Taarifa ya ukaguzi, national audit report, kutinga bungeni April 20 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Taarifa ya ukaguzi, national audit report, kutinga bungeni April 20

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pascal Mayalla, Apr 14, 2010.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Apr 14, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 23,551
  Likes Received: 14,430
  Trophy Points: 280
  Ile Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali, CAG, Ludovic Utouh, ijulikanayo kwa jina maarufu la Ripoti ya Ukaguzi, itawasilishwa rasmi Bungeni mjini Dodoma siku ya Jumanne Ijayo, Tarehe 20 April, 2010 Saa 3:05 asubuhi.

  Baada ya kuwasilishwa mezani kwa ripoti hiyo, CAG, Ludovick Utouh atafanya mkutano na Waandishi wa habari ambapo atatoa mhutaasari wa ripoti hiyo, itakayofuatiwa na maoni ya Wenyeviti wa Kamati za Hesabu za Serikali (John Cheyo), Serikali Mitaa (Dr. Wilbroad Slaa na Mashirika ya Umma (Zitto Kabwe) kwenye ukumbi wa Press Conference wa Bunge.

  Kuwasilishwa kwa ripoti hiyo kunaifanya ripoti hiyo kuwa public document, hali inayopelekea wanahabari kuipongeza serikali maeneo iliyofanya vizuri, na kuitundika msalabani maeneo yenye maroroso.

  Kama kawaida ya habari, serikali ikifanya vizuri sio habari kwa sababu ndio inavyotarajiwa kufanya vizuri, habari kubwa ni pale inapoboronga.

  Ripoti ya Mwaka huu pia itatoa picha halisi ya mrejesho wa matumizi ya lile fungu la fedha za EPA, zilizorudishwa, hivyo kumaliza minong'ono kama kweli zilirudi ama kilikuwa ni kiini macho tuu.

  Uthibitisho wangu kuwa fedha ni kweli zilirudi, ni kwa baadhi tuu ya washtakiwa kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria, hawa ni wale waliogoma kurudisha. Ila hata hao waliofikishwa mahakamani kama kina Jeethu (Jitu) Patel, wamefikishwa kwa kudaiwa kiasi kidogo tuu kile ambacho hawakukiridisha, hii ikimaanisha kile kiasi walichorudisha, hawajashitakiwa nacho.

  Ripoti ya mwaka huu pia itakuwa ya kwanza kuainisha balozi moja moja sio kama ile inaoziweka balozi zote ndani ya kapu la Wizara ya Mambo ya Nje, hali itakayopelekea uwezekano wa Wizara kama Wizara, kupata hati safi licha ya uchafu wa kwenye baadhi ya balozi zetu.

  Angalizo, Ripoti ya ukaguzi, ni ile ripoti inayaangalia kama sheria, taratibu na kanuni za matumizi ya fedha za umma zimefuatwa na sio ripoti ya ufanisi (efficiecy) au thamani, (Value for Money). Kwa maneno mengine, kama imepitishwa ndizi moja yakisukari ni Sh. 10,000, bajeti ya ndizo hiyo ilipitishwa, taratibu ya kuinunua ndizi hiyo zilifutwa, then ripoti ya ugaguzi huo, itakuwa niripoti safi.

  Tuisubirie Jumanne hiyo kama kawaida yetu, JF ni wa kwanza kupata habari, naahidi pia kuwa tutakuwa wa kwanza kuipata na kuirusha.
   
 2. T

  Tall JF-Expert Member

  #2
  Apr 14, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 1,431
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 0
  1.ukiipata ilete tu mzee...kiutaratibu pesa iliyokusanywa kama ile ya epa inatakiwa iwekwe kwenye deposit account (code to be created) na receipt hutolewa(erv) hizi ni risiti za serikali hutwa hivyo
  tatizo la hizi deposite account ni kuwa matumizi yake.....unalipa aliyeziweka akizitaka,kwa kuambatanisha risiti aliowekea,sijui tupo pamoja? Maqana hiyo ni government accounting.
  2.maeneo nyeti ya report:
  1.unvouched expenditure.
  2.improperly vouched
  3.missallocatins
  4. Nugatory expenditure
  hapa ndipo ulaji mwingi hutokea pesa nyingi za umma mabillion hupotelea hapo.
  3.tatizo ni kuwa,watu wachache sana kwa kweli ni watu wachache wanaoweza kuielewa ripoti inasema nini na inamaanisha nini.
  Nini epa bwana epa cha mtoto tu.

  Eeeeee eeee ngoja ninyamaze mie.
   
 3. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #3
  Apr 15, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 23,551
  Likes Received: 14,430
  Trophy Points: 280
  Tall, kwanza nakushukuru sana kwa sababu wewe ni mmoja wa wachache miongoni mwetu wanaoweza kupokea ripoti ya CAG na kui grasp. Wengi wetu including media zetu, zinamung'unya mung'unya tuu na kutupa tumeze mabonge mabonge. Ripoti ikitoka tuu, JF ni miongoni mwa media za kwanza kuipata, utatusaidia kuitafuna ili tuweze kumeza kwa urahisi.
  Nakuomba usijinyamazie.
   
 4. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #4
  Apr 15, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 23,551
  Likes Received: 14,430
  Trophy Points: 280
  Mode, naomba nirekebishie heading, siyo taarifa bali ni Ripoti ya Ukaguzi, hivyo heading isomeke "Ripoti ya CAG kutinga Bungeni Jumanne"
  Natanguliza shukrani.
  Pasco.
   
 5. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #5
  Apr 15, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 23,551
  Likes Received: 14,430
  Trophy Points: 280
  Mode bado nakumbushia Pleas change heading to "Ripoti ya CAG kutinga Bungeni Jumanne"
   
 6. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #6
  Apr 18, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 23,551
  Likes Received: 14,430
  Trophy Points: 280
  Mode, bado nakumbushia, naomba change headline isomeke Ripoti ya CAG kutinga Bungeni Jumanne.
   
Loading...