliza.Je, kwa nini magazeti yenye mlengo wa kiccm yaandike habari hii ya Chadema kwa kiasi hiki tena kwa kulazimisha chanzo (source) ambayo haipo kwa mujibu wa katiba ya Chadema??Pili, Je, magazeti haya lenye mlengo wa kiccm kuendelea kuandika habari hii kwa nguvu zote inatupa picha gani kwa mwanachadema anayetumia akili yake kufikiri??Nikisema hii ni ishara ni ukweli wa kuumia kwa ccm nitakosea au ndo ninazidi kuweka ukweli uliojificha hadharani!Je,Kitendo cha hawa wenye malengo yao kushindwa kupata m/kiti halali wa chadema wa kijiji/mtaa, kata au wilaya au mkoa wa kutoa kauli hiyo na badala yake wakaibua chanzo feki na kukipa cheo kikubwa ambacho hakipo ndani katiba ya chadema, siyo ishara ya umoja kwa wanachadema wote katika sakata hili?? Nihitimishe kwa kusema kuwa malalamiko ya makada wa ccm kama Nape, Mwigulu na wengineo, press ya zitto kuandaliwa na uvccm na kitendo cha magazeti yanayomilikiwa na wanaccm kushupalia jambo hili kiasi cha kutumia chanzo feki na kuiweka ukurasa wa mbele kunafichua ukweli moja tu. Ukweli huo ni kuwa ccm imeumizwa sana na uamuzi huu. Binafsi sijajua kwa nini wasishangilie kama ni uamuzi wa kuiumiza chadema. Akili za kuambiwa nachanganya na zangu.
 
Zitto ni jiwe lililowashinda washi. Kaskazini yote makamanda mmeungana kumshambulia kwa chuki zenu za kikanda, kidini na kikabila. Ila huwa siku zote haki ya mtu haipotei hata ikiwa mission atashindwa kuikamilisha wapo kina Zito wengine watazaliwa na watapigania kuisimamisha haki na kuondoa dhulma chadema mnayofanya. Ni ishu ya muda tu.
 
Zitto ni jiwe lililowashinda washi. Kaskazini yote makamanda mmeungana kumshambulia kwa chuki zenu za kikanda, kidini na kikabila. Ila huwa siku zote haki ya mtu haipotei hata ikiwa mission atashindwa kuikamilisha wapo kina Zito wengine watazaliwa na watapigania kuisimamisha haki na kuondoa dhulma chadema mnayofanya. Ni ishu ya muda tu.

Acha kupayuka kwenye keyboard
 
Mwananchi nalo lina malengo ya ki-CCM? Mliopo anza ubaguzi mlitegemea nini? Media imeshawashtukia, single zenu haziuzi.

Yule Jamaa, kasema wazi viongozi wao ni vibaraka na makuwadi wa CHADDEMA KASKAZ ndio maana wameaamua kuanzisha umoja wa matawi!
 
Masikini zitto ndio kwanza anaonekana na upande wake wa pili kwamba mtu mwenye akili timamu hawezi shindwa ku-connect dots na kujua huyu jamaa alikuwa kibaraka wao!!Tumefukuza nyoka ndani mwetu ajabu ni kwamba majirani wametahayari wanatetea yuda!!!
Wake up bro wanakutumia kama ndomu baadae watakutupa kwa aibu kubwa!!
 
mda mwingine si kila atachosema mpinzani hakutakii jema!!ZZK ni mtu wa watu
 
Bado yatakuja mengi sana....kinachotakiwa wahusika kuwa wavumilivu tu
 
Zitto ni jiwe lililowashinda washi. Kaskazini yote makamanda mmeungana kumshambulia kwa chuki zenu za kikanda, kidini na kikabila. Ila huwa siku zote haki ya mtu haipotei hata ikiwa mission atashindwa kuikamilisha wapo kina Zito wengine watazaliwa na watapigania kuisimamisha haki na kuondoa dhulma chadema mnayofanya. Ni ishu ya muda tu.
humeonaheee!
 
Kwanza kitendo cha Zitto na Kitilla kuwakosa makamanda wa CHADEMA siku aliyofanya press conference na kuwakodi uvccm, na kitendo cha matamko yanayotolewa na wanaojibambikia vyeo ambavyo havipo chadema ni kufilisika kisera kwa Zitto Kabwe na CCM aliyokuwa anakiwakilisha kukihujumu CHADEMA.
 
sijawahi kuona aweda aanzishe mada yenye akili. huwa anatabiri tabiri tu vitu vya kijinga
 
Vichwa vya TZ Daima vipi ? Be specific na usiongee kama mtu mpumba-vu ! Mwenzako ametaja magazeti specific na habari specific, sasa kama wewe una habari iliyopo kwenye TZ Daima ambayo ni ya uongo au uzushi si uitaje ?

Kumbe upo??

Vichwa vya TZ Daima mbona husemi!!! mkuki kwa nguruwe...
 
[h=5]KATIKA RIPOTI YOTE YA MATAWI YA MWANZA KIPENGELE HIKI CHA HITIMISHO NI HATARI SANA NANUKUU:-

"Hitimisho: Tunataka maamuzi haya HARAMU yaliyofanywa na kamati kuu yabatilishwe na mchakato wa kuwavua viongozi hawa nyazifa zao ufuate taratibu na kanuni kwa mujibu wa katiba.

Tofauti na hapo tarehe 4/12/2013 tutaungana na wapigania Demokrasia kote nchini kufanya maandamano yasiyokuwa na ukomo mpaka uongozi uliopo utoke madarakani.
Baada ya tarehe hiyo tunataka mhakikishe mnawahamisha wabunge vibaraka wote wa chadema mkoa wa mwanza.

Mchukueni Wenje mkamtafutie jimbo Moshi na Highness Kiwia mkamtafutie jimbo HAI na MACHAME.Hii ardhi ya kanda ya ziwa sio saizi yao na tunataka waondoke mara moja. Kinyume na hapo tutawaondoa huku wakishuhudia kwa macho yao.

Pia tunamuagiza Mbowe na Slaa wasithubutu kukanyaga ardhi hii ya kanda ya ziwa ikiwa bado hawajajiuzulu ama kubadili maamuzi yao HARAMU haraka iwezekanavyo. Hatuna sababu ya kuendelea kuwa watumwa wa fikra ndani ya chama chetu."



[/h]
 
Back
Top Bottom