Taarifa ya TANESCO: Katizo la Umeme Ilala

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,495
3,458
hirika la Umeme Tanesco linawataarifu wateja wake wa Mkoa wa Ilala kuwa jana, saa 4 usiku kumetokea hitilafu ya dharura kwenye kituo chake cha kupooza umeme cha Ilala hivyo kusababisha ukosefu wa umeme kwa baadhi ya maeneo ya Kurasini, Kigamboni, Mbagala, Changombe, Nyerere rd.

Mafundi wa karakana ya umeme wanashugulikia tatizo na tunatarajia umeme utarudi saa 10:00 jioni leo.

Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

IMETOLEWA:

OFISI YA UHUSIANO

TANESCO MAKAO MAKUU
 
Afisa uhusiano naona ana hugover ya pesa za escrow.mkoa wa ilala hakuna kurasini,chang'ombe wala kigamboni,
 
Huyu afisa uhusiano labda kaspecialize kwenye mahusiano ya mke NA mume. Huku Kimara,Mbezi mpaka kibamba hakuna umeme NA Wala hajatangaza. #bring back our umeme!
 
sisi wa mbagala charambe leo siku ya pili hakuna umeme,kuhusu chang'ombe leo umeme upo mpaka sasa ninavyoandika.
 
Wadau
Kuna taarifa zipo kwamba IPTL wamezima mitambo yao ya kuzalisha umeme na kusababisha umeme kutokuwepo katika mikoa mbalimbali Tanzania.

Hii inatokana na mwekezaji huyo kufanya maamuzi ya kuondoa mitambo yake na kuipeleka Burundi
IPTL wanatoa 75% ya umeme wa Dar es Salaam
 
Fucck him,hiyo mitambo ni nuksi imetutesa sana bora iondoke nchini
 
Wadau
kuna taarifa zipo kwamba iptl wamezima mitambo yao ya Kuzalisha umeme na kusababisha umeme kutokuwepo katika mikoa mbalimbali Tanzania.
Hii inatokana na mwekezaji huyo kufanya maamuzi ya kuondoa mitambo yake na kuipeleka Burundi
IPTL wanatoa 75% ya umeme Wa dar es salaam
iptl sio baba wala mama yetu,hata hivyo wakizima ndio tutapata akili yetu na mbinu zetu wenyewe!
 
Wadau
kuna taarifa zipo kwamba iptl wamezima mitambo yao ya Kuzalisha umeme na kusababisha umeme kutokuwepo katika mikoa mbalimbali Tanzania.
Hii inatokana na mwekezaji huyo kufanya maamuzi ya kuondoa mitambo yake na kuipeleka Burundi
IPTL wanatoa 75% ya umeme Wa dar es salaam

inabidi iwe angani isikae ardhini kubana nafasi yetu.
 
Ndio Mida mzuri kwa serikali kuichukua kabisa NA kuibadili itumie gas
 
Bora tuishi kwenye giza kuliko kudili na uhanithi wao. Wapeleke huko Burundi na ------- wote wliohusika tuwahamishie Burundi ---- ya mama zao na utashangaa Burundi watachajiwa bei ndogo kuliko sisi.
 
Afadhali labda watanzania watazinduka usingizizini na kujua ccm ni janga
 
kwanini asipatiwe leseni asambaze umeme sambamba na tanesco? jamani dili likibuma msilazimishe.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom