Taarifa ya Lissu kwa vyombo vya habari kuhusu Spika wa Bunge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Taarifa ya Lissu kwa vyombo vya habari kuhusu Spika wa Bunge

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mpaka Kieleweke, Jun 17, 2011.

 1. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #1
  Jun 17, 2011
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Nawawekea taarifa ya Press Conference ya Mhe.Lissu leo kuhusiana na sakata la mauaji ya polisi Tarime....


  [TABLE="class: MsoNormalTable"]
  [TR]
  [TD="colspan: 3"]
  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  BUNGE LA TANZANIA

  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Simu Na. 026 2322761-5
  Fax Na. (255) 026 2324218
  E-Mail: poctz@parliment.go.tz (Barua zote za kiofisi ziandikwe kwa (Kiongozi wa Upinzani)
  Unapojibu tafadhali taja:
  [/TD]
  [TD="width: 143, bgcolor: transparent"][/TD]
  [TD="width: 315, bgcolor: transparent"] OFISI YA BUNGE
  S.L.P. 941 DODOMA  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  17 Juni, 2011

  SPIKA ANAPENDELEA MAWAZIRI, SERIKALI: ANAKIUKA KANUNI ZA BUNGE!

  TAARIFA KWA UMMA

  Dodoma, Juni 17, 2011

  Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imeelezea kusikitishwa na namna ambavyo Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano amekuwa akishughulikia mijadala ya masuala muhimu kwa umma na ambayo yanaelekea kuibua uozo katika utendaji wa Serikali na watendaji wake wakuu.

  Hii inafuatia uamuzi wa Spika kukataa maswali aliyoulizwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuhusu mauaji ya wananchi wengi wa vijiji vinavyozunguka Mgodi wa Dhahabu wa North Mara katika eneo la Nyamongo wilayani Tarime yaliyofanywa na Jeshi la Polisi, Kanda Maalum ya Polisi ya Tarime na Rorya kwa vipindi tofauti tangu mwaka 2008.

  Maswali hayo yaliulizwa na Mheshimiwa Tundu Lissu (Singida Mashariki, CHADEMA) na Mheshimiwa Esther Matiko (Viti Maalum, CHADEMA) wakati wa Kipindi cha Maswali kwa Waziri Mkuu katika Kikao cha Tisa cha Bunge la Jamhuri siku ya Alhamisi ya tarehe 16 Juni 2011.
  Hata hivyo, katika hatua ya kushangaza, Spika wa Bunge alikataza maswali hayo kujibiwa kwa hoja kwamba yalikuwa yanahusu mambo ambayo tayari yako mahakamani na kwa hiyo kuyajadili Bungeni itakuwa sawa na kuingilia uhuru na mamlaka ya Mahakama kinyume na kanuni 64(1)(c) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, 2007.

  Alipoombwa mwongozo wake kutokana na ukweli kwamba hakuna kesi hata moja ambayo imefunguliwa au inayoendelea katika mahakama yoyote ya Tanzania inayohusu mauaji ya wananchi wa Nyamongo au yanayowahusu polisi wanaohusika na mauaji hayo, Spika Anna Makinda alidai kwamba wauliza maswali wenyewe walikuwa wanakabiliwa na mashtaka ya jinai katika Mahakama ya Wilaya ya Tarime yanayotokana na matukio ya mauaji ya wananchi watano yaliyofanywa na polisi katika eneo la Mgodi wa North Mara tarehe 16 Mei mwaka huu na kwa hiyo hawakupaswa kuuliza maswali yao.


  Akizungumzia uamuzi huo wa Spika Makinda, Mbunge Lissu - ambaye pia ni Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni - alimtuhumu Spika Makinda kwa kumkingia kifua Waziri Mkuu na kukiuka Kanuni za Kudumu za Bunge. "Mimi sijashtakiwa mahakamani kwa kosa lolote linalohusu mauaji ya wananchi wa Nyamongo, Tarime na wala kesi yangu katika Mahakama ya Wilaya ya Tarime haiuhusu matukio ya Nyamongo", Lissu alisema.

