Taarifa za Msiba Italia

X-PASTER

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
11,610
1,809
pama.JPG
Marehemu Mohamed Abddul Shakur a.k.a Captain PAMA

Watanzania Italy wanasikitika kutangaza kifo cha Ndugu MOHAMED ABDUL SHAKUR (PAMA) kilichotokea 5th Jan asubuhi katika hospitali ya SAN GIOVANNI DI DIO E RUGGI D'ARAGONA" SALERNO.

Mwili wa marehemu utaondoka Rome siku ya jumanne tarehe 13/1/2009 kupitia Amsterdam kwa ndege ya shirika la KLM, na unatarajiwa kuwasili nyumbani Dar kwa mazishi siku ya jumatano 14/01/2009 saa 22:40. na ndege ya shirika la KLM namba 569.

Mwenyekiti wa jumuiya ya Watanzania Italy, kwa niaba ya uongozi na watanzania wote Italy, anatoa salam za rambirambi kwa wazazi na ndugu wa marehemu nyumbani na popote walipo, zimepokewa taarifa hizi kwa masikitiko makubwa na waunaungana na wafiwa katika wakati huu mgumu wa maombolezo.

Mungu ailaze roho yake mahala pema.
Amin.

Watanzania Italy

Picha na Habari zaidi Fungua Hapa Watanzania Italy
 
Asante sana, mkuu X-Paster kwa taarifa hii.

Mungu Aiweke roho ya marehemu mahali pema.

Huyu marehemu, kaka yake (Nuru), na wengine wengi, walikuwa ni jamaa wa mitaa ya kwetu kule Ngamiani, TA.

Kifo chake kimenihuzunisha sana!
 
Poleni wafiwa.....
Ngamiani mitaa gani hiyo mkuu...unagusia maeneo yenyewe hayo...

Ukaderwazee, mkuu!

Mitaa ya Miti Ulaya, brbr inayopita idara ya maji, Central Bakery, hadi njia panda ya kuelekea Bombo Hosp., Mkonge, Yatch Club, .... Kulichangamka sana wakati ule kabla ya viwanda vya mbolea, chuma, na bandari kufa.
 
Utasema miti ulaya bila ya kujua mskiti wa ijumaa mkuu....kwa Prakash jee? Vipi pale kwa Hamisi Mzee? Dah ndo kwenyewe huko...Najaribu kucollect kumbukumbu ni huyu huyu mkuu aliyekuwa akija mitaa ya Chumbageni anahang out na akina Majisu??
 
R.I.P PAMA. Poleni wafiwa wote. Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe. Amen.
 
Kwanza poleni sana wafiwa...

Mkuu X-PASTER, huyu marehemu alishakuwa mtangazaji wa Sauti ya America (VoA) pia? naomba unikumbushe hilo tafadhali?

RIP (MOHAMED ABDUL SHAKUR)
 
Utasema miti ulaya bila ya kujua mskiti wa ijumaa mkuu....kwa Prakash jee? Vipi pale kwa Hamisi Mzee? Dah ndo kwenyewe huko...Najaribu kucollect kumbukumbu ni huyu huyu mkuu aliyekuwa akija mitaa ya Chumbageni anahang out na akina Majisu??

Daah! Mkuu ulikuwa unaishi Msambweni, nadhani!

Sijui unamzungumzia Majisu gani? Labda ni yule aliyekuwa footballer, aliyekuwa akiishi karibu na Usagara Sec.! Huyu jamaa alikuwa ktk mob ya akina Mhina Guni (marehemu), Kocho, Yakub (Tengema). Nakumbuka alishawahi kushiriki ktk boxing tournament fulani.
 
Kwanza poleni sana wafiwa...

Mkuu X-PASTER, huyu marehemu alishakuwa mtangazaji wa Sauti ya America (VoA) pia? naomba unikumbushe hilo tafadhali?

RIP (MOHAMED ABDUL SHAKUR)

Mkuu, Baba Enock, huyu jamaa hajawahi kufanya kazi ya utangazaji, na sidhani km alishawahi kufika US.
 
poleni sana wafiwa, kwa wale wa kinondoni maeneo ya mkwajuni watamkumbuka sana bwana PAMA
 
Daah! Mkuu ulikuwa unaishi Msambweni, nadhani!

Sijui unamzungumzia Majisu gani? Labda ni yule aliyekuwa footballer, aliyekuwa akiishi karibu na Usagara Sec.! Huyu jamaa alikuwa ktk mob ya akina Mhina Guni (marehemu), Kocho, Yakub (Tengema). Nakumbuka alishawahi kushiriki ktk boxing tournament fulani.

Mkuu No! Ila msambweni makaburini pale kwenye miembe shule ya msingi nimeshakipiga cha ndimu sana tu, ndie haswa Majisu aliwahi kuishi karibu na Usagara Sec. pia alikuwa na ndugu mitaa ya Chumbageni, alishawahi kuichezea Coastal Union wagosi wa kaya halafu akawa baharia...Nina imani nilisikia amefariki na yeye....
 
Back
Top Bottom