Taarifa ya SSRA kuhusu Fao la Kujitoa

mpiga domo

JF-Expert Member
Apr 30, 2013
852
1,505
Habari wanabodi,

Hii ni taarifa ilipo kwenye website ya SSRA kuhusu fao la kujitoa.

6d37fe8cb1f5f19ef4d370b7dddff53b.jpg
 
Sijaelewa,mbona sijaona kitu cha kuelewek
Ndio nini hii sasa..,, dah nchi ngumu hii.
Kama kawaida kunapokuwa na jambo lenye utata hata kauli za taasisi za serikali huwa zina utata alafu mwisho wa siku zinakuja kutolewa ufafanuzi kwamba nilinukuliwa vibaya. Hapo mtu mwingine akisoma ataelewa "fao la kujitoa limeondolewa" alafu mwingine yaani hata mie nimeelewa kwamba "kwa sasa fao la kujitoa liendelee wakati taratibu za marekebisho ya sheria ukiendelea".

Btw nikiona habari inayojadili issue za fao la kujitoa mapigo ya moyo yanakwenda kwa kasi haswa
 
Hii barua inautata zaidi ya utata wa mifuko ya hifadhi ya jamii inavyojikanganya kuhusu fao la kujitoa.
 
Serikali hata mkipitisha na kurekebisha sheria .,kufanya figisu ili kumdhulumu MTU mafao yake ni unyan`ganyi kama ilivyo kwa majambazi kutumia silaha.sijawaji ona serikali kuwa nyan`ganyi ,only in Tanzania it may happen. Shame on you.
 
Yaani kabisa kurugenzi ya mawasiliano inaandika kitu kisichoeleweka kama hiki?
Habari ilikuwa tata na taarifa ilibidi iende kiundani badala yake haitoi ufafanuzi.Hawajamaliza warudie tena wakaandike upya.
 
walikifanya hawa nikutoa habari jinsi ilivyo mtaani hakuna jingine sijaona wakiongelea kutjitoa sijaona wakiongelea kuondoa kipengele cha kujitoa au printer zao zina wino wakutosha na karatasi nyingi hazikazi..
 
Kunakila sababu wananchi wanchi hii kuipindua serikali yao,kikubwa niutayari wao tu wengi tumefunikwa na utando wasisi masikini tu hatuna lakufanya
 
Hela ya makato yanazuiliwa bila idhini ya mkatwaji, tambueni kwamba serekali nyingi za Afrika vyombo vyake haviko huru, na viongozi wake kutokana na elimu ya kiukandamizaji tuliyopata ndio maana hata uwezo wetu wa kufikiria hauko huru,
wenye maamuzi ya mwisho ni wakatwaji ila utaona kwamba serekali inatumia hizo fedha kwenye miradi bila indini.
na niutumwa ambao unatakiwa ukataliwe kwa nguvu zote! La kujiuliza ni nani mwenye nia ya kweli kufanya hivyo?
Mwanasiasa hawezi kukusaidia kwa hili....
Tunatakiwa tuwe na viongozi wenye mawazo huru,,
Na tujielekeze kwenye ajira binafsi ambazo zinakupa uhuru zaidi.
 
Eti muwe watulivu wakati tunalitafutia ufumbuzi suala hili, kazi sina, nimeshindwa kulipa ada za watoto kwa sababu ya kuporwa fao langu la kujitoa halafu anakuja mtu na kusema Uwe mtulivu, hawa ssra ni wametumwa sio bure
 
Hiyo taarifa ina changanya zaidi kuliko kutoa ufafanuzi, inawezakana wanataka kuiambia uma kuwa katika hayo mabadiliko yaliyofanyika kipengele cha fao la kujitoa haikuguswa, kwahiyo kila mfuko inaendelea na utaratibu wake juu ya fao la kujitoa.
Tatizo ni kuwa wale walioko serikali wanachukulia fao la kujitoa kama tatizo la Private sector employees na sio tatizo la wafanyakazi wote ktika nchi hii, bila umoja taarifa km hizi tutazisoma sana.
 
Wafanyakazi wa Tanzania wapo busy wanaangalia series ya madawa. Wakija kushtuka imekula kwao.
 
Back
Top Bottom