  Aliongeza kwamba: "Wakati mauaji ya wananchi wa Nyamongo yalifanywa na Jeshi la Polisi tarehe 16 Mei, mimi na wenzangu wengine saba tumeshtakiwa kwa madai ya kuingia kijinai katika eneo la kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Wilaya ya Tarime; kwa kufanya mkusanyo haramu katika eneo hilo; na kwa kuwazuia mganga wa Hospitali hiyo na askari polisi kufanya uchunguzi wa miili ya marehemu Emmanuel Magige, Chacha Ngoka, Chawali Bhoke na Mwikwabe Marwa waliouawa na Jeshi la Polisi. Makosa yote matatu yanadaiwa kutokea mnamo majira ya saa nne usiku wa tarehe 23 Mei 2011."


  Kuhusiana na Mbunge Matiko, Lissu alidai kwamba Mbunge huyo wa Viti Maalum hakabiliwi na mashtaka yoyote mahakamani kwa jambo au kosa lolote lile.

  "Inaelekea Spika wa Bunge alitoa uamuzi wake huo bila hata kuuliza au kupewa taarifa sahihi kuhusu masuala ya mauaji ya Tarime na kesi iliyofunguliwa dhidi yangu na wenzangu. Hii ni hatari sana kwa uendeshaji bora wa Bunge kama Spika ambaye ndiye kiongozi mkuu wa Bunge atakuwa anatoa maamuzi ambayo hana taarifa sahihi juu yake. Sio tu mijadala inayohusu masuala muhimu kwa umma na ambayo yanatakiwa kujadiliwa Bungeni itazuiliwa kwa hoja zisizozingatia Kanuni za Kudumu za Bunge, bali pia hadhi na heshima ya Bunge na ya Spika mwenyewe itashuka kwa vile wananchi wataona kwamba Spika anafanya maamuzi kwa lengo la kuwakingia kifua mawaziri na Serikali ili wasiwajibishwe Bungeni. Hii ikitokea itakuwa ni hatari sana kwa demokrasia yetu ya kibunge."


  Mheshimiwa Lissu alidai kwamba hii si mara ya kwanza kwa Spika Makinda kutoa uamuzi ulioonekana kumkingia kifua Waziri Mkuu wakati wa Kipindi cha Maswali kwa Waziri Mkuu. "Itakumbukwa kwamba wakati wa Mkutano wa Pili wa Bunge la Jamhuri uliofanyika mwezi Februari mwaka huu, Mbunge wa Arusha Mjini, Mheshimiwa Godbless Lema aliomba Mwongozo wa Spika kutokana na kauli ya uongo iliyotolewa na Waziri Mkuu kuhusu mauaji ya Arusha. Badala ya kutoa mwongozo alioombwa, Spika wa Bunge alimkemea Mheshimiwa Lema na kumtaka athibitishe kauli yake juu ya uongo wa Waziri Mkuu.

  Hata hivyo, Lema alipotoa uthibitisho wake Spika Makinda alizima mjadala huo kwa kukalia uthibitisho wa Mheshimiwa Lema. Hadi leo Watanzania hawajaambiwa chochote juu ya jambo hilo."
  Mheshimiwa Lissu alisema kwamba vitendo hivi vya Spika vinakiuka Kanuni za Kudumu za Bunge.

  "Kwa mujibu wa Kanuni hizi, Spika wa Bunge ana mamlaka makubwa sana kimaamuzi. Hata hivyo, Spika hawezi akaendesha Bunge kama anavyoona yeye binafsi. Anatakiwa kuzingatia kanuni. Na kanuni kuu anayotakiwa kuizingatia muda wote ni kanuni ya 8 inayomtaka kuendesha shughuli za Bunge na "kutoa maamuzi kwa haki, uadilifu na bila chuki wala upendeleo wowote, kwa kuongozwa na Katiba, Sheria za nchi, Kanuni hizi, Kanuni nyingine zilizopo, maamuzi ya maspika wa Bunge waliotangulia na pia kwa kuzingatia uzoefu pamoja na mila na desturi za mabunge mengine yanayofuata utaratibu wa kibunge unaofanana na unaofuatwa na Bunge la Tanzania."

