Taarifa ya Upatikanaji wa Mayai Nchi Tanzania

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,806
11,968

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI

TAARIFA FUPI KUHUSU TAARIFA ZINAZOZUNGUKA KWENYE MITANDAO YA KIJAMII (SOCIAL MEDIA) JUU YA KUSHUKA KWA BEI YA MAYAI NCHINI

15 JUNI 2021


1. UTANGULIZI
Tarehe 15/06/2021 Wizara ya Mifugo na Uvuvi iliona ujumbe unazunguka kwa njia ya WhatsApp kuhusu uwepo wa mayai mengi nchini kiasi cha kwamba bei yake umeshuka ghafla mpaka kufikia shs 4000= kwa trei. Ujumbe huo ulikuwa na kichwa cha habari kinachosomeka “SOKO LA MAYAI DSM KITENDAWILI” na ujumbe wake ulisomeka kama ifuatavyo:

“Kuna changamoto imejitokeza ghafla kwenye Soko la mayai nchini. Mayai jijini DSM yanauzwa hadi TZS 4,000 kwa tray moja na wanakuachia tray. Kwa mfugaji wa kuku wa mayai Nchini Tanzania hawezi kabisa kushindana kwa bei hiyo.

Mayai hayo yanadaiwa kuingizwa kutoka nchini Kenya. Hali hii ikiendelea kwa mwezi mmoja tu, wafugaji wa bongo watauza au kuchinja kuku maana kwa wastani wa TZS 5000 ndio mfugaji wa bongo anarudisha gharama za uendeshaji (break-even point) hawezi kuvumilia hasara ya TZS 1000 kwa zaidi ya mwezi.

Ninachojiuliza, hivi kweli inawezekana Kenya wazalishe mayai na kusafirisha hadi Dar kisha wauze kwa TZS 4000= za bongo na wapate faida? Kwa nini walete mayai kwa bei ya chini na wasilete chakula cha kuku kwa bei ya kutupwa?

Jibu ni rahisi sana. Wanafanya hivyo makusudi ili kuua uzalishaji wa mayai Tanzania na kisha wakifanikiwa hilo, watapaisha bei juu na hapo ni wao tu watakuwa wazalishaji. Wenzetu wana uzoefu wa uchumi wa kibepari namna ya kushindana.

Hapa serikali lazima iliangalie vizuri maana gharama za uzalishaji kwa TZ bado ziko juu sana na kushuka ni changamoto kwa kuwa Soya ambayo hutumika kutengeneza chakula cha kuku ilipata soko China na kusababisha kupanda kwa bei ya chakula.

Waziri wa kilimo na mifugo na wasaidizi wao wasipoliangalia hili kwa makini yafuatayo yatatokea!

1. Mitaji ya watu itakatika ghafla.

2. Waliokopa watakwama, marejesho yatashindikana na kupoteza mali walizoweka dhamana.

3. Mabenki hayawezi kurejesha fedha yote kwa kupitia minada ya stressed sale!

4. Ufugaji wa kuku Tanzania hasa DSM utasimama kwa muda ili wadau wajipange upya.

5. Viwanda vya chakula cha kuku vitapunguza sana uzalishaji na kujikita kwenye chakula cha broilers.

6. Wafanyakazi wa mashamba ya kuku na viwandani watapoteza ajira zao.

7. Serikali itapoteza kodi kupitia kushuka kwa uzalishaji wa viwanda husika.

8. Waliokuwa wanafanya kazi kwenye mashamba ya kuku watapata ajira mpya ya umachinga wa mayai kutoka nje.

9. Wakulima wa mazao ya nafaka yaliyokuwa yanatumika kuzalisha chakula cha kuku watakosa soko la ndani la mazao yao.

10. Wachuuzi wa mahindi na nafaka zingine watatafuta soko nje ya nchi ikiwemo kenya.

11. Nafaka zitashuka bei na kupelekwa nje kwa bei ya kutupwa ikiwemo Kenya. Na hivyo kufanya gharama za uzalishaji wa chakula cha kuku nchini humo kushuka zaidi na hivyo kuendelea kutuletea mayai hayo kwa bei ya chini zaidi.

