drphone
JF-Expert Member
- Sep 29, 2009
- 3,542
- 281
Unaweza kutusaidia kufuatilia na kutupa uhakika?
DC
wakuu nimefwatilia na nimeambiwa itaanza kufanya kazi next week na waliniambia riba zao zipo chini kulinganisha na mabenki mengine nawakilisha
Unaweza kutusaidia kufuatilia na kutupa uhakika?
DC
mkuu, nilisikia muda kidogo kwamba wangeingia bongo, branch zao zipo wapi?
nimeweza ku confirm location zao, Equity bank kwa dar wapo quality centre (pugu road) na nyingine posta wapo PSPF plaza karibu na ppf. Ni bank nzuri sana kwa mikopo ya wafanyabiashara wadogo na wakulima, niliongea muda mrefu sana na wafanyakazi wao na kweli niliwakubali.
Target yao ni watu wa kipato cha chini hata kama una biashara ya maandazi watakuthamini
Asanteni kwa michango mizuri na ushauri wa wapi pa kupata mikopo ya biashara. Naamini itasaidia kwa wale ambao tunafikiria kuongeza mitaji kwenye biashara tulizokwisha kuanzisha na zile tunazofikiria kuanzisha.
Ushauri wangu tu ni kuwa ikiwezekana mtu afanye biashara zaidi ya moja kwani kuna kupanda na kushuka na ukiwa na biashara zaidi ya moja anagalau zitasaidiana.
Swali dogo tu lililoko nje ya mada, hivi tuna benki au taasisi zinazotowa mikopo ya kujenga nyumba Tanzania kwa kiwango cha mil 100 mpaka mil 150
nimeweza ku confirm location zao, Equity bank kwa dar wapo quality centre (pugu road) na nyingine posta wapo PSPF plaza karibu na ppf. Ni bank nzuri sana kwa mikopo ya wafanyabiashara wadogo na wakulima, niliongea muda mrefu sana na wafanyakazi wao na kweli niliwakubali.
Target yao ni watu wa kipato cha chini hata kama una biashara ya maandazi watakuthamini
Namshauri kama kweli anatafuta mkopo wa kujenga nyumba awatembelee Azania bank, wanao huo mpangoAhsante sana ndugu kwa maoni na ushauri wako. Naamini wadau wataufanyia kazi!!
Kuhusu mikopo ya nyumba...ni kweli kuna benki zinatoa ila sina details. Nitajaribu kulifanyia kazi.
DC
Msisahau na 10% za maafisa mikopo otherwise utafuatilia huo mkopo hadi soli za viatu ziishe
Dark City!
Hakika upo makini ktk ukombozi wa Mtanzania yeyote yule mwenye kutaka kujikwamua katika hatua moja kwenda kwingine!
Mi nafikiri ni wakati mwingine tena wa MwanaJF yeyote aliye kama Mi binafsi kutafakari kwa makini THREAD hii na kurudi upya kwa namna ajuavyo kwa Dark City!
Hongera sana na hakika uko MAKINI!
Pamoja Daima DC!
kaka mimi nilichikua kamkopo kangu AccessBank hakika hawana masharti mengi na wanatoa mikopo kuanzia laki 1, na kwa muda mfupu kabisa! mi nadhani ni wakati wa kwenda kuwatembelea hawa jamaa wako vizuri kwa wajasiriamali tofauti na mabenki ambayo umeyataja hapo juu,. Kwa sasa NMB si ya makabwela tena ndo mana wanaitwa NMB PLc kwa sasa.
Asante sana kwa kutuletea hii topic, binafsi nimeelimika sana. Nina swali, iwapo mimi mfanyakazi nimechukua mkopo bank na nimepangiwa au kuchagua kulipa laki saba kwa mwezi. sasa ktk kuutumia mkopo wangu kwenye biashara nimeacha kazi na kusimamia biashara. Je inawezekana bank ikakubali kupunguza kiwango cha kurudisha kwa mwezi ili nimudu kulipa bila kuathiri biashara yangu? Mkopo ni wa kujengea nyumba.
Ok DC nashukuru sana kwa hili, kifupi nilichukua muda na collateral ilikuwa ni mshahara, sasa juzi wamekuja kutambia habari ya top up, ila ningependa deni lao liishe mapema na niwe free kutoingia ktk ajira.
Tuliwauliza kuhusu hilo na wamejibu kuwa wanatuongezea hata muda wa marejesho usogezwe mbele ikiwa tunachukua top up. Kutokana na jibu lako nashukuru sana nadhani ni bora nisichukue kabisa na ni bora niendelee na Saccos ambayo nimeishaanza kuweka taratibu. Interest zao pia ni kubwa mno. Asante sana