  Kuhusiana na hatua wanazotazamia kuchukua dhidi ya uamuzi wa Spika Makinda wa kukataza maswali yao, Mheshimiwa Lissu alisema kwamba watapeleka malalamiko yao kwa Kamati ya Kanuni za Kudumu za Bunge ili uamuzi wa Spika uchunguzwe na Kamati hiyo na kutolewa uamuzi.

  "Kwa bahati nzuri, uamuzi Spika kuhusiana na jambo lolote sio wa mwisho kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu za Bunge letu. Pamoja na kwamba tusingependa kufanya hivyo, lakini kuuachia uamuzi potofu wa Spika wa Bunge usimame itakuwa ni kuweka precedent ya hatari kwa Bunge letu kwani uamuzi huo ukiachwa bila kupingwa unaweza kutumiwa kwa mijadala mingine kwa siku zijazo. Ili kuepuka hili, inabidi tumpeleke Mheshimiwa Spika kwenye Kamati ya Kanuni za Kudumu za Bunge ili uamuzi wake ukajadiliwe na kutolewa maamuzi ya haki. Kazi ya kuandaa malalamiko hayo itakamilika baada ya muda mfupi kwani vielelezo vyote muhimu tayari vimekwishapatikana."


  --------------------------------------------------------------
  Tundu A.M. Lissu (MB.)
  MNADHIMU MKUU, KAMBI RASMI YA UPINZANI

   
 2. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #2
  Jun 17, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,312
  Likes Received: 5,598
  Trophy Points: 280
  Kweli kabisa amewekwa pale sio kwa maslahi ya taifa hapana kwa maslahi ya mafisadi wenzake!!anatia aibu kila kitu wakianzisha wapinzani anakipinga tu....huyu wala hana demokrasia maana anajuaa vilaza wenzake hawawezi kutoa majibu sahihi kaama issue ya Lema alivyomuaibisha PM!!wote hao vilaza hakuna afadhali
   
 3. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #3
  Jun 17, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,507
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  ni wazi kabisa kuna walakini kwenye uendeshaji wa bunge anaofanya madame speaker! ukiangaia bunge sasa, mwenyekiti jennister mhagama anaweza kudhibiti fujo za wanamagamba kuliko hata spika!
   
 4. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #4
  Jun 17, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Wembe ni ule ule kukomaa na spika maana anapendelea sana wazee wa magamba nataka barua kama izi zifike ata mia ili iwe fundisho kwake na waliomtuma
   
 5. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #5
  Jun 17, 2011
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Kuna watu ni wagonjwa wa akili ktk ofisi za umma ! Damn !
  Sielewi Kama kuna mwenye uwezo wa uongozi ktk ccm , huyu mama kafilisika kiakili,
  rejea kufunga kwake barabara, kauli ya Mzee Sitta kuwa mama mkurupukaji, Hovyo huyu mtu.
   
 6. s

  sem2708 JF-Expert Member

  #6
  Jun 17, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 3,093
  Likes Received: 505
  Trophy Points: 280
  Shame on her,historia itakuhumu mama makinda...hautakuwa na lolote la kujivunia katika uzee wako.
   
 7. Mohamedi Mtoi

  Mohamedi Mtoi R I P

  #7
  Jun 17, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,326
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 0
  Bunge limemshinda Makinda kwa kuliendesha kwa kulinda maslahi ya chama. Binafsi nafurahi maana ni ishara ya anguko.
   
 8. itnojec

  itnojec JF-Expert Member

  #8
  Jun 17, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 2,191
  Likes Received: 223
  Trophy Points: 160
  kudadeki, jamaa ni gurudumu haswaaa la mapinduzi.
   
 9. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #9
  Jun 17, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  hii ishikiwe bango kila anapofanya madudu atapagawa zaidi na kuharibu
  huyu spika ni mtu wa jaziba hivyo ni rahisi kutengea na wananchi wakaona
  yeye anafanya hivyo kulipa fadhila kwa kupewa kiti
  dawa kila anapochema elimu kama hii inatolewa kwa umma ili kujua ni kanuni gani zimevunja
  ataelewa tu
   
 10. Mkiliman

  Mkiliman JF-Expert Member

  #10
  Jun 17, 2011
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 957
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Nakubali kuwa Madam Speaker anapendelea sana hadi anapitiliza, tangu issue ya Lema hata jana nilichek hiyo na baada ya kuona mpango wa spika sio niliamua kuachana na hilo bunge lao. Spika anafikia hatua anamwambia waziri kuwa jibu au usijibu,au hata jibu kwa kifupi! huo ni uzuzu wa madaraka na kulinda maslahi mfu,ukweli namchukia sana spika MAKINDA,hayupo huru hata kidogo.
   
