Taarifa za Ben Saa Nane kuonekana, Jeshi la Polisi lizifanyie kazi Taarifa za Kubenea

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Taarifa za Mhe. Kubenea kwamba Ben yupo mtaani anarandaranda na kujificha kwa rafiki zake, ni taarifa zinazopaswa kufanyiwa kazi na Jeshi la Polisi na uongozi wa Chadema. Takribani mwezi mmoja sasa polisi na Uongozi wa Chadema umetoa taarifa rasmi za kumtafuta Ben. Leo Kubenea anasema Ben yupo mtaani, anaonekana kwenye vijiwe vya kahawa.

Ni vizuri Polisi wakamkamata Kubenea aeleze ni mitaa ipi Ben alionekana, na ni vijiwe vipi vya kahawa alivyokutwa. Je alikua na nani? ni siku gani? aliyemuona ni nani? na kwanini alipomuona hakutoa taarifa polisi? Na kwa kuwa Kubenea anajua polisi wanamtafuta kwanini alipojua Ben yupo mtaani hakwenda kuripoti polisi ili awasaidie ktk kufanya uchunguzi? Kwanini Kubenea anawaacha Polisi watumie rasilimali kubwa kumtafuta Ben wakati anajua Ben amejificha ili kujipatia umaarufu wa kisiasa?

Kubenea anasema Ben anatafuta umaarufu, je ni umaarufu gani wa kujipoteza? Ili iweje? Kwa faida ya nani? Kwamba Ben akijipoteza ndo anakua maarufu? Halafu huo umaarufu unamsaidiaje? Kugombea nafasi ya uongozi kwenye chama? Ni nafasi gani ambayo mtu huchaguliwa kwa kujipoteza? Na ni akina nani watakua wajinga wa kumpa mtu kura kwa sababu tu alijipoteza? Hivi kujipoteza kwa Ben kunamuongezea kura au kunampunguzia?

Kama kweli Ben yupo mtaani, je Kubenea haoni kuweka taarifa gazetini ni kumfanya azidi kujificha? Kwanini asingewaarifu polisi kwanza wamkamate then ndo aweke gazetini? Na hao marafiki zake Ben waliomficha huko mtaani ni mahiri wa ujasusi kiasi gani? Je wamewazidi akili polisi, usalama wa taifa na intelijensia ya Chadema? Je Kubenea kuandika habari bila kujibu maswali muhimu (5Ws +H) haoni kunaifanya habari hiyo kukosa uhalali wa kuaminika mbele ya jamii?

Na kwa kuwa Mwenyekiti wa Chadema Mhe.Freeman Mbowe alitamka hadharani kuwa kuna uwezekano Ben ametekwa, je Kubenea kusema Ben kajificha haoni anamfanya Mbowe kuonekana ameshiriki kumficha Ben? Kwa kuwa Kubenea ameshindwa kutaja vyanzo vyake vya habari haoni habari hiyo inaweza kuonekana ni ya kutunga maana haina credible source? Je ikija kubainika kuwa Ben ametekwa au amekufa, je Kubenea haoni kwamba atakua amewakosea sana watanzania, kuikosea familia ya Ben, na hata nafsi yake mwenyewe?

Sisemi kuwa Ben hawezi jificha, as a human being anaweza kufanya hivyo na ikibainika kajificha nashauri achukuliwe hatua kali za kisheria. Lakini ukweli ni kuwa habari ya Kubenea imeacha maswali mengi kuliko majibu.

Nahofia Kubenea asije kuwa ameandika habari hiyo kwa chuki binafsi dhidi ya Ben halafu baadae akaja kujuta. Nafahamu ugomvi binafsi kati ya Ben na Kubenea uliosababishwa na tofauti za kisiasa. Kuna mengi yalitokea ambayo siwezi kuyasema yote hapa lakini Ben na Kubenea wamewahi kunyukana kwa nyakati tofauti kwa sababu mbalimbali (ushahidi wa maandishi yao wakinyukana upo).

Sasa isije kuwa Kubenea anaendeleza mnyukano kati yake na Ben akasahau suala la uhai wa mtu ni muhimu kuliko tofauti zao za kisiasa. Ikibainika Ben amejificha Kubenea atakua shujaa kwenye hili, lakini ikija kubainika kuwa Ben amekufa, kuuawa au kutekwa, dhamiri ya Kubenea itamhukumu maisha yake yote. Ni vizuri kuwa na akiba ya maneno.!

[HASHTAG]#BringBackBenAlive[/HASHTAG].!

Malisa GJ
 
Ni mahari gani Kubenea kanukuliwa juu ya taarifa hizi?? naona zinasambaa sana pasipo kuonesha Kubenea aliandika au kusema wapi juu ya hii inshu
 
Hiyo ilikuwa fake news kwa tunaojua kuziangalia fake nyuzi watajua tu

Anaonekana na marafiki zake wasio na majina,
Anaonekana sehemu isiyojulikana ni wapi ,Anaonekana muda gani hakuna
Kumbuka hiyo ni investigative news lazima iwe na ushahidi wa hayo niliyataja hapo.
 
Taarifa za Mhe.Kubenea kwamba Ben yupo mtaani anarandaranda na kujificha kwa rafiki zake, ni taarifa zinazopaswa kufanyiwa kazi na Jeshi la Polisi na uongozi wa Chadema. Takribani mwezi mmoja sasa polisi na Uongozi wa Chadema umetoa taarifa rasmi za kumtafuta Ben. Leo Kubenea anasema Ben yupo mtaani, anaonekana kwenye vijiwe vya kahawa.

