Taarifa ya ufafanuzi kwa wakazi wa mkoa wa Iringa juu ya kauli ya mkuu wa mkoa wa Iringa.

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,898
Kuna Video Ikimuonesha Mkuu wa Mkoa wa Iringa Rc Hapi Akihoji Tukio La kuzindua Sera za Chama na hususisha Viongozi wetu wa kutokuoneka Ukerewe Kwenye Ajali Ya MV Nyerere
na Akisema ipo siku ccm Iringa mjini inachukua halmashauri na jimbo

Tunapenda Kumwambia Mkuu huyu Wa Mkoa wa Iringa Moja kuwa Kabla ya kuuliza Viongozi wa Chadema Amuulize Mwenyekiti wake Wa Ccm taifa Pamoja na msiba mzito Kwanini hatukumuona Ukerewe kipindi ambacho kama taifa liliondokewa na watanzania wengi kwa ajali

Pili Mkuu wa mkoa tunapenda kumwambia Kuwa Chadema Tumesikitishwa sana Matukio mbalimbali ya kuwapoteza Watanzania kwa Ajali Za Majini,Kutokana Na chama chake kutokuwa na sera Madhubuti na imara juu ya usafiri wa Majini

Chama makini na Viongozi Makini hawaishii Kuhuzunika ila wanachukua hatua kwa kutunga Sera thabiti zitakazo toa majibu Ya changamoto ya Ajili za Usafiri Wa Majini

Na Ndo Maana Chadema tulifanya uziduzi wa sera ili kuwapa fursa wananchi kujua sera zetu juu ya mambo mbalimbali yanayorikabili taifa

Na Kupitia Sera za Chama Toleo 2018 Chadema Tumepambanua namna tutakavyoboresha usafiri wa Majini Kutoka na changamoto Ya usafiri wa Maji nchini kama inavyosomeka

Chadema itapanua na kuboresha uwezo wa bandari zetu zilizopo ili kukidhi Mahitaji yanayotokana na ukuaji wa biashara na kuongezeka kwa mizigo pamoja na meli za abiria,hii itajumuisha kuendeleza na kuboresha Mfumo wa Usafiri wa Majini wenye ufanisi.

Chadema itahakikisha kuwa inajenga na kuboresha bandari kwa ajili ya mashua za watu binafsi

Chadema itahimiza ushiriki wa Sekta binafsi kwa kuyavutia Mashirika makubwa ya meli kuja kuwekeza Nchini,Pia Chadema Itaboresha na kuendeleza ViVuko vyote kwa ajili ya Kuwaunganisha Wananchi

Pili Mkuu wa Mkoa Amekuja Iringa Amekuwa akikaririwa Sehemu mbalimbali Akisema amekuja Kusafisha iringa,Mara Atahakikisha halmshauri na jimbo 2020 Vinaenda CCM

Tunapenda Kumuuliza Mkuu wa Mkoa hayo ndo majukumu yake yaliyoanishwa na *Sheria ya Tawala za mikoa Na 19 ya Mwaka 1997 kifungu cha 5(1,2,3)*????

Ipi Tofauti yake yeye Kama mkuu wa Mkoa Na Katibu wa ccm mkoa au Mwenyekiti wa ccm Mkoa?? Au ndo Uthibitisho kuwa Viongozi wa CCM mkoa wa Iringa hawana Uwezo wala Ujasiri Wa Kukisemea chama chao??

Tunapenda Kumkumbusha Mkuu wa Mkoa Kuwa Mbunge wa Iringa Mjini Peter simon Msigwa Alichanguliwa na Wananchi na Halmashauri hii Ipo Chadema kwa Ridhaa ya Wananchi na Sio Watakwa ya Mtu binafsi

Kwa Mwenendo Wa Mkuu wa Mkoa kuwaandamana Viongozi wa kuchaguliwa na Wananchi Kupitia CHADEMA na Uthibitisho wa Msemo Usemao

Simple minded politicians think of next election, but great leaders think of next generations.

Wanasiasa wenye fikra finyu huwazia uchaguzi ujao, lakini viongozi bora hufikiria mustakabali wa vizazi vijavyo

Ni kwa jinsi hii, vyama makini na vyenye uongozi bora vitaendelea kujipambanua kwa siasa za sera zaidi, huku vyama uchwara vikijikita kwenye siasa za propaganda, fitina, chuki, ubaguzi na matumizi ya mabavu dhidi ya wapinzani wao.

Jackson Mnyawami
Katibu CHADEMA
Mkoa Wa Iringa
 
Labda nikusaidie kujibu kuwa Mwenyekiti wa CCM Taifa aliwakilishwa na watendaji wengine kama Katibu mkuu na katibu mwenezi. Halafu CCM si mtu bali ni watu, hivyo kutokwenda kwa mwenyekiti hakumaanishi kuwa CCM haijaenda. CCM si chama cha mtu mmoja hadi useme asipotokea huyo mtu basi CCM haipo. Halafu tambua pia katika tukio lile, Mwenyekiti wa CCM hakusimama kama chama, bali alisimama kama serikali. Na serikali iliwakilishwa na Waziri mkuu.
 
Hata CHADEMA iliwakilishwa na watu kule akiwemo Mbunge wa Ukerewe. Wote hamna hoja za maana. Ni vijembe tu vya kisiasa visivyo na maana yoyote. Kwani mlitaka watu waonekane wakiwa na sare za vyama vyao kule msibani?
 
Pumbavu ulimuona Katibu mkuu wa ccm Ukara?
 
Kwa hiyo Chadema ni mtu sio watu ? Ila ccm sio mtu ni watu ? Halafu hapo wewe ndio umejitolea kujibu hoja ?

Sijui mnalishwa nini huko ccm

Salalee!
 
Labda nikusaidie kujibu kuwa Mwenyekiti wa CCM Taifa aliwakilishwa na watendaji wengine kama Katibu mkuu na katibu mwenezi. Halafu CCM si mtu bali ni watu, hivyo kutokwenda kwa mwenyekiti hakumaanishi kuwa CCM haijaenda. CCM si chama cha mtu mmoja hadi useme asipotokea huyo mtu basi CCM haipo. Halafu tambua pia katika tukio lile, Mwenyekiti wa CCM hakusimama kama chama, bali alisimama kama serikali. Na serikali iliwakilishwa na Waziri mkuu.
Unazungumzia CCM ipi hii ya bwana Juma??? Bwana J ndio kila kitu na mbona waliomwakilisha walikuwa wanasema kila baada ya saa alikuwa anawapigia ulishawahi ona wapi uwakilishi wa namna hii.
 
We, kuwa muelewa mwalimu wako alipata shida sana kukuelewesha, hapo anamzungumzia mkuu wa kaya rais, kwann hakuenda? Badala yake tunasoma kwenye mitandao yuko na traffic wanakunywa chai kwa furaha, wakati tukio ni la huzuni? Hawa wa upande wa pili wangeenda wangekamatwa na kuweka ndani kwa uchochezi
Labda nikusaidie kujibu kuwa Mwenyekiti wa CCM Taifa aliwakilishwa na watendaji wengine kama Katibu mkuu na katibu mwenezi. Halafu CCM si mtu bali ni watu, hivyo kutokwenda kwa mwenyekiti hakumaanishi kuwa CCM haijaenda. CCM si chama cha mtu mmoja hadi useme asipotokea huyo mtu basi CCM haipo. Halafu tambua pia katika tukio lile, Mwenyekiti wa CCM hakusimama kama chama, bali alisimama kama serikali. Na serikali iliwakilishwa na Waziri mkuu.
 
