Dodoma: Ripoti ya CAG 2015/16 yawasilishwa, deni la taifa linakuwa kwa kasi ya 20%

Casuist

JF-Expert Member
Jul 23, 2014
1,179
2,940
Habari waungwana,
Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali(CAG) anawasilisha ripoti yake kwa wanahabari leo. Fuatana nami kujua atachosema.
======

Assad.jpg

Mkaguzi anasema ripoti inaonyesha fedha nyingi zaidi zilitumika katika matumizi ya kwaida kuliko matumizi ya maendeleo. Ukusanyaji ni mdogo wa maduhuri katika kusimamia bajeti. Bila kutumia mikopo, serikali ingeweza kugharamia asilimia 62 pekee ya bajeti yake.

Assad: Deni la Taifa limefikia trilioni 41 Juni 2016 kulinganisha na trilioni 33 2015 na kiasi hiko hakijajumuisha trilioni nane ambalo ni deni katika hifadhi za jamii, serikali iliadi kutoa non cash bond na haijatimiza.

Deni la taifa linakuwa kwa kasi, zaidi ya 20% ikimaanisha baada ya miaka mitano litakuwa mara mbili. Sio vizuri deni kukua kwa namna hii.

Serikali haikuwasilisha michango kwa mifuko ya hifadhi ya jamii ya bilioni 400, si busara serikali kuchelewesha kwani hata wastaafu watacheleweshewa.

Malipo ya mishahara ya bilioni 9.8 yaliyofanyika kwa wafanyakazi waliofariki, watu wamelipwa na kodi zimekatwa, serikali ifanye juhudi kuhakikisha database yao iko updated.

Mishahara kwa kawaida isipochokuliwa benki inaitwa unclaimed salaries na inatakiwa kurejeshwa hazina lakini tumefatilia hairejeshwi na mabenki.

Pia Assad kazungumzia baadhi ya taasisi kukosa hati za malipo na kusema anazitaka kwani sheria inamruhusu kuzidai. Magari 2172 yametelekezwa ikiwa ni ongezeko la 88% kutoka mwaka 2015, amesema magari yaliyofikia ukomo wa matumizi bora kuuza kama ipo busara ya kuuza au kuzipa taasisi nyingine ambazo zinaweza kuyatumia.

Bilioni 24 imetumika bila kushindanisha tenda, serikali inatakiwa kufuata sheria ya manunuzi.

Vyama vya siasa tumeshindwa kufanya ukaguzi kwa sababu havifati sheria na vitatu havina hata akaunti benki.

Benki ya wanawake mtaji umekuwa eroded kwani sheria ya benki kuu ni lazima mtaji ufike bilioni tano na yenyewe haina hivyo haitakiwi kuendelea.

Twiga benki japo imechukuliwa na benki kuu lakini ilifikia hasi ya bilioni 19, walikuwa wapi wahusika mpaka kufika hapo.

TANESCO inapata hasara kwa sababu muundo wake hauko sahihi hasa kwenye kununua umeme wa dharura na mpango huo hauna tija katika nchi hii, tunaishauri kufanya uwekezaji kuachana na mpango wa dharura.

Kuna mradi uko chini ya Rubada na tunafikiri hana uwezo.

Mifuko ya pensheni ishuka uwekezaji umeshuka kutokana na kutokuwepo ufanisi wa kusimamia mikopo.

Kampuni zote za madini hazijawahi kulipa kodi kutokana na faida, inawezekana vipi kuendesha biashara kwa miaka 10 bila faida? Lazima tuangalia muda wa allowances tunazotoa kwa kampuni za madini. Nchi nyingine hazifanyi kama tunazofanya sisi. Anatolea mfano wa Botswana ambayo inatumia kipimo cha madini yanayotoka na sio muda, ambapo kipimo kikifika wanagawana nusu kwa nusu na serikali.
=======

Majibu ya Maswali

Assad: Bajeti ya mwaka uliopita haikutosha lakini mwaka huu tumepewa bajeti.