 11. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #11
  Jun 17, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,102
  Likes Received: 22,142
  Trophy Points: 280
  Lissu kama mwanasheria anashangaza sana. Sasa mara aseme yeye yuko mahakamani kwa kesi inayohusu hao waliouiliwa Nyamongo halafu alaume Spika hakutenda haki kuzuwia yasiongelewe. Hivi ananini huyu? Ili mradi alalamike tu?

  SI asuse kama anaona hatendewi haki? Asuse na kwenda mahakamani pia (Spika sikasema yuko nje kwa dhamana? Au alidanganya hapo Spika). Lissu susa kwenda mahakamani halafu muulize Mbowe zile siku mbili alilaa kitandani? Sakafuni au juu ya desk? Alipokaidi kwenda mahakamani?
   
 12. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #12
  Jun 17, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Hiki ndicho nilichokuwa nakisubiri kwa muda mrefu.
   
 13. M-mbabe

  M-mbabe JF-Expert Member

  #13
  Jun 17, 2011
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 4,988
  Likes Received: 3,737
  Trophy Points: 280
  Statement ya Lissu ni nzuri sana....I mean kwa context ya umaamuma wangu.
   
 14. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #14
  Jun 17, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  safi sana,lazima tuwe na mwendo kama huu. viva Tundu Lisu, viva Chadema!!!!!!!!!!!!!!!!!!, nchi hii ni yetu sote
   
 15. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #15
  Jun 17, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Toka mwanzo mwonekano wa spika huyu ulinitia mashaka. Anaonekana kamezeshwa mambo na chamj cha mkuu wa kaya, lengo lake ni kuua mageuzi. Aibu sana kwa bunge letu! Nguvu ya umma itashinda!
   
 16. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #16
  Jun 17, 2011
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Usikurupuke. Soma uelewe kilichoandikwa sio kuanza kutuletea tafsiri zako mfu hapa!!! Aaah, sorry nimesahau kwamba huko kazini, unatetea unga wa watoto!!! Kila la kheri.

  Tiba
   
 17. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #17
  Jun 17, 2011
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Pamoja na kumpa heshima yake kubwa kama mama na mzazi; Mh. Spika Anna Makinda anajivunjia heshima yake kama kiongozi na kulivunjia heshima Bunge kwa mambo kama haya yanayoongelewa ya kupindisha pindisha mambo alimradi tu amependelea upande fulani.

  Badala ya kumkumbuka kama mwanamama wa kwanza wa kuliongoza Bunge katika Taifa letu, tutamkumbuka kama mwanamama wa kwanza kupindisha pindisha kanuni na sheria kwa kuvuruga mijadala bungeni. Inasononesha!
   
 18. HOYANGA

  HOYANGA Senior Member

  #18
  Jun 17, 2011
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 180
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  teh! Tehe!
   
 19. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #19
  Jun 17, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  barua haina hata paragraph jamani??? aisee.......

  aniwei, spika Makinda ni reflection ya uongozi wa CCM kwani huyo ndiye waliyemuona cream, she is the best speaker CCM can provide at the moment, tutafanyaje sasa wakati Mama Makinda uwezo wake ndio huo

  Kwa CCM yeye ni cream of the crop!! aisee.....
   
 20. luvcyna

  luvcyna JF-Expert Member

  #20
  Jun 17, 2011
  Joined: Feb 24, 2009
  Messages: 1,441
  Likes Received: 1,034
  Trophy Points: 280
  naomba tuelimishane kidogo kuhusu hii kamati ya kusimamia kanuni za kudumu ya bunge, wahusika wanapatikanaje? tusije tukawa tunazunguka round about...ni vyema tukatizama indepency yao imekaa vipi kabla ya kutegemea maamuzi yao
   
Loading...