Taarifa za mapato Kituo cha Mabasi Ubungo zifanyiwe kazi

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,462
21,334
kwa hii serikali ya kichwa cha mwendawazimu sijui...la hasha ndio kwanza wamewapa machinga complex...wasubiri kuchunguza tena....Taarifa za mapato Kituo cha Mabasi Ubungo zifanyiwe kazi






http://habarileo.co.tz/kitaifa/?n=282
TAARIFA ya kwamba Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam sasa inapata zaidi ya shilingi milioni 3 kwa siku kama makusanyo kutoka Kituo cha Mabasi yaendayo Mikoani cha Ubungo (UBT), ni taarifa yenye kuleta udadisi mwingi kwa kila mwanajiji.

Kiasi hicho cha fedha kinaonyesha tofauti kubwa na shilingi milioni moja kwa siku iliyokuwa ikielezwa na Kampuni ya Smart Holdings kabla ya mkataba wake kumalizika hivi karibuni.

Taarifa hiyo njema kutoka kwa Halmashauri ya Jiji inatoa nafasi kadhaa za mawazo yenye hoja kali za kutaka kujua nini hasa kilikuwa kinafanyika katika kituo hicho. Kwanini kuna mabadiliko makubwa ya mapato?

Ingawa maelezo hayo ya 'ghafla' ya mapato yamepatikana katika Baraza la Madiwani, hakuna shaka ni maelezo sahihi yanayoashiria kuwapo kwa ufisadi mkubwa uliokuwa unafanyika katika kituo hicho.

Kwa mantiki hiyo, sisi tunaungana na kauli ya Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji, Ahmed Mwilima kuwa ongezeko hilo, linaonesha kulikuwepo na mizengwe katika taarifa zilizokuwa zikitolewa awali juu ya mradi huo.

Kwa namna nyingine ya pekee ushahidi huo wa mapato unatoa ukinzani kwa taarifa za awali kwamba mradi huo ulikuwa ukikusanya mapato kidogo; na sasa inastahili tafakari ili kujua ni kiasi gani Jiji limepoteza katika mradi huo wakati Smart Holdings ndio waliokuwa wakikusanya fedha.

Ni vyema hilo likajulikana ili wahusika waweze kuchukuliwa hatua za kisheria za kwanza, kutoa taarifa za uwongo na kutumia kwa hila fedha za makusanyo ambazo zingelisaidia sekta nyingine katika Jiji.

Pamoja na kutambua ukweli huo, Jiji sasa nalo lina wakati mzuri wa kuangalia aina hii ya 'wizi' ambayo ni lazima kuizuia kabla mtu mwingine hajakabidhiwa kazi ya kuendesha kituo hicho.

Shauri zima la kutokuwapo ukweli katika makusanyo ya Ubungo kwa kuangalia mapato yaliyodhibitiwa na Jiji kunafanya kuwapo kwa haja ya umakini katika shughuli za zabuni na ukaguzi.

Kama hapakuwapo na kipengele cha ukaguzi na mtu akionekana ameshindwa kushtakiwa, kipengele hicho lazima kiwapo kwani hatuwezi kuwa na watu wanaodanganya umma kwa manufaa yao binafsi.

Ni matumaini yetu na wakazi wa Jiji suala hili la Kituo cha Mabasi Ubungo litafanyiwa kazi ili ijulikane mapema kwamba huwezi kuchezea fedha za umma na kuachwa bila kuadabishwa.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom