Taarifa ya Prof. Lipumba kwa vyombo vya Habari kuhusu CAG na ukaguzi wa Tegeta Escrow Account

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
12,258
2,000
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI, 23 Novemba 2014

Katika Kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2000 na 2005 nilitumia muda mwingi kuelezea rushwa inayohusiana na mkataba wa TANESCO na IPTL. Kwa bahati mbaya hoja zangu hazikupewa uzito na vyombo vya habari.

Wakati Tanzania inaelekea kwenye uchaguzi Mkuu, Serikali ya CCM imewawekea fursa wapambe wake kujichotea fedha za umma kupitia fedha zilizowekwa katika akaunti maalum ya Escrow kwenye Benki Kuu ya Tanzania. Akaunti ya Tegeta Escrow ilianzishwa baada ya Shirika la kufua na kusambaza umeme la Tanzania TANESCO kudai kuwa kampuni binafsi ya kufua umeme ya IPTL imekuwa inaitapeli TANESCO kwa kuitoza Capacity Charge kubwa kuliko makubaliano yaliyoko katika mkataba. Toka imeanzishwa kampuni ya IPTL imekuwa mzigo mzito kwa TANESCO na watumiaji umeme wa Tanzania kwa sababu ya kuilipa capacity charge kubwa na mashine zake zinatumia mafuta mazito kufua umeme. Mafuta mazito yana bei kubwa zaidi ya mara mbili ya gharama za gesi.

UKAGUZI WA MDHIBITI NA MKAGUZI WA HESABU ZA SERIKALI (CAG)

Ukaguzi wa CAG wa akaunti Tegeta Escrow umebainisha kuwa TANESCO ililipa capacity charges zaidi ya kiwango kinachotakiwa kulipwa. TANESCO walipaswa kurejeshewa tshs 321 bilioni zilizolipwa ziada kwa IPTL kati ya mwaka 2002 - 2012. Kwa hiyo fedha zote za akaunti ya Escrow jumla ya tshs 306 bilioni ni mali ya Tanesco na bado wanaidai IPTL shilingi bilioni 15.

Kampuni ya Pan-Africa Power Tanzania Ltd (PAP) haikununua kihalali asilimia 70 ya hisa za kampuni ya Mechmar katika IPTL kwani zilizuiwa na mahakama na PAP hawana hati halisi za hisa hizo ( share certificates). Pia PAP ilifanya udanganyifu mkubwa katika malipo ya kodi kwa kutoa nyaraka za uwongo kuwa walinunua hisa kwa tshs 6m badala dola 20m na kuikosesha Serikali Mapato ya tshs 8.7 bilioni. Kosa hili linahusu pia mamlaka ya TRA Ilala ambao walihusika katika kupokea kodi ya mauzo hayo.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali alivunja sheria kwa kuelekeza kuwa kodi ya ongezeko la thamani kwenye capacity charges isilipwe na kupelekea Serikali kupoteza mapato ya tshs 21 bilioni.
Waziri kwa kushirikiana na Katibu mkuu Wizara ya Nishati na Madini hawakufanya uhakiki (due diligence) kuhusu uhalali wa umiliki wa kampuni ya IPTL. Katibu Mkuu alisaini kutoa fedha za escrow bila ya kuhakikisha fedha za TANESCO zinarudi na hivyo kupelekea kulipotezea Shirika zaidi ya tshs 321 bilioni.

Mkurugenzi wa Tanesco na Bodi ya Shirika la TANESCO haikutimiza wajibu wake wa kulinda maslahi ya shirika wanaloliongoza na kugeuza maamuzi yake yenyewe ( ama kwa kushinikizwa na Wizara au kwa rushwa) na kulikosesha Shirika shilingi bilioni 321.

Waziri Mkuu ambaye ndiye Kiongozi wa Serikali Bungeni na Msemaji Mkuu alilipotosha Bunge aliposema bungeni mwezi Mei kuwa fedha hizo sio za umma isipokuwa kodi.

James Rugemalira wa VIP Engineering and Management (VIPEM) na Harbinder Singh Sethi, wa Pan African Power (PAP) kwa kushirikiana na viongozi wa serikali wameitapeli na kuibia serikali fedha zote zilizochukuliwa toka akaunti ya Tegeta Escrow.

HATUA ZA KUCHUKUA

CUF inaitaka serikali kupitia TAKUKURU kuwakamata James Rugemalira na Harbinder Singh Sethi na kuwafungulia mashtaka ya rushwa na wizi wa mali ya TANESCO. TAKUKURU isifanye ajizi kama ilivyokuwa katika kesi ya Rada ambapo walimpeleka Sailesh Vithlani Mahakamani baada ya yeye kutoroka nchini. Hatuna uhakika kama Harbinder Singh Sethi bado yuko nchini.

Akaunti zilizopokea fedha ya Tegeta Escrow zisimamishwe (freeze). Fedha iliyobakia kama bado ipo isichukuliwe.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Werema, Waziri wa Madini na Nishati Prof. Sospeter Muhongo, Katibu Mkuu wa Waziri wa Madini na Nishati E. C. Maswi wajiuzulu au kufukuzwa mara moja.

TAKUKURU iwachunguze kama wamehusika na rushwa katika kuwezesha PAP kuchukua fedha za Akaunti ya Tegeta Escrow.

Ni wazi Benki Kuu ilikuwa na wasiwasi kuwa fedha za Tegeta Escrow zilikuwa zinachukuliwa kinyume cha utaratibu. Bila shaka Gavana alimjulisha Rais Jakaya Kikwete. Je Rais Kikwete alichukua hatua gani? Rais Kikwete aueleze umma kwa nini serikali yake ilishindwa kuzuia fedha za Tegeta Escrow zisiporwe wakati Benki Kuu ilionyesha wazi wasiwasi wake kuhusu uhalalali wa kuhamisha fedha hizo.

Sakata la Tegeta Escrow Account linaonyesha umuhimu wa Bunge kuisimamia serikali na Wabunge kutokuwa Mawaziri kama ilivyopendekezwa katika Rasimu ya Katiba na kuondolewa kwenye Katiba Inayopendekezwa. Waziri Mkuu amekuwa anatafuta kisingizio cha kuzuia mjadala wa taarifa ya CAG ndani ya Bunge.

Rasimu ya Katiba ilipendekeza zawadi za viongozi zirejeshwe serikalini. Taarifa ya vigogo wengi kupewa fedha toka akaunti inayomilikiwa na James Rugemarila inaonesha umuhimu wa kifungu hiki kilichomo katika Rasimu ya Katiba. Katiba Inayopendekezwa iliyoandaliwa chini ya uongozi wa Andrew Chenge imenyofoa kifungu hiki.

Baada ya mjadala ndani ya Bunge kukamilika CUF kwa kushirikiana na wadau wengine tutaandaa maandamano makubwa kulaani vtendo vya kifisadi kuhusiana na akaunti ya Tegeta Escrol na kuwapongeza Wabunge walioibua hoja hii na PAC mpaka kufikia CAG kufanya ukaguzi wa akaunti hii.

Viongozi wa serikali kushiriki kuihujumu TANESCO kunaonesha jinsi CCM kimekuwa Chama Cha Mafisadi kisichokuwa na hata chembe ndogo ya uzalendo. Nchi yetu inahitaji mabadiliko na uongozi thabiti wenye utashi wa kisiasa wa kupambana na rushwa na mafisadi bila woga. Uongozi utakaouhamasisha na kuushirikisha umma katika vita dhidi ya mafisadi. La sivyo Tanzania itakuwa na dola iliyofeli (A Failed State).

HAKI SAWA KWA WOTE

Ibrahim Haruna Lipumba
Mwenyekiti,
Jumapili, 23 Novemba 2014.
 
gsu

JF-Expert Member
Apr 28, 2014
3,463
1,225
Lipumba angeenda kulima matikiti maji tabora kichwa chake kimefikia mwisho kufikiri.
 
Kimbunga

Platinum Member
Oct 4, 2007
14,361

Tutashuhudia sana matamko mwaka huu! Hili ni tamko la CUF, litakuja tamko la NLD, tamko la CHADEMA, etc kisha tamko la UKAWA.

Mkuu Lipumba hivi report imesemaje? Wengine hatujaiona lakini huku site watu wanasema kuna viongozi wengi wamejinyakulia mabulungutu toka kwa James Rugemalira; hawa ni pamoja na makasisi, wabunge, mawaziri (zaidi ya nishati), viongozi wa vyama vya siasa, majaji, watumishi waandamizi wa serikali, etc. Hao nao unawatolea tamko gani?

namanyele

JF-Expert Member
Oct 19, 2012
1,855
1,250
Lipumba angeenda kulima matikiti maji tabora kichwa chake kimefikia mwisho kufikiri.
Ndiyo tatizo la kutumia kijambio kufikiri, sasa hapo Lipumba amekosea nini wewe mwehu ?, Mmepewa ubongo muweze kuchambua mambo wewe unaenda kutumia nyuma kufikiria
 
respect wa boda

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
4,536
2,000
Yeyote Mwana UKAWA anayetoa matamko bila kuihusisha UKAWA iwe kwa Maandishi wala kwa kauli nitamdharau sana Lipumba,.... Watch out.!!!

