Taarifa za Msiba: Babu yangu amefariki akiwa na miaka 95

technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
11,975
48,841
Alizaliwa mwaka 1921 huko mjini Musoma.

Ajaugua alilala vizuri tu Jana akiwa anacheka na watu waliokuwa naye karibu lakini kuamuka asubuhi amefariki.

Alikuwa mwanajeshi mstaafu

Mazishi yatafanyika nyumbani kwake Musoma .

Ameacha watoto 19 na wake wawili .

Wajukuu 56 na vitukuu 122.

Nipo ndani ya majonzi makubwa babu yangu ndiye alisababisha mafanikio yangu mpaka hapa nilipo kwa ushauri wake na kwa namna moja hama nyingine.

Nasikitika kutangaza kifo...
 
Aisee amekufa kifo cha amani sana, ni wachache sana wenye kupata bahati kama hiyo, hapo hakuna masikitiko wala msiba bali ni sherehe ya babu kupumzika kwa amani, RIP babu yetu
 
Wote mauti yangetufikia hivyo. Mwache apumzike salama. R.I.P babu. Mkamfanyie sherehe huyo!!
 
Kwa umri huo hajafa huyo ameenda kupumzika! Amemaliza safari yake Salama!!!!
 
Apumzike kwa amani babu yetu....kwa umri huo wala usilie mshukuru Mungu kumuweka miaka yote hiyo maana ni baraka kubwa,mwaka jana pia nilifiwa na babu yangu alifariki akiwa na miaka 115 wakati wa kusomwa historia yake ilipotajwa umri ndugu wote walishangilia na vigelegele vikapigwa, hakuna mtu aliyelia.
 
Hongereni sana Mkuu kwa kuwa na karama ya kuwatunza wazee.....Si sehemu zote za Tanzania wazee wanaishi kwa amani.

Jitahidi kuishi kama Babu yako ili nawe uache Legacy ya kukumbukwa kama ya Babu yako.
 
Alizaliwa mwaka 1921 huko mjini Musoma.

Ajaugua alilala vizuri tu Jana akiwa anacheka na watu waliokuwa naye karibu lakini kuamuka asubuhi amefariki.

Alikuwa mwanajeshi mstaafu

Mazishi yatafanyika nyumbani kwake Musoma .

Ameacha watoto 19 na wake wawili .

Wajukuu 56 na vitukuu 122.

Nipo ndani ya majonzi makubwa babu yangu ndiye alisababisha mafanikio yangu mpaka hapa nilipo kwa ushauri wake na kwa namna moja hama nyingine.

Nasikitika kutangaza kifo...
Babuska rest in eternal peace
 
Back
Top Bottom