Taarifa ya Msimamo wa CDM Juu ya Uteuzi wa Tume ya Mchakato wa Katiba Mpya

Tumaini Makene

JF-Expert Member
Jan 6, 2012
2,642
6,070

TAARIFA KWA UMMA

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinaendelea kuchambua wasifu wa wajumbe walioteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kuwa wajumbe wa tume ya mabadiliko ya katiba.

CHADEMA kitatoa tamko juu ya uteuzi wa tume husika baada ya uchambuzi kukamilika wa kutafakari iwapo uteuzi husika umezingatia matakwa ya umma na dhamira ya kujenga muafaka wa kitaifa wa kuwa na katiba mpya na bora.

Pamoja na kutaja majina ya wajumbe wa tume, CHADEMA kilitarajia kwamba Rais Jakaya Kikwete angeeleza pia ratiba ya kufanyika kwa marekebisho mengine muhimu ya awamu nyingine kuhusu bunge maalum la katiba na hatua ya kutunga katiba mpya na usimamizi wa kura ya maoni itakayowezesha wananchi kufanya maamuzi kwa uhuru na kwa haki kabla ya mchakato kufikia katika hatua husika.

Katika muktadha huo, Kamati Maalum ya Kamati Kuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) iliyoundwa tarehe 20 Novemba 2011 kwa ajili ya kukutana na Rais Jakaya Kikwete kuhusu sheria ya mabadiliko ya katiba ya mwaka 2011; itafanya kikao chake karibuni kupitia taarifa ya uchambuzi unaoendelea kufanywa juu ya uteuzi uliofanyika wa wajumbe wa tume na tamko litatolewa kwa umma kuhusu mchakato huu muhimu kwa maslahi ya taifa.

Itakumbukwa kwamba tarehe 27 na 28 Novemba 2011 Rais Kikwete alifanya mkutano wa siku mbili na viongozi wa CHADEMA kuhusu muswada wa sheria ya mabadiliko ya katiba na pande mbili kukubaliana kuhusu haja ya sheria husika kufanyiwa marekebisho kwa mashauriano na wadau mbalimbali kwa lengo la kudumisha muafaka wa kitaifa kwenye mchakato wa katiba mpya.

Kamati Maalum ya CHADEMA ilikutana tena na Rais tarehe 21 Januari 2012 Ikulu Dar es salaam ambapo kamati hiyo ikiongozwa na Mwenyekiti Freeman Mbowe ilitaarifiwa hatua ambayo ilifikiwa na serikali katika kuanza kuiboresha sheria ya mabadiliko ya katiba ya mwaka 2011 ili ikidhi mahitaji ya kujenga kuaminiana na muafaka wa kitaifa kwa mawasiliano na mashauriano na wadau mbalimbali.

Tarehe 22 Januari 2012 Kamati Kuu ilipokea na kujadili taarifa ya Kamati Maalum kuhusu Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2011 na kujulishwa hatua ambazo serikali ilifikia katika maandalizi ya kuifanyia marekebisho tajwa katika Mkutano wa Sita wa Bunge unaotarajia kuanza tarehe 31 Januari 2012.

Kamati Kuu iliamua kwamba Kamati Maalum iendelee kufanya mawasiliano na mashauriano na Rais Kikwete na Serikali kwa ajili ya kuhakikisha kwamba Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2011 inafanyiwa marekebisho ya msingi kabla ya mchakato wa kukusanya maoni kwa mujibu wa sheria husika haujaanza.

Kamati Maalum ilitakiwa kuendelea kufuatilia utekelezaji wa maazimio matatu ya Kamati Kuu yaliyofikiwa kwenye kikao cha Kamati Kuu ya CHADEMA kuhusu mchakato wa katiba mpya; maudhui ya maazimio hayo ni kama ifuatavyo:

Mosi; “kutoa elimu kwa wananchi na wadau wote juu ya ubovu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na juu ya haja ya kuwa na sheria itakayoweka utaratibu bora zaidi wa kuunda Tume Shirikishi ya Katiba kwa lengo la kukusanya maoni ya wananchi, kuandaa ripoti na Rasimu ya Katiba Mpya, Bunge Maalum la Katiba na usimamizi wa kura ya maoni itakayowezesha wananchi kufanya maamuzi kwa uhuru na kwa haki”.

Pili; “Ushiriki wa CHADEMA katika mchakato mzima wa kupata Katiba Mpya uliowekwa na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba utategemea utayari wa Serikali ya Rais Kikwete kufanya mabadiliko ya kimsingi katika sheria hiyo kwa lengo la kujenga muafaka wa kitaifa juu ya mchakato huo”.

Tatu; “viongozi wote wa chama na wa kuchaguliwa katika ngazi zote kufanya mikutano ya ndani na ya hadhara yenye lengo la kuwaelimisha wananchi juu ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na madhara yake kwa mchakato wa kupata Katiba Mpya na bora kwa nchi yetu kwa lengo la kuunganisha umma wa watanzania kuweza kufanya mabadiliko ya msingi”

Imetolewa tarehe 07 Aprili 2012 na: John Mnyika (Mb)
Mkurugenzi wa Habari na Uenezi
 
Asante kwa taarifa hii, ninanasubiri sana maoni yenu kuhusu hawa walochaguliwa.

Mie sijaridhika nao, sioni mtu mwenye kusimamia anachokiamini kwa hoja.
 
Haya kaka utapata analysis, wala usihofu. Tunapaswa kuwa makini sana Watanzania na kila hatua au kila kinachofanywa na watawala. Asante.
 
Mkuu mimi binafsi kama mwananchi mzalendo ninakubaliana na majina yaliyotajwa kwa upande wa bara'ninaamini hata nyie mtakubaliana na hilo'swala moja ambalo linanitia mashaka ni kwamba hii kamati ikishamaliza kazi itakabidhi kwa mwenyekiti wa ccm ambaye ni rais'na inasemekana anaweza kuikataa au kuikubali''hapo ndio kwenye tatizo na nafikiri mngeangalia jinsi ya kurekebisha kabla hatujafika mbali
 
Ni muhimu wananchi wakawa na imani na wajumbe wa hii kamati na kwa maoni yangu Prof Kabudi ni mgogoro. Sina imani naye kabisa. Msimamo wake alishaanza kuuonesha kupitia TV huko nyuma. Atoe maoni kama mwananchi wa kawaida lakini sio mtu wa kukusanya maoni ya wananchi maana ataacha yale yasiyompendeza mteule wake.
 
nilivyoona orodha ya wajumbe wa tume kuanzia mwenyekiti wake nilichoka na nikajua matokeo yatakuwa ni katiba itakayokuwa inatakiwa na magamba sio wananchi

Warioba ni kada wa ccm kuwa m/kiti sio sahihi kabisa

mbona prof. Issa Shivji ameachwa wakati ni mchambuzi mzuri wa masuala haya

kwa maoni yangu m/kiti alipaswa kuwa mtu neutral, asiyetokana na chama chochote cha siasa, halafu wajumbe wengine wawe ni watu ambao wanaaminika katika jamii

sehemu kubwa ya wajumbe wa tume mm naona ni ccm A na CCM B, hamna watu wanaoweza kuaminika na watz, ikiwa magamba hawataki amani watajbiwa uzuri wa amani na mifumo ya amani ni nini
 
Mimi sijarizika na wajumbe wa upande wa Tanganyika kati ya wajumbe 15; wanne tu ndio waislam kwanini? ina maana Tanganyika inawakilishwa na wakristo tu?
 
Mimi sijarizika na wajumbe wa upande wa Tanganyika kati ya wajumbe 15; wanne tu ndio waislam kwanini? ina maana Tanganyika inawakilishwa na wakristo tu?
Dah!!....

Udini...Udini...Udini!!!..

Na wa Zanzibar/Visiwani je?....Wakristu ni wangapi?....

Ubaguzi wa aina yoyote ile(wa rangi,kabila,ukanda n.k) ni unyama.....Tuuepuke
 
Mimi sijarizika na wajumbe wa upande wa Tanganyika kati ya wajumbe 15; wanne tu ndio waislam kwanini? ina maana Tanganyika inawakilishwa na wakristo tu?

ina maana ulitaka mbake mchakato mzima? Haya katika 32 wakristo 10 waliobaki wote ni mashabiki wa dini,au ndo mambo yenu ya kutaka mambo yenu ya dini tusiyokuwa na manufaa nayo yaendeshwe kwa kodi zetu? Wengi wenu najua ccm mtaihama 2015 mgombea mkristo atakapowekwa. Si mukama ameshawaambia sasa hivi siyo zamu ya wacheza ngoma? Watu mnahamishia ikulu kwenye ngoma za taarabu!!!...sijui mtaanza kukifufua cuf, maana cdm inataka watu wasiopenda mikumbo ya kidini.
 
bange!!!!

Kwanini aisee? kweli nimesikitika sana JK kuchagua viongozi wakuu wa tume wakristo (chair na makamu) wake..hii katiba lazima itakuwa na elements za kikanisa ...bado sijarizika au unaona sawa

Kwanini katika watu 15 wa Tanganyika 4 tu ndio wawe waislam (very unfair representation of muslims in tanganyika)
 
Usinitishe mkuu hata kama chadema, cuf or ccm, itachukua nchi lazima uondokane na sera za udini..

Hii tume kwa upande wa Tanganyika imekaa kidini dini zaidi wajumbe 15 vs 4...hii wangefanyiwa wakristo pasingetosha hapa..nashangaa masheikh wamelala???
 
Topical lazima una kasoro za kimaoni.
Bahati nzuri aliyeunda tume ni muislam
Hii habari ya kuhesabu wakristo na waislam kwenye kila kitu ni dhambi ya kipuuzi lakini ambayo itatugharimu sana
Mnahesabu idadi ya mawaziri kwa misingi ya udini, wakuu wa mikoa na sasa wajumbe wa tume
Huu ni udini wa hatari sana, unapandikiza mbegu za hovyo sana
Leo raisi na makamu waislamu, umeongezwa nini ambacho hukuwa nacho kabla au wakristo wamepungukiwa nini walichokuwa nacho kabla?
Acheni upuuzi huu wa udini
 
Hivi katika nchi hii hamuwezi tazama watu kwa tofauti zao za ki dini, ki kabila hata kwa mara moja tu? SHAME UPON YOU... lakini nisiwalaumu, pengine ni mfumo uliolelea hilo ndio mbovu.
 
Kwanini aisee? kweli nimesikitika sana JK kuchagua viongozi wakuu wa tume wakristo (chair na makamu) wake..hii katiba lazima itakuwa na elements za kikanisa ...bado sijarizika au unaona sawa

Kwanini katika watu 15 wa Tanganyika 4 tu ndio wawe waislam (very unfair representation of muslims in tanganyika)

kubwa jinga tu wewe
 
Usinitishe mkuu hata kama chadema, cuf or ccm, itachukua nchi lazima uondokane na sera za udini..

Hii tume kwa upande wa Tanganyika imekaa kidini dini zaidi wajumbe 15 vs 4...hii wangefanyiwa wakristo pasingetosha hapa..nashangaa masheikh wamelala???

tuweni fair Zanzibar wametoka wakristo wangapi? Si kulalamika tu kuonewa
 
Back
Top Bottom