Taarifa ya Ofisi ya Mbunge wa Kigamboni, Dkt Faustine Ndugulile kwa mwezi April,2021

PendoLyimo

JF-Expert Member
Sep 30, 2014
877
955
TAARIFA YA OFISI YA MBUNGE WA KIGAMBONI KWA MWEZI APRILI, 2021

Mbunge wa Kigamboni Dkt Faustine Ndugulile (Mb) atakuwa na utaratibu wa kutoa taarifa za kila mwezi kwa lengo la kuhabarisha umma kazi zinazofanyika Jimboni.

Kwa mwezi mzima wa Aprili, 2021 Dkt Ndugulile amekuwa Bungeni Jijini Dodoma kushiriki vikao vya Bajeti ya Serikali.

Pamoja na majukumu hayo Mbunge aliweza kufanya ukaguzi wa miundombinu ya barabara ya Barabara ya Tarura na Tanroads katika kata za Mjimwema, Kibada na Somangila mnamo tarehe 9 Aprili. Tarehe hiyo hiyo Mhe Mbunge alikuwa Mgeni Rasmi katika tamasha la wajasiriamali lililofanyika Mjimwema.

Aidha, katika kusukuma maendeleo ya Wilaya ya Kigamboni, Mhe Mbunge amewezesha kufanikisha upatikanaji wa fedha kwa ajili ya miradi ifuatayo:

1. Upatikanaji wa Tsh 20 Milioni kwa ujenzi wa chumba cha kompyuta Shule ya Sekondari ya Pembamnazi.
Huko nyuma, Mhe Mbunge amewezesha kuanzishwa kwa maabara za kompyuta katika shule za Sekondari Kimbiji na Kisarawe II.

2. Upatikanaji wa Tsh 30 Milioni toka CRDB kwa ajili ya ujenzi wa Shule mpya ya Msingi Geuzaulole.

3. Upatikanaji wa Tsh 10 Milioni toka Benki ya Posta kwa ajili ya kutengeneza madawati.

4. Kuwezesha kupatikana kutoka Serikali Kuu Tsh 601,600,000 kwa ajili ya ujenzi wa mabweni, madarasa, maabara na vyoo katika Manispaa ya Kigamboni.

5. Kufanikisha kupatikana kwa Tsh 150 Milioni toka Serikali Kuu kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati za Kijaka, Mwasonga na Buyuni.

6. Kuwezesha upatikanaji wa mabati 250 toka Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) yenye thamani ya Tsh 5 Milioni kwa ajili ya kuezeka madarasa ya shule za msingi.

Hivyo, katika mwezi huu wa Aprili, 2021 Wilaya ya Kigamboni imeweza kupokea Tsh 816,600,000 kwa ajili ya miradi mbali mbali kupitia jitihada za Mhe Mbunge.

Imetolewa na:

Ofisi ya Mbunge wa Kigamboni


IMG_20210502_123818_810.jpg
 
mheshimiwa ndungulile ni member mwenzangu wa JF tokea miaka ile na ni member active na uzuri PM yake anakujibu fasta ningefurahi kama ungedeclare interest au angalau taarifa hii aiseme yeye mwenyewe..ili wakati wa matokeo tumuhoji yeye
 
Kuna kazi kubwa ameifanya mbona hajaiandika hapa au anadhani tumesahau? Tumsaidie;
1.Kutunga kanuni za kifashisti zilizopelekea gharama za vifurushi vya mitandao kupaa mara 2-3 ya alivypvikuta wakati anaapishwa kuwa Waziri.
Sawa kabisa...
 
Huyu mbunge ni bure kabisa hana msaada na waTanganyika masikini kapandisha bei ya vifurushi balaa.
 
Mbona anaweweseka au anahisi makonda atarudi?et amesaidia kupatikana 601m kutoka serikali kuu,af na serikali kuu nayo itajisifu kua imetoa 601m kwenda manispaa ya kigamboni ilimradi sifa sifa tu,CCM bana
 
Back
Top Bottom