TAARIFA: YAH:Kuvunjika RASMI kwa ndoa kati ya Ruttashobolwa na Madame B

Baba V

JF-Expert Member
Dec 29, 2010
19,487
2,000
Wapendwa wana chit chat ni dhahiri kwamba wote tumekuwa mashuhuda wa kilichokuwa kikiendelea katika iliyokuwa ndoa ya loya Ruttashobolwa na Madame B huku kwa upande mwingine ikimuhusisha Chimbuvu. Kama ilivyo lengo kuu la tume ya Mahusiano na Ndoa hapa chit chat ni kuhakikisha kuwa members wanaendelea vizuri na kufurahia mahusiano yao, tume ilijitahidi kufanya jitihada za kutatua mgogoro ili ndoa iendelee kudumu lakini sote tumeshuhudia Madame B kushindwa kutoa ushirikiano.

Nawashukuru wadau wa kamati mbalimbali na members kwa ujumla ambao walifanya jitihada za kuikoa ndoa hiyo.
Napenda kuchukua nafasi hii kuwatangazia wana chit chat kuwa baada ya jitihada za muda mrefu kuokoa uhusiano wake na Madame B ,Ndugu Ruttashobolwa ameniletea taarifa za kumpa talaka RASMI Madame B leo hii tar.01/12/2012 (siku ya kujitafakari TUKO WANGAPI).
Nikiwa kama mwenyekiti wa tume ya kuratibu mahusiano na ndoa, natangaza rasmi kuwa Madame B sio mke wa Ruttashobolwa tena.
Aidha ni vema nikawasilisha MASIKITIKO yangu juu ya kitendo cha ndugu Chimbuvu kuanzisha uzi kwa lengo la kunivunjia heshima na kwa kunituhumu kuwa namtaka Madame B huku akijua kuwa ni uzushi na kafanya hivyo kwa makusudi kabisa.ningependa kumshauri kuwa siku nyingine awe makini kabla hajafanya jambo.
Aidha ninapenda kutoa WITO kwa wana chit chat wote kufuata taratibu zilizowekwa kama tulivyokubaliana.
cc. KAMATI YA SCREENING
cc.KAMATI YA SHERIA
cc.KAMATI YA MAADILI
cc Madame B


Wenu Baba V
MWENYEKITI WA TUME YA KURATIBU MAHUSIANO CHIT CHAT 2012
 
Last edited by a moderator:

Inside10

JF-Expert Member
May 20, 2011
24,402
2,000
Chit-chat bwana..
Kila kukicha watu walewale, thread zilezile zenye manufaa yaleyale/upuuzi uleule
 

Chimbuvu

JF-Expert Member
Jul 17, 2012
4,404
2,000
Kwenda kwa:mwenyekiti mahusiano Baba V
kk:sreening committee
yah:masikitiko makubwa

Kwa masikitiko makubwa nimepokea taarifa kutoka kwa mwenyekiti kuhusu uhusiano wa Ruttashobolwa kuvunjika rasmi,nikiwa kama mwanachitchat nimesikitishwa na tukio hilo.
Napenda kumpa pole ndugu Ruttashobolwa kwa yote yaliyomkuta,pia kama wanachitchat tuchukulie hili tukio sio kwa upande mmoja bali iwe kama fundisho kwa wote kwa kuangalia makosa yaliyotendeka nasi katika mahusiano yetu na ndoa zetu hapa chitchat ziweze kudumu na zisirudie makosa na chitchat iwe sehemu nzuri ya kifamilia na kulea watoto vizuri kama @C6, charminglady na mtoto wao pekee tedo, Baba V na mama V na mtoto wao Chilli.
Asanteni sana.
Chimbuvu & Madame B
 
Last edited by a moderator:

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom