Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
Ndugu waandishi wa habari;
LEO tumewaita hapa ili mtufikishie ujumbe kwa wananchi, kuhusu mambo manne makubwa.
Kwanza, Baraza la Uongozi la mkoa wa Pwani CHADEMA, linampongeza kwa dhati, mwenyekiti wa taifa wa Chadema, Mhe. Freeman Mbowe mbunge wa Hai na kiongozi wa kambi rasmi ya Upinzani bungeni kwa kumteuwa Waziri mkuu mstaafu, Mh. Fredrick Sumaye, kuwa mjumbe wa Kamati Kuu (CC) ya Chadema.
Baraza la uongozi la Mkoa wa Pwani limepokea uteuzi wake huo kwa moyo mkunjufu na linampongeza Mhe. Sumaye kwa kukubali uteuzi huo.
Tunafanya hivyo, kwa kuzingatia kuwa Mhe. Sumaye atakisaidia chama chetu kuimarika na kwa kuwa yeye ni mkazi wa Kiluvya – wilayani Kisarawe mkoani Pwani, mkoa huu utanufaika zaidi na mchango wake.
Kwa niaba ya Baraza la uongozi la Mkoa wa Pwani, ninachukua nafasi hii kumkaribisha sana Mhe. Sumaye katika safu ya uongozi wa mkoa wa Pwani na hii linatokana na matakwa ya katiba ya CHADEMA, toleo la 2006 Ibara ya 7.5.3(f), inayomtambua Mjumbe wa Kamati Kuu na Baraza Kuu anayeishi katika mkoa husika.
Pili, nyote mnafahamu kinachoendelea bungeni. Kwamba serikali kwa njia ya mabavu imezuia urushaji wa matangazo ya Bunge; Bunge limevamiwa na serikali na kuporwa mamlaka yake muhimu kwa ustawi wa taifa na hotuba ya Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni kuhusu wizara ya mambo ya ndani, iliamriwa kuhaririwa kwa maelekezo ya Ikulu.
Hotuba ya upinzani iliyokuwa iwasilishwe bungeni na waziri kivuli wa mambo ya ndani, Mh. Godbless Lema, ambaye ni mbunge wa Arusha Mjini, ilisheheni hoja na ililenga kuumbua serikali kuhusu sakata la ukwapuaji wa mabilioni ya shilingi uliofanywa na kampuni ya Lugumi.
Aidha, baadhi ya wabunge wa upinzani, wamefukuzwa bungeni kwa amri ya Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson, kinyume cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano, Kanuni za Kudumu za Bunge na sheria nyingine za nchi.
Mapambano kati ya Dk. Tulia Ackson na wabunge wa upinzani yanafahamika. Ni wao waliompinga alipogombea nafasi hiyo baada ya kugonga mwamba katika jitihada zake za kuwa Spika wa Bunge akiwa mtumishi wa umma nafasi ya naibu mwanasheria mkuu wa serikali.
Dk. Tulia aliteuliwa haraka na Rais Magufuli kuwa mbunge na hapo hapo kugombea tena nafasi ya naibu spika na kuandika historia kuwa mtu wa kwanza Tanzania kuomba nafasi zote za Uspika na Unaibu Spika akiwa sio mbunge wa jimbo/kuchaguliwa na baadae kuwa naibu spika wa kwanza ambae hana jimbo.
Uongozi wa Dk. Tulia umethibitisha kuwa hauhitaji kuwa na shahada ya chuo Kikuu kumjua anayemtumikia. Hivyo basi, Baraza la uongozi la Mkoa wa Pwani, linalaani kwa nguvu zote ukiukwaji wa Katiba unaotendwa na Naibu Spika; na kwamba tunaunga mkono maamuzi ya wabunge wa upinzani wa kususia vikao vya Bunge vinavyosimamiwa na yeye.
Baraza la uongozi la Mkoa wa Pwani linawataka wabunge hao kutoteteleka kusimamia haki zao na haki za watanzania wengine. Wananchi wana imani kubwa sana na wabunge wanaotokana na upinzani kwenye kusimamia hoja na haki zao.
Ndugu waandishi wa habari; kitendo cha kuzuiwa urushwaji wa matangazo ya moja kwa moja ya Bunge mara baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu, kumethibitisha kuwa taifa hili linaelekea katika utawala wa kiimla.