Labda nikusaidie kujibu kuwa Mwenyekiti wa CCM Taifa aliwakilishwa na watendaji wengine kama Katibu mkuu na katibu mwenezi. Halafu CCM si mtu bali ni watu, hivyo kutokwenda kwa mwenyekiti hakumaanishi kuwa CCM haijaenda. CCM si chama cha mtu mmoja hadi useme asipotokea huyo mtu basi CCM haipo. Halafu tambua pia katika tukio lile, Mwenyekiti wa CCM hakusimama kama chama, bali alisimama kama serikali. Na serikali iliwakilishwa na Waziri mkuu.
Chadema alikuwepo mbunge na viongozi wa kanda. Tofauti ni nini? Halafu ujue kisiasa na ki nchi yaani kimataifa aliyefiwani rais siyo Mbowe. Rais ndiye baba wa taifa na mfariji mkuu. Ndiyo maana hata salam za pole kutoka nje ya nchi anatumiwa rais siyo viongozi wa upinzani. Sasa tupe jibu rais alikuwa anafanya nini Dsm wakati watoto wake kwa mamia wameangamia ziwani? Hapo nafasi ya baba ikoje? Kwanini awakilishwe? Alikuwa nje ya nchi au alikuwa anaumwa? Je ni halali kumtuma baba mdogo wakati baba mzazi upo na unaonekana eti umetoka kanisani kisha unaenda kunywa chai na traffic! Acheni unafiki wa kutetea hata vilivyo wazi.

Wakati wa tetemeko Kagera rais hakwenda kama kawaida yake. Mbowe na Lowassa walienda. Unajua kilichowatokea? Wakati wa ajali ya wanafunzi 32 Arusha hakwenda as usual. Viongozi wa upinzani wakiwemo wa CHADEMA na wa dini walikwenda kuhani. Unajua kikichowatokea? Walirudi nyumbani wakitokea Lopango! Teteeni vingine siyo hilo mlipaswa kuwa hata na aibu kutetea!
 
Labda nikusaidie kujibu kuwa Mwenyekiti wa CCM Taifa aliwakilishwa na watendaji wengine kama Katibu mkuu na katibu mwenezi. Halafu CCM si mtu bali ni watu, hivyo kutokwenda kwa mwenyekiti hakumaanishi kuwa CCM haijaenda. CCM si chama cha mtu mmoja hadi useme asipotokea huyo mtu basi CCM haipo. Halafu tambua pia katika tukio lile, Mwenyekiti wa CCM hakusimama kama chama, bali alisimama kama serikali. Na serikali iliwakilishwa na Waziri mkuu.
Kwa hiyo tukisema uongozi wa CDM uliwakilishwa na mbunge inaweza kuwa sahihi pia!
 
Mbunge wa Ukerewe hakuwa mwakilishi wa chama, bali mfiwa aliyefiwa na wapiga kura wake.
Kwa Mtazamo haihitaji ata cheti wale shahada;
Wapiga kura wa ukerewe/ukara ni wafuasi wa CHADEMA baada ya muda mrefu kusahaulika katika maendeleo likiwapo tatizo la huduma za usafiri; mitumbwi, karua iliwatesa sana,Kivuko hakikutosha mahitaji yao..kila aliyekata tamaa alihamia chama kingine cha siasa( sipendi neno Upinzani)akitumaini mabadiliko..Matokeo yake ndio huyo Mbunge ambaye anawakilisha CDM.kitu cha msingi CCM kama inataka kiti huko ipeleke maendeleo..sasa sijui humu kelele zinatoka wapi!
 
Hata CHADEMA iliwakilishwa na watu kule akiwemo Mbunge wa Ukerewe. Wote hamna hoja za maana. Ni vijembe tu vya kisiasa visivyo na maana yoyote. Kwani mlitaka watu waonekane wakiwa na sare za vyama vyao kule msibani?
Huyo mbunge si ndo mfiwa mwenyewe?
 
21 Reactions
Reply
Back
Top Bottom