Ni vizuri Polisi wakamkamata Kubenea aeleze ni mitaa ipi Ben alionekana, na ni vijiwe vipi vya kahawa alivyokutwa. Je alikua na nani? ni siku gani? aliyemuona ni nani? na kwanini alipomuona hakutoa taarifa polisi? Na kwa kuwa Kubenea anajua polisi wanamtafuta kwanini alipojua Ben yupo mtaani hakwenda kuripoti polisi ili awasaidie ktk kufanya uchunguzi? Kwanini Kubenea anawaacha Polisi watumie rasilimali kubwa kumtafuta Ben wakati anajua Ben amejificha ili kujipatia umaarufu wa kisiasa?

Kubenea anasema Ben anatafuta umaarufu, je ni umaarufu gani wa kujipoteza? Ili iweje? Kwa faida ya nani? Kwamba Ben akijipoteza ndo anakua maarufu? Halafu huo umaarufu unamsaidiaje? Kugombea nafasi ya uongozi kwenye chama? Ni nafasi gani ambayo mtu huchaguliwa kwa kujipoteza? Na ni akina nani watakua wajinga wa kumpa mtu kura kwa sababu tu alijipoteza? Hivi kujipoteza kwa Ben kunamuongezea kura au kunampunguzia?

Kama kweli Ben yupo mtaani, je Kubenea haoni kuweka taarifa gazetini ni kumfanya azidi kujificha? Kwanini asingewaarifu polisi kwanza wamkamate then ndo aweke gazetini? Na hao marafiki zake Ben waliomficha huko mtaani ni mahiri wa ujasusi kiasi gani? Je wamewazidi akili polisi, usalama wa taifa na intelijensia ya Chadema? Je Kubenea kuandika habari bila kujibu maswali muhimu (5Ws +H) haoni kunaifanya habari hiyo kukosa uhalali wa kuaminika mbele ya jamii?

Na kwa kuwa Mwenyekiti wa Chadema Mhe.Freeman Mbowe alitamka hadharani kuwa kuna uwezekano Ben ametekwa, je Kubenea kusema Ben kajificha haoni anamfanya Mbowe kuonekana ameshiriki kumficha Ben? Kwa kuwa Kubenea ameshindwa kutaja vyanzo vyake vya habari haoni habari hiyo inaweza kuonekana ni ya kutunga maana haina credible source? Je ikija kubainika kuwa Ben ametekwa au amekufa, je Kubenea haoni kwamba atakua amewakosea sana watanzania, kuikosea familia ya Ben, na hata nafsi yake mwenyewe?

Sisemi kuwa Ben hawezi jificha, as a human being anaweza kufanya hivyo na ikibainika kajificha nashauri achukuliwe hatua kali za kisheria. Lakini ukweli ni kuwa habari ya Kubenea imeacha maswali mengi kuliko majibu.

Nahofia Kubenea asije kuwa ameandika habari hiyo kwa chuki binafsi dhidi ya Ben halafu baadae akaja kujuta. Nafahamu ugomvi binafsi kati ya Ben na Kubenea uliosababishwa na tofauti za kisiasa. Kuna mengi yalitokea ambayo siwezi kuyasema yote hapa lakini Ben na Kubenea wamewahi kunyukana kwa nyakati tofauti kwa sababu mbalimbali (ushahidi wa maandishi yao wakinyukana upo).

Sasa isije kuwa Kubenea anaendeleza mnyukano kati yake na Ben akasahau suala la uhai wa mtu ni muhimu kuliko tofauti zao za kisiasa. Ikibainika Ben amejificha Kubenea atakua shujaa kwenye hili, lakini ikija kubainika kuwa Ben amekufa, kuuawa au kutekwa, dhamiri ya Kubenea itamhukumu maisha yake yote. Ni vizuri kuwa na akiba ya maneno.!

[HASHTAG]#BringBackBenAlive[/HASHTAG].!

Malisa GJ

Mkuu Mwanahabari Huru

Kubenea ni huyu Mbunge wa Ubungo, Mh Saed Kubenea ambaye ni mwanachama wa ngazi za juu wa CHADEMA?

Ama anayetajwa humu ni Kubenea mwingine?
 
Mkuu, ni huyo huyo ambaye aliwahi kuzua kuwa Masheikh wanafanyiwa unyqnyasaji kwa kuingizwa vitu sehemu za haja kubwa. Ni huyo huyo aliyesema kuwa wabunge wanawake wa UKAWA wamevuliwa shanga na chupi
 
wakat mnachangia mkumbuke pia kubenea ana ugomvi binafsi na ben... na historia inaonyesha kubenea ni mzur sn kuwachafua maadui zake kupitia vyombo vyake vya habari.
 
Mimi nilijua hili jambo litawageuka Cdm na washirika wao ukiangalia hata jinsi gani chama kilitumia mwendo wa kinyonga kulishughulika,

utagundua tu ndani yake kuilikuwa na sarakasi za kisiasa na kutafuta umaarufu kuliko uhalisia.
Kama kubenea kaandika hayo inawezekana yuko sahihi.

Ikibainika kuwa ni kweli alijipoteza ili kuipaka matope serikali

Achukuliwe hatua yeye na washirika wake wote walioihusisha serikali na kupotea kwake ili liwe fundisho hata kwa wengine.
 
Back
Top Bottom