Taarifa ya msiba:baba mdogo wa rafiki yetu x-pin afariki dunia

Teamo

JF-Expert Member
Jan 9, 2009
12,272
1,034
kwake x-pin ni kama mzazi wake kwasababu ndiye aliyemlea hapa dar.i mean,ndugu x-pin ameanza maisha na amezikamata channel akiwa na huyo mzee.Ndugu x-pin amepata jiko takribani miaka kumi na moja iliyopita kwa support kubwa ya huyu mzee

Ndugu zangu wana jf mlio na mapenzi mema,tusaidiane kumuombea mzee wetu marehemu apewe raha ya milele na kuangaziwa mwanga wa milele....

''RAHA YA MILELE APEWE MZEE WETU,NA MWANGA WA MILELE UMUANGAZIE,APUMZIKE KWA AMANI -AMINA''

msiba huu upo maeneo ya tabata-bima.

kwa sasa hatujajua ratiba zinakwenda vipi,lakini lolote litakalokuwa linaendelea tutafahamishana tu

kwa anayeguswa,naomba awasiliane na mimi kwa pi-emu,au anipigie ili tuongozane kwenda msibani.

ratiba yangu ni kwamba saa tano unusu au saa sita mimi nitakuwa barabarani kuelekea msibani

POLE SANA KAKA YANGU X-PIN
MUNGU AKUPE NGUVU YA KUKABILIANA NA WAKATI HUU MGUMU ULIO NAO
POLE SANA BROTHER!
meet you there
 
Pole sana X-pin mungu awape nguvu faraja na ujasiri katika jambo hili gumu na zito
RIP mzee wetu
Tulitoka mavumbini na mavumbini tutarudi
Jina la bwana libarikiwe
Amen
 
Pole sana X-pin mungu awape nguvu faraja na ujasiri katika jambo hili gumu na zito
RIP mzee wetu
Tulitoka mavumbini na mavumbini tutarudi
Jina la bwana libarikiwe
Amen
ni kweli mama!
sisi sote tu-mavumbi
it hurts a lots loosing the people you love most
 
R.I.P mzee wetu!!! Kuna wazee wengi wa aina hii walileta vijana mjini na kuwalea hadi wakapata maisha, yaani unakuta nyumba enzi hizo imejaa vijana wa jirani kijijini na ndugu na marafiki pia, yaani kule ulikuwa ukisafiri say kuja Dar utasikia shukia kwa fulani, na fulani huyo anawahi stesheni kukupokea asubuhi na mapema anasubiri train liingie!!! Leo hii huu utamaduni upo?? Ni wangapi tumesaidia wakawa na maisha kama sisi au ndiyo tumezidi kujjiwekea ukuta na gate imara na kuachana na traditional (extended family)? Ni kitendawili maana tunabaki kuwa na house boys/girls tu na wengine wanatumaliza kwa kuwa ni wawakilishi wa majambazi wanatumwa tu kujifunza mazingira!!!
 
Jana tulipokea kwa mshituko mkubwa taarifa za msiba za rafiki na ndugu yetu xspin. Mungu akutie Nguvu katika kipindi hichi kigumu na tukumbuke maneno ya mwanamuziki marehemu TUPAC alisema "we should not look death at selfish side" . Tupo pamoja bro.
 
R.I.P mzee wetu!!! Kuna wazee wengi wa aina hii walileta vijana mjini na kuwalea hadi wakapata maisha, yaani unakuta nyumba enzi hizo imejaa vijana wa jirani kijijini na ndugu na marafiki pia, yaani kule ulikuwa ukisafiri say kuja Dar utasikia shukia kwa fulani, na fulani huyo anawahi stesheni kukupokea asubuhi na mapema anasubiri train liingie!!! Leo hii huu utamaduni upo?? Ni wangapi tumesaidia wakawa na maisha kama sisi au ndiyo tumezidi kujjiwekea ukuta na gate imara na kuachana na traditional (extended family)? Ni kitendawili maana tunabaki kuwa na house boys/girls tu na wengine wanatumaliza kwa kuwa ni wawakilishi wa majambazi wanatumwa tu kujifunza mazingira!!!
ni kweli kabisa mkuu maane
WAZEE NI GREASE YA TAIFA
 
ni kweli mama!
sisi sote tu-mavumbi
it hurts a lots loosing the people you love most

Ni kweli Geoff inaumiza sana ..
Mungu wetu ni mwema awape faraja familia yote ya wafiwa ndugu jamaa na marafiki
 
"MSIFADHAIKE mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu niaminini na Mimi; Nyumbani kwa baba yangu kuna makao mengi; la sivyo ningaliwaambia - maana naenda kuwaandalia mahali; Basi Mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo Mimi na Nanyi Muwepo" Yohana 14: 1-3

POLE SANA NA FARIJIKA KWA MANENO HAYA YA MUNGU
 
Pole sana Chrispin

Mwenye Mungu akujalie nguvu wewe pamoja na familia yenu katika kipindi hiki kigumu
 
Pole Xpin , mungu akupe nguvu na subra katika wakti huu mgumu. Na ailaze roho ya baa mdogo mahali pema peponi. Unto Allah we belong and to him is our return.
 
Pole nyingi kwako Xpin na wote wanaohusika na msiba huu.
"Yeye Mwenyezi Mungu ndiye aliyetuumba na Kwake ndio marejeo yaviumbe wote;"
 
Ooh jamani Pole sana Xpin na ndugu na jamaa na marafiki wa Xpin amabo ni membas wa JF.
Bwana alitoa na bwana ametwaa jina la bwana libarikiwe.
 
Kwako X-pin na familia yenu!

Mungu awe nanyi wakataki huu mgumu kwenu; awapatie faraja na amani zaidi ya yote awatie nguvu!

Jina lake libarikiwe!
Amen!
 
POle mpwa Xpin kwa kipindi hiki kigumu, tupo pamoja nawe.
Raha ya milele umpe ebwana.
Pumnzika kwa amani mzee wetu.
 
Pole sana X-pin.

Mungu awape faraja na ujasiri ndugu wote wa wafiwa.

Amen.
 
Pole Sana my Hommie X-pin!! Nawatakia Amani ya Upendo Itawale hapo nyumbani! Mungu awatie nguvu wapendwa wafiwa wote!! Ingawa ki mwili sitakuwepo ila kiroho tupo pamoja wapwa wote! Mwanga wa milele amwangazie Ee Bwana! Pole sana X-pin na familia kwa ujumla!
 
Back
Top Bottom