Taarifa ya ziara ya kutembelea na kutoa semina kwa wanafunzi wa darasa la saba katika shule ya msingi kata ya Kandete.

BEDECCA

Member
Oct 27, 2016
10
4
BEDECCA- IN TANZANIA.

Busokelo Education Development for Child and Counseling Association in Tanzania.

Katika semina hii iliyofanyika kuanzia tarehe 22/08/2017 hadi tarehe 24/08/2017 tumeweza kuelimisha na kuhamasisha wanafunzi wa shule za msingi zote katika kata ya Kandete ambazo ni Ipelo, Kisalala, Kandete, Lugombo,Bujingijila na Ndala, idadi ya wanafunzi walionufaika na semina hii ni mia tatu sitini na moja (361) tu.

Uongozi wa ”Bedecca in Tanzania” unashukuru sana kwa kuwa katika shule zote uongozi wa shule husika umepata ushirikiano mzuri, wanafunzi husika wamepokea elimu hii kwa furaha kubwa na kuahidikuwa watayatendea kazi pindi watakapo fika kidato cha kwanza mwakani (2018).

Yafutayo ni baadhi ya mafunzo ya elimu waliyokuwa wameipata wanafunzi wa darasa la saba katika shule sita za msingi:-

Elimu ni nini?

Ø Ni tendo au uzoefu wenye athari ya kujenga akili, tabia ama uwezo wa kimaumbile wa mtu binafsi.

Ø Katika dhana ya kiufundi elimu ni njia ambayo hutumiwa kimakusudi na jamii kupitisha maarifa, ujuzi na maadili kutoka kizazi kimoja hadi kingine.

Ø Elimu ndiyo pambo tukufu na lenye thamani kuliko mapambo yote anayojipamba nayo mwanadamu.

Ø Elimu ndio mwangaza na taa pekee inayomwangazia mwanadamu katika maisha ya ulimwengu huu.

Ø Elimu ndio chombo pekee anachoweza kutumia mwanadamu kujua halali na haramu baina ya lenye kudhuru na lenye kunufaisha.

Pia elimu ndio chombo chenye kuzisafisha na kuzitakasa nafsi za wanadamu
Ø kuzirekebisha tabia zao mbaya na kuwaongoza katika njia njema na yenye maadili.

SABABU ZINAZOPELEKEA WANAFUNZI KUACHA SHULE:

a) Mimba za utotoni.

b) Ajira za utotoni.

c) Watoto kutopewa mahitaji muhimu kama vile sare za shule, vifaa vya shule nk.

d) Mzazi mmoja kuwa na kauli ya mwisho katika familia.

e) Kutokuwa na ushirikiano bora baina ya wazazi/walezi, waalimu na wanafunzi.

f) Mazingira duni anakotoka mwanafunzi,

g) Baadhi ya wazazi/walezi kulazimisha watoto wa kike kuolewa ingali bado nia wadogo.

MADHARA YA KUTOA MIMBA KWA WANAFUNZI:-

Hii ni hali ya mwanamke kwa hiari yake mwenyewe kuharibu mimba iliyoingia ndani ya kizazi chake.

i. Uwezekano mkubwa wa kufa.

ii. Kutokea kwa ugumba kwa mwanamke.

iii. Mimba kutunga nje ya kizazi.

iv. Kujifungua watoto wenye upungufu wa akili (wasio na akili nzuri).

v. Kutokea kwa kansa katika mlango wa uzazi.

vi. Msichana kuadhirika kisaikolojia.

WANAFUNZI WEMA WANAHITAJIKA KUWA NA YAFUATAYO :-

ü Nidhamu,

ü Ushirikiano,

ü Heshima,

ü Bidii/Kujituma,

ü Mdadisi/Mbunifu,

ü Mwajibikaji,

ü Mnadhifu,

ü Mtiifu,

ü Msikivu na

ü Mwenye Upendo.

Ukiwa ni mwanafunzi jiulize na kujifunza mazingira magumu pia Jitahidi kuwa na marafiki wema wanaohitaji kupata elimu (Utambue kuwa huyu rafiki anapendelea nini/ mambo gani au anataka nini kutoka kwako? Kipimo kiwe ni je anapenda kusoma?

Hivyo ukiwa ni mwanafunzi mwema na unayetaka maendeleo usikurupuke kuchagua marafiki wa kuwa karibu nao, watafute marafiki wanaoweza kukusaidia kimasomo.

Wanafunzi wengi hawajui kupanga muda wa kujisomea , akishafundishwa anafunika daftari anasubiri mpaka mtihani ukaribie ndipo anaanza kujisomea.

ZIFUTAZO NI BAADHI YA CHANGAMOTO ZILIZOJITOKEZA KATIKA SEMINA HII:-

Ø Bedecca imeshindwa kutoa vipeperushi vyenye elimu elekezi kutokana na ukosefu wa vifaa vya kudurufia na kuchapia (photocopy machines and printing machines).

Ø Bedecca imeshindwa kurekodi semina mbalimbali iliyokuwa ikitolewa katika sehemu husika kutokana na ukosefu wa vifaa vya kurekodia au vinasa sauti.

Matarajio ya uongozi wa Bedecca ni kufikisha/kueneza elimu hii kwa shule zote za msingi na sekondari zote ili wanafunzi wajue umuhimu wa elimu kwani baadhi ya wanafunzi huwa hawamalizi shule kuanzia shule za msingi hadi sekondari katika halmashauri ya Busokelo na Tanzania yote kiujumla.

Kutokana na semina iliyotolewa uongozi wa Bedecca unaamini kuwa ufaulu wa wanafunzi utaongezeka kwa kiwango kikubwa pia na swala la utoro mashuleni utapungua kwa kiasi kikubwa.

Uongozi wa Bedecca unapenda kutoa shukrani kwa mratibu kata, kata ya kandete kwa kutoa ushirikiano wake mkubwa pamoja na waalimu wote wakuu wa shule husika, kwa kweli ushirikiano huo walioutoa uwe endelevu ili kukuza taaluma kwa wanafunzi wote Tanzania.

Mwenyezi Mungu awabariki kwa ushirikiano wenu.

Wenu katika ujenzi wa Taifa,

Peter A. Mwakatobe

Katibu mtendaji - Bedecca.
 
Ndaga Fijo Ba Kukaja Kyala Ajege Nanumwe Amasiku Gosa Itolo
 
Back
Top Bottom