Taarifa ya Waziri Kairuki inajichanganya na haina misingi ya haki

abudist

JF-Expert Member
Oct 25, 2009
850
781
Baada ya kukurukakara na majigambo yote ya serikali ya kuondoa wafanyakazi wenye vyeti vya kughushi serikalini. Taarifa ya waziri Kairuki imetufundisha mambo kadhaa kwamba:

  • Serikali hii imewagawanya raia yake kwenye madaraja mawili imekuwa na raia wa aina mbili wa daraja la kwanza na la pili. Raia wa daraja la kwanza hawaguswi na wako juu ya sheria kama kina Daudi Bashite. Na raia wa daraja la pili wanafungwa kwa makosa hayo hayo ya jinai yaliyofanywa na hao raia wa daraja la kwanza.
  • Huyu rais anapanda sumu na kuwagawanywa watanzania, leo anasema hili na kesho anasema lile. Anasema anapiga vita uhalifu na kuwatetea wanyonge na hapo hapo anawalinda wahalifu kibabe na kuwaadhibu wengine kwa makosa hayo hayo.
  • Mawaziri wake serikali ya awamu ya tano wengi ni wanafiki hawachukui hatua stahiki za maamuzi mbali mbali kwa ajili ya kumogopa na kumridhisha Rais.
  • Serikali hii inajichanganya jinsi gani inaitumia hii katiba ya sasa ambayo imepitwa na wakati. Katiba haiwatambui wanachama wa majeshi kama ni wanasiasa, lakini hapo hapo kwa kauli ya waziri Angela Kairuki inaonyesha wanajeshi walioteuliwa kwenye vyeo mbalimbali hususan wakuu wa mikoa kuwa ni wanasiasa.
  • Matokeo ya uchunguzi huu yanawafanya watanzania kuamini haki haiko pande zote kama inavyotakiwa! Kitendo cha waziri Kairuki kusema ''Zoezi hili halikuhusisha Viongozi wa Kisiasa wakiwemo mawaziri, wabunge, wakuu wa mikoa, wa wilaya na madiwani. Kwa mujibu wa sheria na kanuni za nchi, wote tunafahamu uteuzi na uchaguzi kwenye nafasi zao unafanyika kwa misingi ya wahusika kujua kusoma na kuandika, Ibara 67 (1) ya Katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania'' Kwa hiyo kauli hii imetamkwa kumkinga mkuu wa mkoa wa Dar es salaam na kumfurahisha mtu aliyemteua.
  • Taarifa hii pamoja na kuwabainisha watumishi walioghushi vyeti, lakini pia imethibitisha rasmi kwa kwa njia ingine kwamba serikali inatambua kwamba mkuu wa mkoa wa Dar es salaam ana vyeti vya kughushi. Na imetumia ibara hiyo ya Ibara 67 (1) kumkinga yeye binafsi na siyo kwa faida ya taifa.
  • Kama Paulo Makonda ni halali kuendelea kuwepo kwenye nafasi yake kwa misingi kateuliwa kisiasa kwa kuwa ' kusoma na kuandika' ingawaje kaghushi vyeti. Basi hata hao watumishi 9000 waachwe. Kwa sababu hata hao walioghushi si wanajua kusoma na kuandika pia? Badala ya kuhakiki watu wa juu kwanza ambao ndiyo wanafanya maamuzi makubwa wao eti ndiyo wameachwa!
Serikali inatakiwa kujua pamoja na jitihada zote wanazofanya kumlinda Daudi Bashite lakini wajue sheria ni msumeno. Na hamna Ibara yeyote katiba hii inayomlinda mkuu wa mkoa wa Dar kwa kughushi vyet,i au kuapa angali akijua binafsi amedhamiria kudanganya na haya ni makosa ya jinai. Kama kuna ibara hiyo waziri Kairuki ilete hapa.
 
Mawaziri wako smart, very smart indeed! waropoke watakula kwako? Wanajua wanachokifanya, kuwa mengi ni kinyume cha haki na sheria etc, ila ni WANAFIKI WA KUTUPWA. Kairuki anajua fika kuwa anayoyafanya ni kinyume cha taratibu, lakini kaagizwa au anaangalia mdomo wa Boss unachexza vipi!
 
Kwa yanayoendelea kufanyika chini ya uongozi ni kumwomba Mungu atuvushe salama kwani kadri siku zinavyozidi kusonga mbele mwisho wake haueleweki.
 
IMG-20170430-WA0030.jpg

Sehemu ya Waraka wa Serikali kuhusu Tawala za Mikoa, Angalia Qualifications za Mtu anayepaswa kushika cheo cha Mkuu wa Mkoa ni atleast awe na degree moja au Equivalent!
 
Back
Top Bottom