Taarifa ya NIDA: Ufafanunuzi wa malipo ya watumishi 597 waliochishwa kazi

Mar 26, 2016
21
7
TAARIFA YA NIDA KWA VYOMBO VYA HABARI
IMG-20160527-WA0007.jpg
IMG-20160527-WA0008.jpg
IMG-20160527-WA0008.jpg
IMG-20160527-WA0008.jpg
 

Attachments

  • TAARIFA UMMA 27052016 - 0001.pdf
    661.4 KB · Views: 76
  • TAARIFA UMMA FRONT PG - 27052016 - 0001.pdf
    699.5 KB · Views: 39
Serikali ilishatoa hadi na siku za kuwalipa kumbe walidanganywa? Urasimu katika nchi hii sijui utaisha lini, watu wenyewe walisimamishwa ghafla malipo yao wanazungushwa hii nchi nani wa kumkimbilia???
 
Wawalipe mafao yao, waache kuwazungusha.. Na kwanini kabla ya kuwaachisha wasingewatayarishia mafao yao kabisa ili walipotangaza tu kusitisha ajira na mikataba yao wangewalipa hayo mafao..?
 
bongo kila kitu magumashi....

unaweza kuta kuna watu hawana mikataba wamwjipachika nida kiujanja na wanadai mafao yao na mishahara...

wakiambiwa walete mikataba wanadai imepotea..

mtu hana barua ya kuanza kazi au kuachishwa kazi na bado mkataba hana... unaanzia wapi kumpa mafao au mshahara??

ghost worker kila sehem hii nchi
 
Wakati Serikali ya JPM imeipatia NIDA Bl.2.3 kuwalipa wafanyakazi 597 walio katishwa ajira zao mapema March,Uchunguzi umebaini wote tangu wameajiriwa,NIDA haijawahi kulipa makato ya Huduma za Kijamii kama Bima,na huduma nyingine,pia watumishi hao walikatwa Tozo la thamani yaani VAT lakini hazikuwakilishwa TRA hata kufikia Zaidi ya Milioni 800,Mikataba yao mingi inautata na wengi wao hawana majalada kazini,Kuna ile Tabia ya Watumishi kudharau kujisajili asubuhi uingiapo na kutoka kazini wapo wadai hawana vielelezo muhimu Kunawasiwasi baadhi ya Watumishi wanaoidai NIDA kuondoka bila Pesa ama kudaiwa na NIDA,anafafanua Kaimu mkurugenzi Mkuu Dr. Modestus Kipilimba
 

Attachments

  • TAARIFA UMMA FRONT PG - 27052016 - 0001.pdf
    699.5 KB · Views: 72
  • TAARIFA UMMA 27052016 - 0001.pdf
    661.4 KB · Views: 77
SERIKALI imeipatia Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Shilingi Billioni 2.3 (Bilioni mbili na milioni mia tatu) kwa ajili ya kuwalipa waliokuwa watumishi wa muda wa mamlaka hiyo, wapatao 597, waliosimamishwa kazi hivi karibuni.


Malipo hayo yanahusisha mishahara yao ya miezi minne, ukiwemo mshahara wa mwezi mmoja wa notisi ya kusimamishwa kazi, pamoja na malimbikizo ya madeni yao katika mifuko ya hifadhi ya jamii.


Kabla ya NIDA kuwalipa watumishi hao fedha hizo, Wizara ya Fedha na Mipango iliamua kufanya uhakiki ili kujiridhisha kama madai hayo yalikuwa sahihi.


Uhakiki huo ulihusisha mahojiano ya ana kwa ana na watumishi hao pamoja na kupitia nyaraka mbalimbali zikiwemo majalada, mikataba ya ajira, madaftari ya mahudhurio, taarifa za kazi za kila siku na namba zao za akaunti za benki zilizokuwa zikitumika kulipa mishahara.


Katika uhakiki huo imebainika kuwa kulikuwa na kasoro ama changamoto kadhaa zikiwemo za kimikataba kati ya NIDA na watumishi hao.


Wakati wa zoezi hilo, jumla ya watumishi 597 walipaswa kuhakikiwa lakini majina ya watumishi yaliyowasilishwa kuhakikiwa ana kwa ana kutoka NIDA, Tanzania bara yalikuwa 565.


Hata hivyo, watumishi 516 pekee ndio waliojitokeza katika zoezi hilo na wengine 49 hawakujitokeza.


Watumishi wa muda 32 kutoka NIDA Tanzania Zanzibar, wanaofanya jumla ya watumishi wa Mamlaka hiyo waliosimamishwa kazi kufikia 597, walihakikiwa kwa kupitia majalada yao yaliyoko ofisi za NIDA Makao Makuu, na kubaini mikataba yao haikuwa na kasoro.


Kwa mantiki hiyo watumishi 427 kutoka Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar ndio waliokidhi vigezo vya kulipwa stahili zao za kuachishwa kazi.


Aidha, watumishi wengine 121, walibainika kuwa na kasoro mbalimbali ambazo zinapaswa kurekebishwa na Menejimenti ya NIDA kabla ya kufanya malipo hayo.


Baadhi ya kasoro zilizobainika katika uhakiki huo ni pamoja na kukosekana kwa mikataba na majalada yao katika Ofisi ya mwajiri, kukosekana majina yao kwenye daftari la mahudhurio kazini, kuwa na utata kwenye mikataba (kutofautiana tarehe na sahihi za wahusika), kufanana kwa namba za majarada, na kukosekana kwa barua za kusitishwa kazi.


Wizara ya Fedha na Mipango imemaliza kazi yake ya uhakiki na kwamba jukumu la kuwalipa watumishi wa NIDA wanaostahili limeachwa mikononi mwa menejimenti ya NIDA.


Imetolewa na:

Benny Mwaipaja

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO


13 Mei, 2016
 
Kapilimba mbona kauli yako inatofautiana na Benny mwaipaja kutokana na tangazo lao apo juu ambapo wanasema wameshamaliza na wamekupa hela kulipa?
Mbona sarakasi zimekuwa nyingi hivyo?
 
kama kawaida hapo kuna watumishi hewa wengine hii ndio ilikuwa serikali ya awamu ya nne kila mwajili alikuwa anaamua anavyofikiri yeye
 
Ni ajabu serekali hii inayojiita inatetea wanyonge kumbe ndio kwanza inaendelea kuwakandamiza bila huruma. Hili linasikitisha sana.
 
Back
Top Bottom