12. Tanzania itaendelea kuwa muuzaji wa malighafi na muagizaji wa bidhaa za viwandani na za mifugo.

Najiuliza maswali kadhaa:

1. Kitu gani kimetokea?

2. Aliyekuruhusu anajua madhara yake?

3. Je huo ndio uchumi wa kati?

4. Je, serikali imeangalia kwa makini madhara ya maamuzi haya?

5. Je waziri husika amekusudia nini?

Mimi ni mfugaji na ninaonge nikiwa na mayai ya kutosha sana yanayoongezeka kila siku nalazimika kuuza ili kuwalisha tu nikiwa naangalia long term trend”.

Baada ya kuona ujumbe huo, Wizara ya Mifugo na Uvuvi imefanya uchunguzi wa ukweli wa ujumbe huu na kuepndekeza hatua za kuchukuliwa.

2. UCHUNGUZI WA HALI YA UPATIKANAJI WA MAYAI NCHINI NA BEI ZAKE
Tarehe 15/06/2021 Wizara ya mifugo na Uvuvi ilifanya uchunguzi kwenye Miji mikubwa yote nchini na baadhi ya Wilaya ili kujiridhisha juu ya upatikanaji wa mayai, bei ya trei ya mayai na soko lake kwa ujumla.

Njia zilizotumika kukusanya taarifa ni pamoja na:

Kuongea na wafugaji wakubwa wa kuku wa mayai;

Kuongea na wafanyabishara wakubwa na wadogo wa mayai;

Kufika sehemu za masoko kunakouzwa mayai na kujionea hali halisi ikiwa ni pamoja na kujua bei ya trei ya mayai, upatikanaji wake na hali ya soko kwa ujumla;

Kuongea na Maafisa Mifugo wa Mikoa, Majiji, Manispaa na Halmashauri ili kupata taarifa juu ya bei ya trei ya mayai, upatikanaji wake na hali ya soko la mayai kwenye maeneo yao ya kiutawala.

3. MATOKEO YA UCHUNGUZI
Zoezi hilo limefanyika nchini kote na muhtasari wa matokeo umeoneshwa kwenye jedwali namba moja hapa chini. Kwa ujumla, katika ngazi ya mfugaji bei ya trei la mayai ilikuwa kati ya shs 6,500 mpaka 9,000. Aidha, kiwango cha chini kabisa cha bei ya trei la mayai katika ngazi ya mkulima kilikuwa shs 6,000 katika Manispaa ya Sumbawanga. Uchunguzi ulibaini zaidi kuwa bei ya trei la mayai sokoni ilikuwa kati ya shs 6,800 mpaka shs 12,000. Jedwali namba moja hapa chini ni taarifa zaidi ya bei ya mayai katika mikoa 26 ya Tanzania Bara.

Jedwali la 1: Bei ya mayai katika ngazi ya mfugaji na sokoni zilizokusanywa tarehe 15/0672021 kutoka kwenye mikoa 26 ya Tanzania Bara

MkoaJiji / Manispaa
/ Halmashauri
Bei kwa trei la mayai ya kununua kwa mfugaji (shs)Bei kwa trei la inayouzwa sokoni
(shs)
Hali ya upatikanaji wa mayaiMaelezo
GeitaGeita TC8,500 - 9,0009,000 - 10,000KawaidaVifanga havipatikani kwa urahisi
MwanzaJiji la Mwanza7,000 - 8,0008,500 - 9,500WastaniWalaji wa mayai ya kuku wa kisasa wamepungua na sababu labda hali ya uchumi ngumu
ShinyangaManispaa ya Shinyanga7,0009,000KawaidaVifanga havipatikani kwa urahisi
KageraManispaa ya Bukoba6,500 - 7,0008,000 - 9,000KawaidaVifanga havipatikani kwa urahisi
Missenyi8,0009,000KawaidaChakula cha kuku kinapatikana kwa urahisi na gharama nafuu
MaraManispaa ya Musoma7,0008,500 - 9,000KawaidaVifanga havipatikani kwa urahisi
SimiyuBariadi TC8,0009,500 - 10,000KawaidaVifanga havipatikani kwa urahisi
KigomaManispaa ya Kigoma8,000 - 8,5009,500 - 10,000KawaidaKumekuwa na uhaba wa vifaranga
TaboraManispaa ya Tabora8,000 - 9,0009,500 - 10,000KawaidaKumekuwa na uhaba wa vifaranga
SingidaManispaa ya Singida7,5008,000KawaidaKumekuwa na uhaba wa vifaranga
DodomaJiji la Dodoma8,0008,500 - 9,000KawaidaKumekuwa na uhaba wa vifaranga
MorogoroManispaa ya Morogoro7,000 - 75008,000 – 8,500Kawaida, bei imebakia ileile kati ya Januari na Juni,
Bei ya yai moja moja ni shs 250=
Baadhi ya makampuni yamepandisha bei ya vyakula vya kuku kuanzia Juni.
PwaniMji wa Kibaha6,500 - 7,0007,000 - 7,500KawaidaBei imekuwa hivyo kwa muda mrefu,
Upatikanaji wa mayai sio tatizo kwa kuwa kuna mashamba makubwa
Dar es SalaamJiji la DSM6,500 - 7,0006,800 - 8,000Kawaida,
Bei ya yai moja moja ni shs 250 – 300=
Bei imekuwa hivyo kwa muda mrefu,
Upatikanaji wa mayai sio tatizo kwa kuwa kuna mashamba makubwa
TangaJiji la Tanga7,000 - 8,0008,000 - 9000KawaidaUpatikana wa mayai sio shida katika Jiji la Tanga na maeneo jirani
KilimanjaroManispaa ya Moshi7,500 - 8,0008,000 - 9,000Kawaida,
Bei imekuwa hiyo tangu Januari mpaka Juni
Kumekuwa na upungufu wa vifaranga wa mayai
ArushaJiji la Arusha7,500 - 8,0008,500 - 9,000Kawaida, bei imekuwa hiyo tangu Januari mpaka JuniKumekuwa na upungufu wa vifaranga wa mayai
ManyaraBabati8,500 - 9,0009,500 - 12,000Upatikanaji ni shidaUhaba wa vifaranga
IringaManispaa ya Iringa6,500 - 7,0007,500 - 8,000Upatikanaji ni shidaHali ya baridi imechangia upungufu huu
NjombeNjombe Mjini6,500 - 7,0007,500 - 8,000Upatikanaji ni shidaHali ya baridi imechangia upungufu huu
MbeyaJiji la Mbeya6,500 - 7,0007,000 - 7,500Upatikanaji ni shidaVifaranga havipatikani kwa urahisi
SongweMbozi6,500 - 7,0007,500 - 7,800Upatikanaji ni shidaUzalishaji ni mdogo kwa maeneo mengi ya mkoa wa Songwe kwa sababu ya uhaba wa vifaranga
RukwaManispaa ya Sumbawanga6,000 - 6,5007,000 - 7,500Mayai ni machache sokoniUzalishaji ni mdogo,
Upatikanaji wa vifaranga shida
Nkasi7,000 - 7,5007,500 - 8,000Mayai ni machache sokoniUzalishaji ni mdogo,
Upatikanaji wa vifaranga shida
KataviManispaa ya Mpanda8,000 - 8,5009,000 - 9,200Uzalishaji ni mdogo,
Mayai mengi yanaingia kutoka Tabora
Mpimbwe8,000 - 9,0009,000 - 12,000Mayai ni machache sokoniUzalishaji ni mdogo,
Mayai mengi yanaingia kutoka Tabora
RuvumaManispaa ya Songea6,500 - 7,0007,500 - 8,000Kuna uhabaUzalishaji ni mdogo,
Mayai mengi yanaagizwa kutoka Iringa na Njombe
Mbinga7,000 - 8,0008,000 - 9,000Kuna uhabaUzalishaji ni mdogo,
Wafugaji wa kuku wa mayai Mbinga ni wachache sana
MtwaraMtwara mjini7,000 - 8,0008000 - 9000Kawaida
Bei hii imekuwepo tangu Aprili – Juni 2021
Baadhi ya wafanyabishara wanatoa mayai Mkuranga (Pwani) na Dar es Salaam
LindiLindi Mjini8,000 - 8,5008500 - 9000Kawaida
Bei hii imekuwepo tangu Aprili – Juni 2021
Baadhi ya wafanyabishara wanatoa mayai Mkuranga (Pwani) na Dar es Salaam

4. MAONI YA WIZARA JUU YA UJUMBE KUHUSU KUINGIA KWA MAYAI NCHINI
Kutokana na ujumbe uliosambazwa kwenye mitandao (social media), Wizara ya mifugo na uvuvi ina maoni yafuatayo:

Baada ya kufanya uchunguzi wa kina katika mikoa yote 26 ya Tanzania Bara, imebainika kuwa hakuna uwingi wa mayai uliopelekea kushuka kwa bei ya mayai katika ngzi ya mfugaji na sokoni;

Kinachoonekana zaidi ni kuwa kuna upungufu mkubwa wa mayai nchini uliopelekea bei kupanda zaidi mpaka kufikia hadi shilingi 12,000= kwa trei kwenye baadhi ya maeneo kama halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe;

Taarifa zilizosambazwa ni uzushi mtupu na hazina ukweli wowote;

Kumekuwa na matukio machache ya uingizaji wa mayai nchini kwa njia za panya lakini kumekuwa na vikosi vya doria ambavyo vimekuwa vikidhibiti hali hiyo;

Serikali ilishazuia uingizwaji wa kuku na mazao yake kutokana na uwepo wa tishio la mafua makali ya ndege duniani. Wizara imekuwa ikitoa vibali maalum vya kuingiza vifaranga na mayai ya kutotolesha ya kuku wazazi;

Mwezi wa Aprili, chama cha wafugaji wa kuku waliomba waruhiswe kuingiza vifaranga wa kuku wa nyama, vifaranga wa kuku wa mayai na mayai ya kutotolesha kutokana na uhaba mkubwa uliojitokeza kutokana na uwepo wa mlipuko wa ugonjwa wa Covid 19 duniani;

Ugonjwa wa COVID 19 umepunguza sana uzalishaji wa vifaranga katika maeneo mengi ambako kumepelekea kupungua kwa kuku wa mayai na hatimaye upungufu wa mayai uliopo nchini;

Taarifa zisizo rasmi ni kwamba hata huko nchini Kenya kuna upungufu wa mayai katika soko kwa maana mahitaji ya mayai ni makubwa kuliko yanayozalishwa;

Ili kukabiliana na hali hii, Serikali imeruhusu kuingiza vifaranga wa kuku wa nyama, vifaranga wa kuku wa mayai na mayai ya kutotolesha kwa kipindi cha miezi mitatu kuanzia mwezi wa Juni mpaka Agosti 2030;

Tayari makampuni kadhaa yameshaanza kuingiza nchini vifaranga na mayai ya kutotolesha.

5. MAPENDEKEZO YA WIZARA
Uzushi uliojitokeza kutokana na kusambazwa kwa ujumbe wenye taarifa za kupotosha kuhusu kuingizwa kwa mayai nchini kutokea nchi ya Kenya unapaswa upuuzwe;

Mtu aliyezusha taarifa hizi za uongo ana nia ovu na tasnia ya ufugaji kuku Tanzania na ameleta taharuki kubwa kwa wafugaji wetu;

Kwa kuituhumu nchi ya jirani ya Kenya kuwa inahujumu ufugaji kuku wa Tanzania pasipokuwa na ushahidi wa aina yoyote ni kudhoofisha mahusiano ya kideplomasia kati ya nchi yetu na Kenya;

Tunapendekeza kuwa vyombo ya kiuchunguzi vichunguze chanzo za taarifa hizi na hatua stahiki ziweze kuchukuliwa dhidi ya mtu huyu mwenye nia ovu ambaye ametengeneza na kusambaza taarifa za uongo zilizoleta taharuki kwenye jamii.
 
Tuwe makini sana na wa kenya hawana dhamira nzuri kabisa na Tanzania.

Sio katika hili la mayai tu bali kila sehemu zetu nyingi wanajiingiza kama wameitwa! Kutu chokonoa kutuchunguza maisha yetu ili waharibu.

Wivu mkubwa ulio ambatana na chuki na roho mbaya walizo nazo ni hatari kuliko tunavyo fikiri kuliko tunavyojua!

Hatari sana hawa viumbe!

Waondoke kabisa! Hatuwahitaji Tanzania.

Waondoke!....
 
Kama mnawauzia kenya mahindi na bidhaa nyingine za kilimo hamtaki nao wawauzie vya kwao? protectionism haitasaidia chochote, watanzania kuweni tayari kushindana kwenye soko. Iweje wafugaji pekee ndo wanataka kulindwa huku mamilioni wakiumia kwa kununua mayai bei juu...
 
Karibu Songwe Tunduma mayai wanakula kutoka Zambia bei ni elfu 4 kwa trei! Pia mafuta ya kula, kuku mpaka beer castle lite from south Africa bei yake ni tsh 900! Karibu Sana, usisahau petrol Lita Moja hapa nakonde ni tsh 1500, so ukija na private unavuka upande wa pili unakula kiwese unachapa raba hakuna wa kuuliza wala kukufatatilia! Kwenye wese ila kwenye hivyo vingine tumia nakonde huko huko au Tunduma only.
 
Back
Top Bottom