Taarifa ya Mwaka:Miaka 3 Baadaye... Asanteni!

Mzee Mwana Kijiji
Mimi naishi mikoa ya pembezoni lakini kila jumanne asubuhi kazi ya kwanza ni kupokea cheche kutawanya kwa wateja wangu wapatao 13. Hao nao wana wateja wao kadhaa. Niliamua kuona kama kinasomwa, nikapokea na kuchelewa kutawanya hadi alhamisi. Nilisumbuliwa kwa simu siku nzima kuombwa nifuatilie. Wacha nijizolee sifa kuwa mimi ndiye mtengenezaji wa Cheche. Nayasema haya kukupongeza.

Ni Wako Bendera anayefuata Upepo.
 
Mzee Mwana Kijiji
Mimi naishi mikoa ya pembezoni lakini kila jumanne asubuhi kazi ya kwanza ni kupokea cheche kutawanya kwa wateja wangu wapatao 13. Hao nao wana wateja wao kadhaa. Niliamua kuona kama kinasomwa, nikapokea na kuchelewa kutawanya hadi alhamisi. Nilisumbuliwa kwa simu siku nzima kuombwa nifuatilie. Wacha nijizolee sifa kuwa mimi ndiye mtengenezaji wa Cheche. Nayasema haya kukupongeza.

Ni Wako Bendera anayefuata Upepo.

Nawe unastaihili sifa hizo kwa kusaidia kazi hii njema
 
Ndugu zangu
Niwape neno la Tumaini. JF ni chombo mahiri cha mabadiliko. Serikali inakiogopa kama ukoma. Kazi za JF ni agenda ya kudumu kwenye vikao vya cabinet. Kama kuna mjumbe wa Cabinet abishe na asiogope maana kwa vyovyote anatumia jina bandia.
Maasimu serikalini wanatishiana kwa kutumia JF. Kimsingi JF imeongeza chachu ya check and balance katika mfumo wetu wa utawala. Japo Mwana Kijiji katika taarifa ameliongelea hili, lakini nilitamani aseme zaidi kwa kusema "JF can stand and be counted" miongoni mwa wanaosemwa kuwa na nia njema na taifa letu.

Nina wasiwasi kidogo na mnivumilie kwa hilo, kuwa mwelekeo wa mazungumzo na serikali usiende haraka kwa sababu, "Mgandamizaji wako wa jana hawezi kamwe kuwa mkombozi wako wa leo". Kwa kifupi, watendaji wala serikali, wasituzoee hata kama wanatupa breaking newz. System ya nchi ni chafu mno, ukikaribiana nayo utachafuka. Naona wengi wanaanza kumshtukia Zitto. Nadhani ni kwa sababu hiyo.

Huwa nawaambia watu wanaonihoji kwa nini siiungi mkono CCM, nami huwajibu kuwa, nasubiri CCM kiwe chama cha upinzani ndipo niwaunge mkono kwa sababu katika taifa letu, ni kazi tukufu kuupinga mfumo unaotawala kwa usalama wa nchi na amani yake.

Wasalaam
Bendera Afuataye Upepo
 
MM,

Kazi yako si tu huwa inanisisimua lakini pia inanishurutisha ni nitoe mchango wangu katika haya mapambano, ambayo ushindi uko katika mikono yetu. Tuko pamoja kwenye CHECHE, nitaongeza usambazaji. Na nitalete picha, za mahali nipolibandika huko mikoani.

Tafadhali naomba mipango ya tamasha la UK, nipo tayari kusaidia kwa hali na mali ili lifanikiwe.

Utatu.
 
Nashukuru wote kwa ujumla wenu.

Mara nyingi (kama siyo zote) ni marafiki na maadui ndiyo wananoa dhamira njema ya mtu. Mahali fulani katika vitabu vitakatifu imeandikwa kuwa "chuma hunoa chuma, ndivyo mtu aunoavyo uso wa rafiki yake". Shukrani ya pekee sana inawaendea wale wote ambao wamekuwa chuma kutunoa kwa ukosoaji wa aina yoyote (hata ule wenye msingi wa chuki au kisasi) kwani kwa kufanya hivyo wanatulazimisha kujipima na kujichunguza dhamira zetu.

Na pia shukrani nyingi na kubwa ni za wale rafiki ambao tulipokuwa tumeangushwa au tumewekwa kwenye kona na kuanza kupigwa mangumi hawakusimama pembeni kuangalia matokeo yake (kama tutasimama au tutaanguka) bali walijiingiza katikati na kuwa walinzi na watetezi wetu. Hawa ni marafiki ambao hawakuogopa kuchukua upande hasa ukizingatia kuwa ukichukua upande wa "mwanakijiji" basi unajiweka kwenye kona mbaya sana ya kuangaliwa kwa shuku.

Lakini zaidi pia tunawashukuru wale ambao katika ukimya wa ofisi zao na usiri wa mioyo yao tumekuwa tukiwasiliana nje ya mitandao hii kabisa na majina yao yanabakia vifuani mwetu kama siri. Ni hawa ambao ndiyo wamekuwa waleta habari ambazo na vidokezo vyenye kuifungua serikali mbele ya wananchi, habari ambazo mwanzoni kuzipata kwake ilikuwa ni mbinde. Kwa vile hatuna sheria ya Uhuru wa Kupata Habari kutoka kwa serikali mara nyingi tunalazimika kutumia njia za mkato au watu waliochoshwa wanaamua kuzunguka pembeni. Hawa wanachukua risk ya ajabu kama mtakavyoona kwenye kijarida cha Cheche wiki hii!

Hawa ndiyo mashujaa wasiotajwa majina na vyanzo visivyotambulishwa rasmi. Ni hawa wanasimama kama walinzi wasiolala katika malango ya watawala wetu. Kwao pekee yao ndiyo wameifanya JF na sisi wengine kuonekana tunafanya kitu ingawa ukweli ni kuwa bila ya wao maneno yetu yangekuwa ni mifupa tu isiyo na nyamanyama na mafuta!

Kama tulivyosema kwenye taarifa, kama unataka kushiriki kweli katika kuhamasika pamoja nasi wasiliana nasi na kwa hakika hatutawaangusha. Kwa ndugu yangu Pasco kuhusu suala la kutoa ujiko wa kile ambacho tunataka kufanya (tamasha) nikuhakikishie kuwa kama haitokuwa hivyo tulivyokusudia hatutafanya. Hatutaki kufanya kile kilichowahi kufanywa au kujaribu kile tusichoweza kufanya. Endapo tamasha litakuwa jinsi tunavyolifikiria basi it'll be the best, the biggest and the boldest summer event of the year! It is that or not. Na tunaposema haijawahi kufanyika mahali popote we absolutely mean that.

Watu wameshawahi kuwa na muziki, bbq, ulaji na unywaji n.k ours will be all that and more! (the more part is the one to look for)
 
Back
Top Bottom