BACK TANGANYIKA
 
Vyamavingi

JF-Expert Member
Oct 3, 2014
5,072
2,000
Lipumba angeenda kulima matikiti maji tabora kichwa chake kimefikia mwisho kufikiri.
Hebu lete hoja zako dhidi ya hoja za Lipumba ili tuone kati yako na Lipumba nani kichwa chake kimefikia mwisho wa kufikiri.

Vv
 
Joel

JF-Expert Member
Sep 1, 2007
965
500
hapa ndipo ambapo huwa siwaelewi wanasiasa wa tz.huyo singasinga na JR washitakiwe but Pinda,Werema,Maswi,Muhongo na wengineo wajiuzulu au wafukuzwe!!!!! kwa mtindo huu basi ufisadi wa namna hii hautakwisha tanzania. Inatakiwa wote waliohusika ambao ni watumishi wa umma wachukuliwe hatua kali stahiki ikiwemo kushtakiwa na kufilisiwa mali zao,sio kuwaacha wajiuzulu tu nafasi zao.
 
Dj faster

Member
Sep 8, 2014
70
0
Lipumba angeenda kulima matikiti maji tabora kichwa chake kimefikia mwisho kufikiri.
You seems to be TOO LOW.
You have to attack on hand issue rather than attacking a personality of the one who has brought it.

Very pathetic young kid!!!!!!
 
Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
3,162
2,000

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda

Chama cha Wananchi (CUF) kimemtaka Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kujiuzulu kwa kupotosha umma kuhusu fedha zaidi ya Sh. bilioni 300 zilizochotwa katika akaunti ya Tegeta Escrow ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Kauli hiyo ilitolewa jana na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, jijini Dar es Salaam wakati akitoa taarifa kuhusu sakata hilo lililotokana na mkataba wa kuuziana umeme wa dharura kati ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na Independent Power Tanzania Limited (IPTL).

Alisema kuwa Waziri Mkuu ndiye kiongozi wa Serikali bungeni ambaye Mei mwaka huu aliuopotosha umma kwa kueleza kuwa fedha za Escrow zilizoibwa si za umma bali ni za wanahisa.

"Tunamtaka Waziri Mkuu awajibike kwa kitendo cha kupotosha umma, alichokifanya, kama asipojiuzulu inabidi afukuzwe kazi mara moja, amekuwa akitafuta visingizio vya kuzuia mjadala wa taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) ndani ya Bunge ," alisema Lipumba.

"Uwajibikaji pia umewalenga Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema, Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo na Katibu Mkuu wake, Eliakim Msawi, hawa wote wanatakiwa kuungana na Pinda kuachia ngazi," alisema.

Aidha, alisema Serikali kupitia Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) iwatie hatiani wamiliki wa IPTL na kuwafungulia mashtaka ya rushwa na wizi wa mali ya Tanesco huku akisisitiza isifanyike ajizi kama ilivyokuwa katika kashfa ya ununuzi wa rada ambapo wakala, Saileth Vithlani, alipelekwa mahakamani na baadaye akatoroka nchini.

Aliongeza kuwa sakata hilo limeonyesha wazi umuhimu wa Bunge kusimamia serikali na wabunge kutokuwa mawaziri kama ilivyopendekezwa katika Rasimu ya Katiba ya Tume ya Jaji warioba, lakini baadaye mapendekezo hayo yaliondolewa na Bunge Maalum la Katiba (BMK).

Alisisitiza rasimu ya Warioba ilipendekeza zawadi za viongozi zirejeshwe serikalini, lakini taarifa za vigogo wengi kupewa fedha toka akaunti ya mmoja wa wanahisa wa IPTL zimeonyesha umuhimu wa mapendekezo ya Warioba yaliyonyofolewa na Mwenyekkiti wa Kamati ya Uandishi, Andrew Chenge.

Alifafanua baada ya mjadala wa Bunge kukamilika CUF kwa kushirikiana na wadau wengine kitaandaa maandamano makubwa ya kulaani vitendo vya kifisadi kuhusiana na akaunti hiyo na kuwapongeza wabunge walioibua hoja na Kamati ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali (PAC) hali iliyopelekea CAG kufanya ukaguzi.

Chanzo: Nipashe
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom