Taarifa ya Lugumi Yapigwa Kalenda Tena Bungeni

Babu wa Kambo

JF-Expert Member
May 2, 2016
559
808
2.jpg
Ripoti ya sakata la mkataba wa kampuni ya Lugumi Enteprises na Jeshi la Polisi, ambayo ilikuwa iwasilishwe kwenye mkutano unaoendelea wa Bunge, sasa itawasilishwa kwenye mkutano ujao.

Makamu mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Hilary Aeshi alisema ripoti hiyo itaunganishwa katika taarifa za kamati ambazo kwa utaratibu huwasilishwa kwenye mkutano huo.

Sakata hilo linahusisha utekelezaji mbovu wa mkataba wa kufunga mashine za kielektroniki za kuchukulia alama za vidole kwenye vituo 108 vya polisi.

Hadi wakati Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) akifanya ukaguzi wa mkataba huo wa Sh37 bilioni uliosainiwa mwaka 2013, ni vituo 14 tu vilivyokuwa vimefungwa mashine hizo, lakini mzabuni alishalipwa Sh36 bilioni.

Baada ya sakata hilo kuibuliwa, wabunge walitaka liwasilishwe kwenye mkutano unaoendelea mjini Dodoma, lakini PAC ikaunda kamati ndogo ambayo sasa inatakiwa iwasilishe ripoti ya uchunguzi wake.

Hadi jana asubuhi ripoti ya kamati hiyo ndogo, iliyoundwa na wajumbe tisa, ilikuwa bado haijawasilisha ripoti yao.

Hata hivyo, Aeshi ambaye pia ni mbunge wa Sumbawanga Mjini (CCM), alisema alitarajia kukabidhiwa ripoti hiyo na kamati ndogo jana na baada ya hapo kazi ya uchambuzi wa kamati nzima itaanza.
 
Gazeti la Tanzania Daima la leo limeripoti kuwa Ripoti ya Lugumi haitawasilishwa kwenye mkutano wa Bunge unaoendelea Dodoma. Badala yake Ripoti hiyo itawasilishwa kwenye mkutano ujao wa Bunge.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa PAC Hilary Aeshi,Ripoti ya Lugumi imeshakamilika lakini itawasilishwa mkutano ujao kinyume na matarajio ya kuwasilishwa kwenye mkutano huu.
 
May be it need to be doctored first .....................!!
 
hahaha mlipoambiwa kitwanga ameenda israel baada ya kutumbuliwa mlidhani ameenda kutalii?. hahaha na bado amesema atafanya ibada ya SHUKRANI mnafikiri anakwenda kushukuru nn? inshort "LUGUMI IS DEAD"
 
haya sasa ****** wote wa ufipa hamia kwenye SUKARI kwa maana LUGUMI ndo ishapotea hiyo.
 
Hata hili litapita. Tumeshatwanga hela kibao kwenye masakata kibao na yenyewe yalipita kama upepo bila hata kuwatingisha wahusika. Naamini hata hili litapita tu.
 
haya sasa ****** wote wa ufipa hamia kwenye SUKARI kwa maana LUGUMI ndo ishapotea hiyo.
Mtanzania huyu anashangilia wezi waliomwibia kusevu mtego wa kukamatwa.
Nadhani umefika wakati vyuo vyetu vikuu vianzishe shahada ya Bachelor of science in Ubwege kwa watu kama hawa
 
Hii ndiyo ccm ninayo ijua mimi. Wanatujua wantanzania ni watu wa aina gani, we are just like flag flaps where the wind blows. Tumefanya siasa kama ushabiki wa Simba na Yanga, leo hii hata serikali ya ccm ikisigina katiba nitashangilia kwasababu mimi ni ccm.
 
Hii ndiyo ccm ninayo ijua mimi. Wanatujua wantanzania ni watu wa aina gani, we are just like flag flaps where the wind blows. Tumefanya siasa kama ushabiki wa Simba na Yanga, leo hii hata serikali ya ccm ikisigina katiba nitashangilia kwasababu mimi ni ccm.
 
Gazeti la Tanzania Daima la leo limeripoti kuwa Ripoti ya Lugumi haitawasilishwa kwenye mkutano wa Bunge unaoendelea Dodoma. Badala yake Ripoti hiyo itawasilishwa kwenye mkutano ujao wa Bunge.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa PAC Hilary Aeshi,Ripoti ya Lugumi imeshakamilika lakini itawasilishwa mkutano ujao kinyume na matarajio ya kuwasilishwa kwenye mkutano huu.
kikanuni PAC inatakiwa iongozwe na kambi ya upinzani! imekuwaje Aeshi wa CCM awe mwenyekiti?
 
Mtanzania huyu anashangilia wezi waliomwibia kusevu mtego wa kukamatwa.
Nadhani umefika wakati vyuo vyetu vikuu vianzishe shahada ya Bachelor of science in Ubwege kwa watu kama hawa
ww unashangaa bachelor ya ubwege? kwa taarifa yako nina masters of science in ubwege ila sinaga tabia ya KUMKIMBIA MWANAMKE na kuzira.
 
Back
Top Bottom