Sababu zilizotolewa awali zilikuwa ni gharama za kurusha matangazo ya Bunge na kwamba Shirika la Utangazaji la taifa (TBC), halina uwezo wa kuendelea kurusha vipindi vya Bunge.
Vituo binafsi vya televisheni vilionyesha utayari wa kuonyesha matangazo ya Bunge. Wadau wa habari na upashaji habari wakaridhia kulipia gharama hizo ili TBC ionyeshe matangazo ya Bunge, lakini serikali ikaja na kisingizio kingine.
Kwamba, ni utamaduni wa mabunge ya Jumuiya ya Madola kuwa na studio zake wenyewe za kurekodi na kurusha matangazo ya Bunge. Hoja hapa ikatoka kwenye gharama. Lakini kilichopo bungeni, siyo studio ya Bunge kurekodi na kurusha matangazo ya Bunge. Ni kuzuia urushaji wa matangazo.
Sisi tunajiuliza, kwa takribani miaka 10 Bunge lilipokuwa linaonyeshwa live jumuiya ya madola iliwahi kulalamikia Tanzania kutofuata utamaduni wake? Je, nchi zingine haziwezi kuja kujifunza kwetu jinsi matangazo ya Bunge yanavyorushwa na televisheni wakati wote yakiwa live?
Ndugu waandishi wa habari; serikali ikajichanganya tena, safari hii ya “Hapa Kazi Tu,” ikasema uonyeshwaji wa Bunge huwafanya baadhi ya wafanyakazi wa umma na sekta binafsi kushindwa kufanya kazi ipasavyo. Haya yalisemwa na waziri mkuu akiwa Uingereza akizungumza na watanzania waishio huko.
Hapa kuna maswali kadhaa ya kujiuliza: Je, kuna utafiti wowote wa kitaalam umeshafanyika kuonyesha ufanisi wa kazi umepungua kwa miaka 10 Bunge lilipokuwa linaonyeshwa? Waajiri wamelalama mahali popote wafanyakazi hawafanyi kazi kwa sababu wanafuatilia Bunge? Je, serikali itaziondoa TV zote zilizopo katika ofisi za umma ili kuendana na hoja hiyo?
Ndugu waandishi wa habari; vitendo hivi na vingine, ikiwamo hatua ya serikali ya kufungia gazeti la kila wiki la MAWIO; kuongezeka kwa vitendo vya kuwakamata watu wanaokosoa serikali kupitia mitandao ya kijamii na kisha kuwabambikiza kesi za makosa ya sheria ya mitandaoni; pamoja na mwenendo wa Rais Magufuli wa kutaka kuandikwa yeye pekee kwenye vyombo vya habari, ni ishara tosha kuwa rais na serikali yake, hawako tayari kupokea mawazo kinzani.
Tatu, jingine ambalo tunaomba mlifikishe kwa umma, ni hili la jeshi la polisi kuzuilia mikutano ya vyama vya upinzani. Ndugu waandishi wa habari; mnakumbuka kuwa mnamo tarehe 07 Juni 2016, limetolewa tamko na jeshi la polisi kuzuia mikutano ya vyama vya siasa na maandamo eti kwasababu za kiintelejensia. Baraza la uongozi la mkoa wa pwani limeshitushwa sana taarifa hiyo ya jeshi la polisi.
Tukiangalia kanuni za jumla za jeshi la polisi namba 403 kifungu cha kwanza inasema;(a) “Any person who is desirous of convening, collecting, forming or organizing any assembly or procession in any public place shall, not less than forty eight hours before the time when the assembly or procession is scheduled to take place submit ‘a written notification’ of his impending assembly or procession to the police officer in charge of the area.”
Hivyo hitaji hapa kwa anayetaka kufanya maandamano au mkutano wa hadhara kwa mujibu wa sheria hii ni kutoa “TAARIFA” tu tena katika kipindi kisichopungua saa arobaini na nane (48).
b) ‘ where a person submits a notification in accordance with the preceeding paragraph, he may proceed to convene, collect, form, or organise the assembly or procession in question as scheduled unless and until he receives an order from the Police Officer in charge of the area directing that the assembly or procession shall not be held as notified.
Hii inasisitiza kuwa Polisi “Officer in charge” wa eneo, ambalo linatajwa hapa ni OCD. Baraza la uongozi la mkoa wa pwani limeshitushwa kusikia msemaji wa jeshi la polisi amekataza mkutano wa hadhara ambao tayari OCD wa wilaya ya Kahama alikuwa amesharidhia kwa maandishi na ametekeleza wajibu wake kama kanuni ya jeshi la polisi linavyomtaka afanye.
Baraza la uongozi mkoa wa Pwani linawasihi viongozi wa jeshi la polisi kuacha kutumika kisiasa na kama wanataka kufanya siasa wavue jezi zao tukutane majukwaani na mtaani wakati wa ujezi wa vyama na demokrasia.
Upo ushahidi mwingi wa jeshi la polisi kutumika kisiasa. Mfano hai, ni pale aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoani Iringa, Michael Kamhanda, alipoagiza kuzuiwa kwa mkutano wa Chadema, katika eneo la Nyororo mkoani Iringa.
Amri hii iliyotolewa tarehe 2 Septemba 2012, siyo tu ilikuwa kinyume cha sheria, bali ilisababisha mauaji ya mwandishi wa habari, Marehemu Daud Mwangosi.
Hata ripoti iliyotolewa na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, chini ya Jaji Manento ilieleza kuwa jeshi la polisi lilitenda kinyume na sheria ya vyama vya Siasa (Cap 258 RE. 2002) kifungu cha 11 (a) na (b) na Sheria ya Polisi (Sura 322).
Jaji Manento alisema, Kamanda Kamuhanda alikiuka sheria hizo Kwa kuingilia kazi za mkuu wa Polisi Wilaya (OCD) ya Mufindi na kutoa amri ya kuzuia shughuli za CHADEMA wakati yeye (Kamuhanda) hakuwa kiongozi wa polisi wa eneo husika.
Ndugu waandishi wa habari; kwa haya na mengine ambayo hatukuyataja, Baraza la uongozi la mkoa wa Pwani, linawataka wafuatao kutekeleze wajibu wao kwa mujibu wa Sheria, Katiba, Kanuni na taratibu za nchi, maana hii nchi ni yetu sote; amani na utulivu wake unatokana na kila mmoja kuheshimu sheria na kanuni.
Kwanza, ni Jeshi la Polisi; Barazala uongozi la CHADEMA-Pwani linataka liache mara moja kutumika na CCM kwa maslahi yake ya kisiasa. Liheshimu taratibu, kanuni na sheria za nchi na watekeleze wajibu wao wa kulinda “Usalama wa raia na mali zao.” Kazi ya siasa waachie wanasiasa na vyama vya siasa.
Pili, Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson. Huyu Baraza la uongozi la Mkoa linamtaka kuacha mara moja kutumia na kutafsiri kanuni za Bunge vibaya kwa maslahi ya chama chake - CCM na serikali yake. Kumbukumbu sahihi za Bunge – Hansard –zitamweka katika kumbukumbu mbaya kwa sasa na vizazi vijavyo.
Baraza la uongozi la Mkoa wa Pwani linamtaka kutoongozwa na mapenzi makubwa ya kuilinda CCM na serikali. Atumie Katiba inayotoa mamlaka kwa Bunge kuisimamia serikali.
Tatu, ni Rais John Pombe Magufuli. Baraza la uongozi la mkoa, linamtaka Rais kutekeleza kwa vitendo kauli yake ya hapa kazi tu kwa kuruhusu wengine watekeleze kazi zao za kuisimamia na kuishauri serikali yake. Aruhusu waandishi wa habari waandike kwa uhuru habari zao hata kama zinakinzana na anayopenda kusikia, ikiwamo Bunge kurusha matangazo yake na Mahakama kufikia maamuzi ya huru na haki juu ya mashauri yaliyopo.
Siyo jukumu la rais kutoa maagizo na maelekezo kwa kutumia vitisho, uteuzi wake kwa baadhi ya watu au zawadi za mabilioni ya shilingi kwa vyombo kama Mahakama.
Ndugu waandishi wa habari naomba mfikishe salaam zetu hizi kwa watanzania wote
CHADEMA VEMA, PEOPLE’S …POWER
Kwa niaba ya baraza la uongozi la mkoa wa Pwani,
Baraka Mwago
Mwenyekiti wa CHADEMA – mkoa wa Pwani.