Assad: Kuna watu wanapoteza nafasi zao na wengine wanateuliwa, mwisho wa kukaimu ni miezi sita. Watu wanatakiwa kukumbusha mamlaka ya uteuzi kuteua nafasi, sisi hatuwezi kupokea hesabu za watu waliosaini kwa niaba baada ya miezi sita.

Assad: NSSF Kigamboni nakumbuka malipo yanatokana na uuzaji wa nyumba na mbia hajaendeleza hivyo hakuna nyumba za kuuza.

Assad: Pale ambapo mtu atashindwa kutimiza mapendekezo aliyokubali yeye mwenyewe, tutaomba mamlaka ya uteuzi impe kazi nyingine.

Assad: TANESCO itaendelea kula hasara kwa sababu sehemu pekee ni kupunguza gharama, bei zinadhibitiwa hivyo wanatakiwa kupunguza gharama na kwa maoni yangu wawekeze katika uzalishaji wa umeme.
 
Mwaka 2015 ambao watanzania tulichezewa sana deni la taifa ni 33 trilion, mwaka 2017 mchezo ule wa watanzania kuchezewa sana tunadaiwa 41 trilion. Mmmmh Mbona kwa akili yangu naona kama saiz ndo Watanzania tunachezewa zaid!!! Miaka hiyo ya kuchezewa sana Tanzania tulikuwa tunapewa na ugali kwa bei cheee miaka hii kila kitu bei juu, deni nalo linapanda kwa kasi ya viwonder. MIKONO JUU MWENDO WA MATEKA.
 
Fedha nyingi zimekwenda kwenye matumizi ya kawaida na sio ya maendeleo......hayo matumizi ya kawaida ni yepi, so nasikia hakuna makopo ya NIDO siku ofisini......au ndio ile miradi ya mwanza, ukarabati wa ofisi na zawadi ya gari kwa shemeji?
 
Deni la taifa linakuwa kwa kasi kwa sababu sasa watanzania wengi hawazalishi hivyo kutokuwa na mchango kwenye uchumi wa nchi...
Serikali inabidi iwekeze sana kwenye kuzalisha ajira mpya ili watu wachangie kwenye output kuliko kukaa vijiweni... Pia ilazimishe utekelezaji wa miradi mingi kutumia larger share of labour / capital... Yani kazi nyingi zaidi zifanywe na watu kuliko mitambo ili kuongeza nafasi za ajira...
 
Nchi iko kwenye hali mbaya sana kiuchumi deni la taifa limezidi kuongeka kwa kasi kwenye utawala wa raisi huyu ambaye anasema anapambana na mafisadi pamoja wakwepaji wa kodi.
Deni la taifa linakuwa kwa kasi, zaidi ya 20% ikimaanisha baada ya miaka mitano litakuwa mara mbili. Sio vizuri deni kukua kwa namna hii.
 
Mwaka mmoja serikali imekopa trilioni 8? Inamaana ndani ya miaka 5 serikali itakua na wastani wa kukopa zaidi ya trilioni 35.
Kuhusu kulipa watu waliofariki,hivi hii serikali si inahakiki kutokea mwaka jana mwezi wa 5? Kwanini haya matatizo ya kulipa watu hewa bado yapo? Nini maana halisi ya uhakiki kama bado wanalipa bilioni 9 kwa watu hewa?
 
Mwaka 2015 ambao watanzania tulichezewa sana deni la taifa ni 33 trilion, mwaka 2017 mchezo ule wa watanzania kuchezewa sana tunadaiwa 41 trilion. Mmmmh Mbona kwa akili yangu naona kama saiz ndo Watanzania tunachezewa zaid!!! Miaka hiyo ya kuchezewa sana Tanzania tulikuwa tunapewa na ugali kwa bei cheee miaka hii kila kitu bei juu, deni nalo linapanda kwa kasi ya viwonder. MIKONO JUU MWENDO WA MATEKA.
Hii ni hadi june 2016 ikifika june 2017 itakua trillion 50.
 
Back
Top Bottom